Ben Msuya: Askari Mtanzania aliyepata kuongoza Uganda

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Ni Maj.Gen.Benjamin "Ben" Msuya wakati huo akiwa na cheo cha Lt.Col.

Ndiye aliyeongoza kikosi vya JWTZ kilichotwaa jiji la Kampala.

Huyu ndiye aliyelazimika kulidhibiti jiji la Kampala na Ikulu ya Uganda wakati akisubiri kuwasili Raisi mpya wa Uganda, Prof.Yussuf Kironde Lul

Watanzania hatuna habari na shujaa huyu, lakini gazeti la Monitor la Uganda walimtafuta na kufanya naye mahojiano.

Soma hapa chini.



Chanzo: Musuya: The Tanzanian general-- who ruled Uganda for three days - Special Reports

cc Manyerere Jackton, Pasco, Ben Saanane, ZeMarcopolo, Mag3, Chademakwanza, Mzee Mwanakijiji, Echolima, Nguruvi3, Ritz
 
Wana siasa ambao hawajaifanyia lolote nchi hii ndiyo wanaongoza kufaidi keki ya Taifa!

Mafao ya akina Zitto,Kafulila,Makamba,Ridhiwani,Mnyika,Lema na wengineo ni MAKUBWA zaidi ya nashujaa kama Brig Msuya na RIP Brig Lupembe

Inauma sana kwa kweki!
 
Rais Pieere Buyoya haji kumsahau huyo alipojitia kuleta za kuleta kwa Tanzania alishitukia kikosi cha makomandoo wakiongozwa na Msuya kimeshatua Ikulu BUJUMBURA aliruka na ndege mbio kupiga magoti Tanzania kwa raisi kuomba msamaha kuwa amekoma harudii choko choko tena
 

Safi mkuu,alifanya choko choko gani??
 
Mkuu hebu dadavua hapo
 
Mwaka 2009 kituo cha TBC walifanya documentary ya major general MSUYA walimtembelea nyumbani kwake,aliongea vitu vingi sana kuhusu vita ya Kagera ila kikubwa ninacho kumbuka alisema walifanikiwa kumthibiti IDD AMIN ila walisubiri amri ya kumua kutoka kwa amir jeshi mkuu Nyerere ambaye aliwakataza wasimdhuru iddi amin, wamwache atoroke,kwa hasira wale majemedari wa kikosi cha mbele waliyapiga magari ya walinzi wake na kuwaua ila wakaacha gari la iddi amin na akakimbia.

Pia walihojiwa mashujaa wengine kama Msuguri,tumainel kiwelhu pamoja na balozi mahiga ambaye alikuwa mkuu wa mafunzo usalama wa taifa,pamoja na RSO wa mikoa ya mwanza na kagera ambao walitoa mchango mkubwa kwenye vita ya Kagera.
 

Kwa hiyo Idd Amin hakutoroka ila alitoroshwa na makamanda, Hii ni heshima kubwa sana kwa Taifa.

Halafu leo kuna wapuuzi wachache kwa kupiga blabla kwenye majukwaa ya kisiasa wanajiita Wazalendo.

Inabidi lipite somo la kutosha kuhusu neno Uzalendo naona linatumika isivyo.!
 
Kuna huyu capt:robert wa mapinduzi mfu ya 1983&84 huwa akianza kuelezea harakati za hii vita umaweza kubaki mdomo wazi!!
--hasa pale ilipotumika nguvu ya ziada toka kwa sir god#
#msuguli ,msuya na komando john nyerere ilikuwa sehemu ya kivutio kikubwa kwa kila mwanajeshi…
 
Tatizo kubwa sana ambalo lilisababisha watu wengi sana wasiweze kuandika au kutoa habari hasa ni UELEWA katika jambo hili wengine waliona wakiandika au kuelezea chochote kuhusu Vita vya Kagera kunaweza kuhatalisha usalama wa Taifa kitu ambacho si kweli Jambo lingine ambalo wengi walihisi na kuhofu kuwa kandika au kutoa maelezo yoyote kuhusu tukio lolote la kijeshi ni sawa na kuuweka usalama wa Taifa matatani maana msemaji wa Jeshi ni Jeshi lenyewe.

Pia Jeshi lenyewe halikuwa na utamaduni wa kuweka kila kumbukumbu ya askari wake wadogo kwa wakubwa wazi(Public) hii pia imechangia kiasi kikubwa sana mashujaa wetu wengi walipopoteza maisha yao jamii kwa ujumla iliwasahau kabisa sababu hakuna kumbukumbu zao kwenye tovuti ya JWTZ hata uki-Google huwezi pata ingawaje majeshi mengine duniani huwa yana utamadumu wa kuweka kumbukumbu kwenye tovuti zao.
Mkuu JokaKuu unajua vita ya Kagera tumekosa uhoondo mkubwa kwasababu ya makamanda wetu wengi hawakutaka kuandika uzoefu wao katika vita hiyo kibaya zaidi wengi wameshatangulia mbele ya haki.
 
Last edited by a moderator:

Umeanza vyema umemaliza kwachuki
 
Mkuu JokaKuu unajua vita ya Kagera tumekosa uhoondo mkubwa kwasababu ya makamanda wetu wengi hawakutaka kuandika uzoefu wao katika vita hiyo kibaya zaidi wengi wameshatangulia mbele ya haki.

Kweli kabisa
 
Last edited by a moderator:
bora wameenda huko kwani deni la taifa lingezidi kupaa juu sana kama wangekuwepo nchini
 

Vita inamambo mengi mkuu
 
Halafu majitu kama Chenge yanaiba tu wakati waliosotea nchi hata hatuwafahamu!!! Tatukana hapa nipigwe ban bure kwa hasira🙁🙁
 

Mkuu huyu John Nyerere (RIP) aliyefariki hivi majuzi alikuwa komandoo!? Nasikia na ndugu yao mwingine alifia vitani. Dah! Kweli Mwl. alikuwa Jemadari, kwake hakuna cha mtoto wala nini linapokuja suala la ulinzi wa taifa. Nikisikia neno "Amiri Jeshi Mkuu" always picha ya Mwl. inanijia.

Sio leo wengine wako pale kwa favor tu kwa sababu Baba naye alikuwa mtu mzito huko Serikalini au Chamani. Nasikia kuna mmoja alitoroka (alikimbia) JKT lakini leo ni mtu mzito sana sana huko juu na kibaya (kizuri?) zaidi pia anautamani u-Amri Jeshi Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…