Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya andiko la JFKUMBUKIZI kuhusu ahadi mbalimbali zilizotolewa na Viongozi tofauti kuhusu ahadi za kushughulikia changamoto ya taasisi au vituo vya Afya kugoma kutoa miili ya Watu kutokana na madeni ya huduma walizokuwa wanapatiwa, maoni yamekuwa mengi kutoka kwa Wananchi.
Ahadi kwamba ndugu na jamaa hawatakiwi kuzuiwa kuchukua mwili hizo zilianza kutolewa tangu Mwaka 2019, tangu wakati huo kumekuwa na matamko mbalimbali ambayo utekelezaji wake umekuwa mgumu.
Kusoma zaidi kuhusu hoja hiyo bofya hapa Samia aahidi kuondoa zuio la maiti hospitalini wakati Waraka wa Serikali wa 2021 tayari ulipiga marufuku
MAONI YA WADAU...
Moja wa waliotoa maoni ni Msanii Ben Pol ambaye ameandika: Nikiwa kidato cha 4 mwaka 2007, Kaka yangu wa kwanza Michael Paul (RIP) alifariki, Mwili ulizuiliwa Muhimbili na familia yangu haikuweza kulipia gharama alikaa almost wiki mbili, leo hii ni miaka 18 baadae…. Sio mchezo.”
Nikiwa kidato cha 4 mwaka 2007, Kaka yangu wa kwanza Michael Paul (RIP) alifariki, Mwili ulizuiliwa Muhimbili na familia yangu haikuweza kulipia gharama alikaa almost wiki mbili, leo hii ni miaka 18 baadae…. Sio mchezo.
Ishu sio kuzuia ishu ni nani atalipia hizo gharama alizotumia marehemu kwenye matibabu? Mgonjwa anaweza kulazwa ICU kwa mwezi na kila siku ni 50k hadi 100,000/-…bahati mabaya akafa…mwili utaachiwa, na ndugu hawatarudi tena hospitali kulipia gharama. Politics aside, nani analipia hizi gharama?
Kuna tofauti kati ya tamko na sheria labda litawekwa kisheria.
This always is so political, tunahitaji Suluhisho la kudumu ambalo ni Bima ya afya kwa wote yenye ruzuku kubwa ya serikali ndani yake... Kama kila mgonjwa anayelazwa angekuwa anatibiwa kwa bima, haya matamko hewa yasingekuwepo... Ifike wakati tuhame kwenye drama twende kwenye actions.
Kule Arusha mawiki yaliopita boda boda alikufa Hospital ikadai ili maiti itoke wanatakiwa kulipa Laki 900,000 ndugu za Marehemu wakaja juu wakasema wakitoa laki 9 basi wapewe na Maiti nyingine 3 😂 maana mgonjwa wao ile anafikishwa tu Hospitali akafariki bila kupata matibabu sasa Laki 9 za nn hospital inadai??😂😂😂😂😂.
Kifuatachoa Huna Hela hupati huduma.