Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata Simba walifanya makosa piaviongozi wa simba walitakiwa wamfungulie kessy shauri katika mahakama ya michezo, Kessy alifanya makosa lakini sio kessy peke yake hata Yanga na TFF pia walifanya makosa na hii yote inasababishwa na ubabaishaji wa Tff na Yanga ambao kwa muda mrfu wamekuwa wakivunja sheria na kanuni za michezo.Yanga kwa kujua wamefanya makosa hawakuthubutu kumchezesha kwenye michuano ya Caf baada ya kuonywa ila kwa sababu wanajua Tff huwa hawafanyi kitu juu yao wameamua kumchezesha kweny michuano ya ligi kuu
Wee unaona sawa mtu kama Kessy kudaiwa hadi bilioni moja au milioni mia hadi mia 2?
Mana kuna hoja zingine hata ukipeleka mahakamani wanaangalia na status na income ya mshtakiwa ili wajidhihirishe vilevile mkataba wa simba hauna kasoro zozote isije kuwa kama ya kina Singano na Kaseja kuambiwa alipe milioni 200 na Yanga mpaka leo kimya ila kesi zao ziliyapa faida magazeti mengi ya michezo
akili yako haina uwezo wa kupambanua mambo usidhani ishu ya kesi iko kama unavyofikiria,manara na wenzake ndo wana mambo ya kitoto,haya mambo yameeanza kitambo sio kwa kesi tu,hizo ni figisu za mikia.
Ukiona mtu anakimbilia Court ujue ni kweli ila anajihami!Uongozi wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa katika mojawapo ya mechi zilizopita baina ya Simba na Mtibwa Sugar
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwa jazba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.
Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mahakamani kutoa ushahidi wa kile alicho-kisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.
“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.
Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.
“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.
Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.
Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.
Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.
Mbona mnalialia sana? kwani mmejipangaje?viongozi wa simba walitakiwa wamfungulie kessy shauri katika mahakama ya michezo, Kessy alifanya makosa lakini sio kessy peke yake hata Yanga na TFF pia walifanya makosa na hii yote inasababishwa na ubabaishaji wa Tff na Yanga ambao kwa muda mrfu wamekuwa wakivunja sheria na kanuni za michezo.Yanga kwa kujua wamefanya makosa hawakuthubutu kumchezesha kwenye michuano ya Caf baada ya kuonywa ila kwa sababu wanajua Tff huwa hawafanyi kitu juu yao wameamua kumchezesha kweny michuano ya ligi kuu
Labda yanga ya comoroKitakacho wapata yanga watajuta sana
Nachukia MTU MJINGA akini nukuuLabda yanga ya comoro
Kwa ujinga wako uliouandika ulitaka uachwe hivihivi kwani jf ya bba yako?Nachukia MTU MJINGA akini nukuu