Beki wa Yanga Hassan Kessy Kuburuzwa Mahakamani na Simba SC!

Beki wa Yanga Hassan Kessy Kuburuzwa Mahakamani na Simba SC!

Manara hadi leo analalamika Ngoma allimpiga kiwiko beki wa Simba,ni aibu hizi klabu kuongozwa na watu wa aina hii
 
viongozi wa simba walitakiwa wamfungulie kessy shauri katika mahakama ya michezo, Kessy alifanya makosa lakini sio kessy peke yake hata Yanga na TFF pia walifanya makosa na hii yote inasababishwa na ubabaishaji wa Tff na Yanga ambao kwa muda mrfu wamekuwa wakivunja sheria na kanuni za michezo.Yanga kwa kujua wamefanya makosa hawakuthubutu kumchezesha kwenye michuano ya Caf baada ya kuonywa ila kwa sababu wanajua Tff huwa hawafanyi kitu juu yao wameamua kumchezesha kweny michuano ya ligi kuu
Hata Simba walifanya makosa pia

1.Mkataba uliopita Simba hawakukamilisha vipengele vya kwenye mkataba

2.Simba hawakumtaka Kessy wanataka kumkomoa na hii sio kesi ya kwanza Yondani,Twite,Singano zote walishindwa
 
Wee unaona sawa mtu kama Kessy kudaiwa hadi bilioni moja au milioni mia hadi mia 2?
Mana kuna hoja zingine hata ukipeleka mahakamani wanaangalia na status na income ya mshtakiwa ili wajidhihirishe vilevile mkataba wa simba hauna kasoro zozote isije kuwa kama ya kina Singano na Kaseja kuambiwa alipe milioni 200 na Yanga mpaka leo kimya ila kesi zao ziliyapa faida magazeti mengi ya michezo

Hoja yangu haiko kwenye kiwango cha fidia. Ni TFF kuiachia hii issue hadi hivi leo. Ingemalizwa tu mapema mwenye kupata apate na mwenye kukosa aendelee na maisha mengine
 
akili yako haina uwezo wa kupambanua mambo usidhani ishu ya kesi iko kama unavyofikiria,manara na wenzake ndo wana mambo ya kitoto,haya mambo yameeanza kitambo sio kwa kesi tu,hizo ni figisu za mikia.

Ndio unapaswa kuonyesha hicho unachokiita"ukomavu" wa akili yako kwa kupambanua hoja husika badala ya kuangalia mtoa hoja ana rangi gani. Naamini umejifunza.
0
 
Hivi hili swala la kesy pia tunahitaji fedha za kigeni kulimaliza? Au tunahitaji msaada wa wamarekani na wachina?
 
Kwa mambo haya tunastahili hili....

TANZANIA FIFA ranking
Current
124
11px-Decrease2.svg.png
1 (11 August 2016)
Highest 65 (February 1995)
Lowest 175 (October 2005)
 
Hukumu ya hii maneno si ni leo?
 
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema utamburuza mahakamani beki wa Yanga Hassan Kessy kwa madai ya kuwatuhumu kumpa rushwa katika mojawapo ya mechi zilizopita baina ya Simba na Mtibwa Sugar

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kwa jazba, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema wanataka iwe fundisho kwa mchezaji huyo na wengine wenye tabia za uzushi.

Manara alisema tayari wamewasiliana na wanasheria wao na baada ya siku mbili watakwenda kumsimamisha mchezaji huyo mahakamani kutoa ushahidi wa kile alicho-kisema katika mahojiano na kituo kimoja cha redio hivi karibuni ambapo Kessy alidai anafanyiwa figisufigisu na Simba kwa vile alikataa rushwa wakati akiwa Mtibwa.

“Labda hayo yote wananifanyia kwa sababu nilikataa kuchukua rushwa nikiwa Mtibwa… ilikuwa kwenye mechi yetu na Simba wakanifuata na kutaka kunipa hela ili niwaachie wasifungwe mimi nikakataa,” alisema.

Aidha Manara alisema mbali na klabu, yeye binafsi pia atamburuza beki huyo mahakamani akimtaka amlipe Sh bilioni moja kama fidia kutokana na kumtamkia maneno yasiyostahili.

“Mimi binafsi nataka kwenda mahakamani na klabu pia itampeleka huko, tunataka atupe ushahidi wa maneno yake kuwa tulitaka kumpa rushwa akakataa, tunataka iwe fundisho kwa wengine,” alisema.

Alisema lakini kabla ya kwenda mahakamani wanasubiri kwanza hukumu ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji itoe jibu kuhusiana na ushahidi wao dhidi ya mchezaji huyo aliyevunja mkataba.

Alisema wanachotaka ni Kamati hiyo itende haki na ikiwa itashindikana kwa kile wanachotaka, basi watakwenda Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupeleka ushahidi juu ya kitendo cha mchezaji huyo kujiunga na Yanga kabla ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake hiyo ya zamani.

Manara alisema Yanga inatakiwa kupokwa pointi tatu baada kumchezesha mchezaji huyo katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon, wakati wakijua kuwa suala la mchezaji huyo halijamalizika bado. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania jana (TFF) Kamati ya Sheria na Hadhi kwa Wachezaji itatoa hatima ya mchezaji huyo mwishoni mwa wiki hii.
Ukiona mtu anakimbilia Court ujue ni kweli ila anajihami!
 
viongozi wa simba walitakiwa wamfungulie kessy shauri katika mahakama ya michezo, Kessy alifanya makosa lakini sio kessy peke yake hata Yanga na TFF pia walifanya makosa na hii yote inasababishwa na ubabaishaji wa Tff na Yanga ambao kwa muda mrfu wamekuwa wakivunja sheria na kanuni za michezo.Yanga kwa kujua wamefanya makosa hawakuthubutu kumchezesha kwenye michuano ya Caf baada ya kuonywa ila kwa sababu wanajua Tff huwa hawafanyi kitu juu yao wameamua kumchezesha kweny michuano ya ligi kuu
Mbona mnalialia sana? kwani mmejipangaje?
 
nasikia tff imehairisha hukumu ya hii shauri la kessy adi mwisho wa mwezi!
 
Back
Top Bottom