Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Sio wote hatujui chochote kumhusu mjenzi huyo wa kizazi kipya cha wanasiasa chipukizi hapa Tanzania. Yupo anaejua alipo. Anayejua alipo yupo miongoni mwetu, na kila tunachozungumza kumhusu mwendazake huyu anakiona, yupo! Yupo anasonya kwa kuwa tu tumenyimwa uwezo wa kumjua ila yupo.
Huenda anaingia na makanisani kusali na kuwahubilia wengine lakini hajutii kuondoa roho ya mtu mwenye ndoto kama Ben. Na huenda anajitambulisha kama mtumishi lakini amesahau roho za watu ni sawa na kubeba furushi la laana kichwani.
Huenda ni kijana mdogo tu lakini namhakikishia hii laana itamla yeye na uzao wake wote, kama asipotubu na kujiweka wazi mbele ya Watanzania. Atubu na atueleze tu kokote ambako walimuweka huyu kijana asiye na hatia.
Tujue tu kwamba alikufa au amefungiwa sehemu ambayo hakuna mchana wala usiku, laana itamtafuna sana kama asipotubu hadharani.
Roho ya Ben ipo miongoni mwetu inazunguka haitakuacha salama wewe shetani ambae huenda ulikuwa na madaraka makubwa na sasa hauna tena. Laana itakutafuna wewe ibilisi ambae huenda ukiingia kanisani unalia sana machozi lakini vishindo vya roho ya Ben havitakuacha salama!
Jitahidi utubu, jitahidi sana kuomba toba kinyume chake kuna giza zito sana mbele yako. Tuambie ukweli Ben ulimzika wapi, ulimtupa wapi au anaishi wapi?
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu u aonywaye mara nyingi akishupaza shingo atavunjika na hatapata dawa.