Baada ya kunyanyasika vilivyo nchini Rwanda madereva wa malori wa Tanzania wamejichukulia sheria mkononi kuyazuia malori yote kutokea Rwanda kuingia nchini.
Inasemekana baada ya Rwanda kuudhibiti ugonjwa wa Corona vilivyo nchini mwao, kitisho pekee kwa sasa kimebakia kuwa kutokea kwa wageni wanaoingia nchini mwao.
Katika hili inasemekana madereva wa malori kutokea nje wamekuwa ndiyo kitisho kikubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa madereva kadhaa tokea Tanzania wamepatikana na virusi hivyo kwenye kuingia huko. Kutokana na hali hiyo, inasemekana Rwanda imebadilisha utaratibu wa malori kuingiza mizigo na sasa kuwataka madereva wa kutoka nje (Tanzania) kuishia mpakani. Utaratibu mpya unawataka madereva walioko (salama) ndani ya Rwanda pekee kuyafikisha malori Kigali na kuwarudishia mpakani.
Utaratibu wa ajabu kabisa. Nani atamwamini mtu asiyemjua na gari lake? Kujibu hilo madereva wa Tanzania nao wamechukua hatua zao na kuanzia jana inasemekana hali huko ni tete. Hakuna lori kutoka Rwanda wanaloliruhusu kuingia nchini. Vinginevyo nao wanawataka waishie mpakani kwa hali ile ile kama inavyotakiwa kwa wetu kufanya.
My take: Serikali inabidi kuingilia kati haraka iwezekanavyo na kuchukua hatua. Yawezekana hawa ndugu tuliowaachia mpaka wazi kwa kuwahurumia ya kwamba watataabika mno, huruma yetu hawaihitaji kabisa!
Kudos madereva wetu si mbaya mkuki kwa nguruwe kuwa ni ule ule kwa binadamu pia.