Benard Membe: Trump alishindanishwa na wenzake na akashinda kugombea awamu ya pili

Benard Membe: Trump alishindanishwa na wenzake na akashinda kugombea awamu ya pili

Huyu ni mwanaCCM mwoga, maneno mengi vitendo sifuri. Akachukue form then ijulikane wamemtosa waziwazi kuliko hizi kelele za mitandaoni. Zaidi ya hapo anachofanya maigizo ya kuwateka wadanganyika.
 
BM amepost ujumbe katika akaunti yake ya Twitter inayodai kuwa Trump amepitishwa na Rebulican kugombea Urais wa Marekani baada ya kushindanishwa na wanachama wenzake watatu. BM amesema kuwa Marekani hawana utamaduni kwa kukataza na kubeza wagombea wengine kama sisi Watanzania.

Siku za hivi karibuni BM tena alikitaka Chama cha Mapinduzi kumsafisha kwa kile alichodai kuwa ameonewa kufukuzwa uanachama. Amesema kuwa anataka kusafishwa mapema ili aweze kuchukua fomu ya kuomba kugombea katika nafasi ya Rais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu. BM alisema iwapo hatasafishwa, basi lolote linaweza kutokea kwani muda uliobaki kuelekea uchaguzi Mkuu bado ni mrefu, kauli iliyotafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa amelenga kuonyesha kuwa ana lengo la kuhamia kwenye moja ya vyama vya upinzani na hasa ACT-Wazalendo.

Anachojisahulisha huyu anayejiita Mwanadiplomasia mbobevu ni kuwa Tanzania si Marekani. Tanzania kama nchi huru haina haja ya kuiga kila kinachofanywa na nchi nyingine. Na hilo limejidhihirisha wazi katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Corona, ambapo hata baada ya watu wengi akiwemo yeye BM kubeza jitihada zetu, bado Rais wetu alisimamia lile ambalo Watanzania wengi walilitaka kusimamiwa katika mapambano hayo dhidi ya Corona, BM mwenyewe amekiri kuwa corona imepungua.

Anajisahaulisha kuwa CCM imekuwa na utaratibu wa kutoa nafasi ya kugombea Urais kwa mara ya pili kwa kila mwanachama anayeshika madaraka ya Rais wa JMT. Wakati alipokuwa ndani ya mfumo hakuona kuwa utaratibu huo una shida yoyote, kwa mfano mwaka 2010 wakati JK alipopitishwa bila kupingwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa 2010 hakukosoa utaratibu huo.

Ninachokiona hapa ni kuwa huyu Mzee ameanza kuweweseka. Hadi sasa hajielewi asimamie wapi, na muda wa kuchukua fomu ndo huo unayoyoma. Sasa anaibuka na kuanza kutoa kauli zisizo na kichwa wala miguu. Kinachonishangaza kuwa bado anaishi kwenye “Fantansy World” akiamini kuwa Watanzania tunampenda sana, na tunamtegemea yeye kuleta maendeleo. Poor BM!!
 
Umetumia muda mwingi kunikashifu ukasahau kujibu swali ...CCM ni chama cha Kijamaa tangu kinaanzishwa mpka leo sasa kutoruhusu mgombea mwingine kuchukua fomu ni kitu cha kukushangaza? Ndio mana nimekupa mfano wa chama kingine cha kijamaa CPC cha china je huoni mfanano we unataka CCm iwe kama CHADEMA haiwezekani ndio mana nikakupa mfano Demokrasia ya Marekani huwezi ifananisha na Uingereza Kila nchi ina model yake ya Demokrasia vivyohivyo vyama vya siasa ...jibu hoja acha kuzungumzia watu
Chama cha kijamaa chenye sera za kibepari, hivi huoni mkanganyiko hapo. Kuna maendeleo yatapatikana kupitia chama hiki kweli.
 
Ndio maana tunashindwa kuvi run hivi vi nchi vyetu vichanga changa.

Huo ni ubabe, matusi, na kushindwa kufuata taratibu tulizojiwekea, i.e. Katiba.

KATIBA ya chama haisemi Rais lazima apewe nafasi ya muhula wa pili.

Walioshikiria dhamana za dola. jifunzeni kuheshimu mikataba ya kijamii tunayowekena, i.e. KATIBA ZETU
Mbali na katiba bado tuna sheria za kitamaduni tulizojiwekea, hizi pia ni muhimu kufuatwa.
 
Chadema hawana mgombea Hadi Sasa. Wamejipima wameona hakuna hata mmoja anayeweza kujaribu kusimama kwenye urais na JPM ndo maana wamekomaa wanamtaka Membe labda wataweza kuangalia wa kupambana na Membe.
Kama Wana mgombea wataje jina, CCM wamemtaja Magufuli.
Empty head, hujaona watu waliotia nia ya kugombea urais kupitia CDM, hujui kuwa mchakato wa kura za maoni bado haujafanyika ndio maana hawana jina.

Kinachoniudhi ni kuwa utalipwa 7,000 kwa upuuzi huu, mnatumia kodi za wananchi vibaya sana.
 
Katiba sio msahafu kamati kuu ya Chama imeridhia kuendelea na mgombea huyohuyo ... Huyo Membe yeye ni nani hasa mpka avunje utamaduni na makubaliano ya kamati kuu ... KUNA VYAMA VINGI AENDE ANAPOONA KUNA MFAA SI NDIO DEMOKRASIA HIYO?
Weka kopi ya barua ya ridhaa
 
Aliyemuwekea sumu Mangula mmeshampata?
Wanamjua sana tuu, Ila hakuna mwenye ubavu hata kumnyooshea kidole maana mambo yote ya chama inategemea "siku hiyo ameamkaje".
CCM imegeuka kuwa chama mdebwedo na hakuna kidume wa kusema 'su'
 
Eti anajifanya kidume sasa hivi! Alikuwa wapi 1995? Alikuwa wapi wakati Mkapa anamaliza awamu yake ya kwanza? Alikuwa wapi wakati JK anamaliza awamu yake ya Kwanza? Sasa hivi ndio anaiona Demokrasia?
Hata hivyo Membe anapaswa sana kumshukuru JK, Alimbeba sana, Hana uwezo.
Hata sisi tunamshangaa alikuwa wapi wakati huo, lakini kama ameamua kuomba ridhaa kugombea sasa kuna ubaya gani?
 
hivi wastaafu hawewezi kumsihi atulie, maana hatujui lengo lake haswa ni kugombea au ?
 
mwambieni jiwe asubiri membe anagombea sasa

Ataongea saana lakini atashangaa muda wa uchaguzi umeisha atatulia tu.
Kama anapenda aende ACT kisha uchaguzi ukiisha wamtimue kwa kukosa nidhamu ya chama.
 
Mbali na katiba bado tuna sheria za kitamaduni tulizojiwekea, hizi pia ni muhimu kufuatwa.
Mambo ya CCM yanaenda kwa vikao.

Kikao gani kiliamua "sheria za kitamaduni tulizojiwekea" za mihula miwili miwili?
 
Kama chama cha republican wanaruhusu huo utaratibu, aende huko akagombee urais wa marekani. CCM ipo TZ na inautaratibu wake ambao si lazima ufanane na chama kingine. Kama anateseka na muwasho wa kugombea urais wa TZ, ahamie chadomo au kile chama cha mkongoman Zitto, huko atakunwa vizuri tu na atafurahia show.
Ulivyomalizia hoja yako ndipo ulipodhihirisha una uwendawazimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom