Ben Msuya: Askari Mtanzania aliyepata kuongoza Uganda

Ni kweli; Col Ben Msuya ndiye aliyeingoza batallion iliyoteka Kampala. Batallion yake (sikumbuki namba KJ....) ilikuwa sehemu ya Brigedi iliyokuwa ikiongozwa na Brigadier Marwa (Kambale) wakati huo.
 
Mkuu nakufagilia kwa kuwa na rational thinking.
Wakati wa vita tulikuwepo na hatukuenda front kwa sababu tu tayari tulikuwa tumeanza masomo vyuo viku, lakini wale wenzetu waliochelewa kwenda JKT waliishia Arua na habari zote tulikuwa nazo , kwa kile kilichokuwa kinaendelea Uganda.

Mwalimu alikuwa very tactical na he was a genius manipulator.
Kwa kupitia RTD majeshi yetu yaliishia mpakani na waliokuwa wakienda mbeke ni "wakombozi" wa nchi ya Uganda, na kina Oyite Ojok na webgine ndio walipewa full coverage ya kusonga mbele.

Si uongo Ben Msuya alikuwa hero lakini wakati huo wala hakutajwa katika harakati za kila siku za vita.
Nakuhakikishia kuwa ni BBC na stringers wake akina Tony Avirgan ndio waliomuinua Ben Msuya akiwa front, na kwa kweli yeye pamoja na vikosi vingine vilivyo kuwa vina wa flank wakati wa vita wanastahili heshima zote za kijeshi na hili lazima liandikwe vizuri kihistoria.
 
..GOOD!!

..nina hakika uta-enjoy sana vitabu hivyo.

..mimi nimesoma hicho cha Tony Avirgan na Martha Honey.

Nataka pia ninsome Waziri mwandamizi wa utawala wa Amini huyu Henry Kyemba kaongea nn kwenye kitabu chake

Sidhani kama ni kweli hizi simulizi kuwa Idd Amin alikuwa anakula nyama za watu eheheheh
 
MARINE HASSAN na JWTZ Waliandaa documentary ya zaidi ya masaa 6 kuhusu vita ya kagera ,mashujaa wote uliowataja wapo humo ndani TBC nafikiri watakuwa nayo library
 
Hii kitu acha kabisa. Nakumbuka ilikua ni kipindi cha rais Mkapa, rais hakutaka kujishughulisha na zile chokochoko huvyo akawaambia vijana wafanye wanachoona kinafaa ndani ya muda sahihi.
Burundi walifanya sana chokochoko, mpaka askari wa mpakani wakaamua kujibu ingawa kwa umakini sana.
Baada ya kujibu mapigo, Buyoya alilalamika kuwa majeshi ya Tanzania yamevamia kambi za kijeshi nchini Burundi na kuua askari wao. BBC nao wakaitangaza sana hii habari lakini ushahidi ulikosekana.
Kilichotokea:
Ni kweli vijana wa Tanzania waliingia Burundi na kuvamia kambi zilikua zinatumika kuandaa mpango vita dhudi ya Tanzania, vijana waliua askari wakateka na silaha kadhaa na zile maiti waliondoka nazo hivyo na kufuta kila aina ya ushahidi utakaothibitisha uvamizi.
Buyoya alilalamika sana na BBC wakaitangaza sana. Lakini haikuthibitika.

Issue ikaingia hadi bungeni, Kikwete ambaye back then alikua waziri wa mambo ya nje akasikika akiongea bungeni kuwa "wakipiga risasi mbili, sisi tutajibu saba".
Nakumbuka safari hii vijana walisali kabisa ili wasikie angalau mlio wa pancha ya gari au baiskeli ili wasingizie risasi na wao waingie kazini. Sara zao zikajibiwa, kwani Buyoya aliingiza majeshi yake ndani ya umbali ambao kisheria inahesabika kuwa ni uvamizi dhudi ya nchi nyingine, ingawa bado ilikua ni nchini mwake.
Hali ya hewa usiku ule ilikua ni ya ukungu fulani hivi na giza nene, hali hiyo vijana waliitumia kama camouflage/concealment kuingia ndani ya Burundi na maeneo yake muhimu. Kulipopambazuka tayari the heart of Burundi ilikua kwenye viganja vya vijana. Kumbuka maneuver inafanyika huku nchini hakuna tena anayeongelea swala hilo hata watanzania wanalisikia tu kupitia BBC huku vyombo vya ndani vikiwa kimya, viongozi nao kimya.
Buyoya akawa amechanga nyikiwa maana alihakikishiwa kuwa maneuver ile ilifanywa na vija kama defensive tu wala haikua order toka juu (Mbali na uhasama uliokuwepo, Buyoya alikua na tabia ya kwenda mpakani na kufanya mazungumzo tu ya kawaida na vijana wetu, tuseme walimzoea na pia alikua ni mwanajeshi, ingawa every time alipokuwa akienda alikua heavily guarded). Hali hiyo ilimchanganya kabisa Buyoya akajikuta yupo at the cross road, hakuwa na ujasiri wa kumvaa Mkapa (Mkapa hakua mtu wa kuingilika kijinga) akalazimika kupitia kwa Nyerere.
Yaliyobaki na yaliyofuata ni historia. Hiyo ndiyo ilikua Tanzania ya Watanzania.
Tanzania ya sasa ikikumbwa na jaribu lolote naomba nisiwe mtabiri. Lakini ukiniuliza Tanzania hii na ile nitakwambia bila kupepesa kuwa never put your money on this Tanzania.
 
Sio muafaka kutamani madaraka ndani ya ccm ya sasa hasa ukikumbuka kuwa kuna maisha baada ya kifo na Mungu atahukumu kwa haki. Hasa tukikumbuka ' ni rahisi ngamia kupenya......... kuliko..........
 
Yaani hivi inawezekana kweli Nyerere atutie kwenye umaskini mkubwa kisa kumrudisha madarakani Obote? Sidhani aiseeee
 
Aiseeeee Sasa Buyoya alikuwa Na Maslahi gani Na Tanzania mpaka aanze chokochoko.Ila Askari wetu nadhani walitumia ujuzi wa Hali ya juu Na umakini mkubwa
 
duh?
 
Umeharibu pale ulipomalizia uzi wako na malawama. Yaani umeboa balaa Mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja kabla vijana hawaja jivinjari Mkuu wa Majeshi wakati ule (Kama sikosei Mboma?) alikwenda kukagua hali ya mpaka. Mwisho wa Ziara akasema hali ya mpaka ni shwari hakuna tatizo na anaondoka kwenda nyumbani kwake kwa mapumziko. Usiku vijana wakafanya yao. Ilikuwa JWT au TPDF

Ilikuwa anzania ! si hii ya ''Vijana kusafisha barabara'' . Sad

JokaKuu
 
..Nakusanya taarifa za Lt.Gen.Imran Kombe, Maj.Gen.Muhidin Kimario, na Brig.Ahmed Kitete na michango yao ktk vita vya Kagera.
Mkuu Project imefikia wapi

Ahsante sana ulimtendea haki Maj Gen Msuya. Pumzika kwa amani shujaa
 
Mkuu Project imefikia wapi

Ahsante sana ulimtendea haki Maj Gen Msuya. Pumzika kwa amani shujaa

..Brig.Ahmed Takadiri Kitete " kamanda super sonic " alikuwa hajulikani nimemuanzishia uzi hapa JF.
 
Nyuzi kama hizi ndio vijana walitakiwa waje huku wajifunze na kuhoji ila huwezi waona huku wamebaki kwenye nyuzi za kula tunda kimasihara tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…