Hii kitu acha kabisa. Nakumbuka ilikua ni kipindi cha rais Mkapa, rais hakutaka kujishughulisha na zile chokochoko huvyo akawaambia vijana wafanye wanachoona kinafaa ndani ya muda sahihi.
Burundi walifanya sana chokochoko, mpaka askari wa mpakani wakaamua kujibu ingawa kwa umakini sana.
Baada ya kujibu mapigo, Buyoya alilalamika kuwa majeshi ya Tanzania yamevamia kambi za kijeshi nchini Burundi na kuua askari wao. BBC nao wakaitangaza sana hii habari lakini ushahidi ulikosekana.
Kilichotokea:
Ni kweli vijana wa Tanzania waliingia Burundi na kuvamia kambi zilikua zinatumika kuandaa mpango vita dhudi ya Tanzania, vijana waliua askari wakateka na silaha kadhaa na zile maiti waliondoka nazo hivyo na kufuta kila aina ya ushahidi utakaothibitisha uvamizi.
Buyoya alilalamika sana na BBC wakaitangaza sana. Lakini haikuthibitika.
Issue ikaingia hadi bungeni, Kikwete ambaye back then alikua waziri wa mambo ya nje akasikika akiongea bungeni kuwa "wakipiga risasi mbili, sisi tutajibu saba".
Nakumbuka safari hii vijana walisali kabisa ili wasikie angalau mlio wa pancha ya gari au baiskeli ili wasingizie risasi na wao waingie kazini. Sara zao zikajibiwa, kwani Buyoya aliingiza majeshi yake ndani ya umbali ambao kisheria inahesabika kuwa ni uvamizi dhudi ya nchi nyingine, ingawa bado ilikua ni nchini mwake.
Hali ya hewa usiku ule ilikua ni ya ukungu fulani hivi na giza nene, hali hiyo vijana waliitumia kama camouflage/concealment kuingia ndani ya Burundi na maeneo yake muhimu. Kulipopambazuka tayari the heart of Burundi ilikua kwenye viganja vya vijana. Kumbuka maneuver inafanyika huku nchini hakuna tena anayeongelea swala hilo hata watanzania wanalisikia tu kupitia BBC huku vyombo vya ndani vikiwa kimya, viongozi nao kimya.
Buyoya akawa amechanga nyikiwa maana alihakikishiwa kuwa maneuver ile ilifanywa na vija kama defensive tu wala haikua order toka juu (Mbali na uhasama uliokuwepo, Buyoya alikua na tabia ya kwenda mpakani na kufanya mazungumzo tu ya kawaida na vijana wetu, tuseme walimzoea na pia alikua ni mwanajeshi, ingawa every time alipokuwa akienda alikua heavily guarded). Hali hiyo ilimchanganya kabisa Buyoya akajikuta yupo at the cross road, hakuwa na ujasiri wa kumvaa Mkapa (Mkapa hakua mtu wa kuingilika kijinga) akalazimika kupitia kwa Nyerere.
Yaliyobaki na yaliyofuata ni historia. Hiyo ndiyo ilikua Tanzania ya Watanzania.
Tanzania ya sasa ikikumbwa na jaribu lolote naomba nisiwe mtabiri. Lakini ukiniuliza Tanzania hii na ile nitakwambia bila kupepesa kuwa never put your money on this Tanzania.