Benard Membe: Trump alishindanishwa na wenzake na akashinda kugombea awamu ya pili

Huyu ni mwanaCCM mwoga, maneno mengi vitendo sifuri. Akachukue form then ijulikane wamemtosa waziwazi kuliko hizi kelele za mitandaoni. Zaidi ya hapo anachofanya maigizo ya kuwateka wadanganyika.
 
BM amepost ujumbe katika akaunti yake ya Twitter inayodai kuwa Trump amepitishwa na Rebulican kugombea Urais wa Marekani baada ya kushindanishwa na wanachama wenzake watatu. BM amesema kuwa Marekani hawana utamaduni kwa kukataza na kubeza wagombea wengine kama sisi Watanzania.

Siku za hivi karibuni BM tena alikitaka Chama cha Mapinduzi kumsafisha kwa kile alichodai kuwa ameonewa kufukuzwa uanachama. Amesema kuwa anataka kusafishwa mapema ili aweze kuchukua fomu ya kuomba kugombea katika nafasi ya Rais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu. BM alisema iwapo hatasafishwa, basi lolote linaweza kutokea kwani muda uliobaki kuelekea uchaguzi Mkuu bado ni mrefu, kauli iliyotafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa amelenga kuonyesha kuwa ana lengo la kuhamia kwenye moja ya vyama vya upinzani na hasa ACT-Wazalendo.

Anachojisahulisha huyu anayejiita Mwanadiplomasia mbobevu ni kuwa Tanzania si Marekani. Tanzania kama nchi huru haina haja ya kuiga kila kinachofanywa na nchi nyingine. Na hilo limejidhihirisha wazi katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona, ambapo hata baada ya watu wengi akiwemo yeye BM kubeza jitihada zetu, bado Rais wetu alisimamia lile ambalo Watanzania wengi walilitaka kusimamiwa katika mapambano hayo dhidi ya Corona, BM mwenyewe amekiri kuwa corona imepungua.

Anajisahaulisha kuwa CCM imekuwa na utaratibu wa kutoa nafasi ya kugombea Urais kwa mara ya pili kwa kila mwanachama anayeshika madaraka ya Rais wa JMT. Wakati alipokuwa ndani ya mfumo hakuona kuwa utaratibu huo una shida yoyote, kwa mfano mwaka 2010 wakati JK alipopitishwa bila kupingwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa 2010 hakukosoa utaratibu huo.

Ninachokiona hapa ni kuwa huyu Mzee ameanza kuweweseka. Hadi sasa hajielewi asimamie wapi, na muda wa kuchukua fomu ndo huo unayoyoma. Sasa anaibuka na kuanza kutoa kauli zisizo na kichwa wala miguu. Kinachonishangaza kuwa bado anaishi kwenye “Fantansy World” akiamini kuwa Watanzania tunampenda sana, na tunamtegemea yeye kuleta maendeleo. Poor BM!!
 
Mhurumieni tingatinga sio akili yake mastress yamemjaa anaona giza giza tu.
 
Chama cha kijamaa chenye sera za kibepari, hivi huoni mkanganyiko hapo. Kuna maendeleo yatapatikana kupitia chama hiki kweli.
 
Mbali na katiba bado tuna sheria za kitamaduni tulizojiwekea, hizi pia ni muhimu kufuatwa.
 
Empty head, hujaona watu waliotia nia ya kugombea urais kupitia CDM, hujui kuwa mchakato wa kura za maoni bado haujafanyika ndio maana hawana jina.

Kinachoniudhi ni kuwa utalipwa 7,000 kwa upuuzi huu, mnatumia kodi za wananchi vibaya sana.
 
Katiba sio msahafu kamati kuu ya Chama imeridhia kuendelea na mgombea huyohuyo ... Huyo Membe yeye ni nani hasa mpka avunje utamaduni na makubaliano ya kamati kuu ... KUNA VYAMA VINGI AENDE ANAPOONA KUNA MFAA SI NDIO DEMOKRASIA HIYO?
Weka kopi ya barua ya ridhaa
 
Aliyemuwekea sumu Mangula mmeshampata?
Wanamjua sana tuu, Ila hakuna mwenye ubavu hata kumnyooshea kidole maana mambo yote ya chama inategemea "siku hiyo ameamkaje".
CCM imegeuka kuwa chama mdebwedo na hakuna kidume wa kusema 'su'
 
Hata sisi tunamshangaa alikuwa wapi wakati huo, lakini kama ameamua kuomba ridhaa kugombea sasa kuna ubaya gani?
 
hivi wastaafu hawewezi kumsihi atulie, maana hatujui lengo lake haswa ni kugombea au ?
 
mwambieni jiwe asubiri membe anagombea sasa

Ataongea saana lakini atashangaa muda wa uchaguzi umeisha atatulia tu.
Kama anapenda aende ACT kisha uchaguzi ukiisha wamtimue kwa kukosa nidhamu ya chama.
 
Mbali na katiba bado tuna sheria za kitamaduni tulizojiwekea, hizi pia ni muhimu kufuatwa.
Mambo ya CCM yanaenda kwa vikao.

Kikao gani kiliamua "sheria za kitamaduni tulizojiwekea" za mihula miwili miwili?
 
Ulivyomalizia hoja yako ndipo ulipodhihirisha una uwendawazimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…