Benchi la ufundi la Timu ya Taifa liwe bora kuliko la vilabu

Gamondi (anaejua) kampa ujuzi wa kucheza namba hii, kocha wa timu ya taifa (asiyejua) anataka ambadilishie namba, wataelewana?
Kwa mfano Mzize anacheza fowadi akitokea pembeni au mbele (9) akiwa Yanga, Dickson Job anacheza beki wa kati au kulia namba hizo hizo ndizo wanazocheza timu ya taifa. Halafu mchezaji kubadilishiwa namba na kocha timu ya taifa ni kitu cha kawaida.
 
1. Hayupo kocha wa kibongo aliyewahi walau kupata kandarasi ya kufundisha nje ya mipaka ya Tanzania...

2..Ndaragije (Mrundi) alifundisha Mbao na Azam, Moses Basena (Mganda) alifundisha Simba na kagera, Razak Siwa (Mkenya) alizi-coach Yanga & mtibwa
Chamangwana (mlawi) alifundisha Yanga nk...mbona wakwetu hawauziki nje.

3.Tofauti na kuzungumza Kiswahili makocha wetu hawana lolote la kumwongezea Dismas Novatus Miroshi anayecheza ligi kuu ya uturuki..au samatta aliyekutana na makocha bora toka Genk, Aston Villa, Royal Antwerp au Paok.

4..Makocha wazawa hatujaanza kuwatumia Leo...Tulishawaamini toka enzi za Mziray, Mkwasa, Kayuni, Kinanda,mpaka salum Mayanga, Amy Ninje au Oscar milambo...
Hatujawahi kupata achievement yeyote chini yao tofauti na cecafa challenge cup ya 1994.

5..Wewe fikiria Kocha Jemedari Said anaweza kumpa nini Himid Mao aliyecheza clubs 5 chini ya makocha tofauti tofauti pale Egypt..

6..Suala sio cheti...kama ni cheti mimi Naamini Oscar Milambo Anaweza kuwa na vyeti begi zima...kamzidi mbali hata Vicent kompany...

7.Hivi huyu Hemed Moroko aliichezea timu gani kwanza, na lini...Ana achievement zipi? Nini kinamtofautisha kaseja.

8..Ifike mahali tuache ku-politisize soka..mtu anapewa timu simply kwasabu ya kubalance Muungano.
 
kocha mzawa hatutoboi, hatuna kocha mzawa mwenye mafanikio kisoka, ni mabifu tu na wachezaji. Wenzetu wanaleta makocha wa kidunia sisi tunachukua makocha ambao hawajawahi kuchukua hata kombe la mbuzi kwenye timu zao walizofundisha.
Kwani makocha wazawa si wanatoka duniani humuhumu.... Kompany kaanzaje Leo yupo Bayern Munich!?? .... Tuendeleee la Morroco mpaka tukomeee...
 
Chibe Chibindu, Mwaikimba ....
 
Upo sahihi mkuu! Makocha wetu hawana exposure! Just imagine mchezaji kama Mzize, Job na hadhi zao wanakuja kufundishwa na Morocco kocha type ya Namungo🤣🚮
Kocha hana uwezo. Unapombadilishia mchezaji namba yake anayocheza kwenye timu yake ni kucheza kamari. Kocha anang'ang'ana Fei TOTO acheze dk 90 hata kama unaona punzi yake imekata.
 
Uko sahihi kabisa.
 
Very true ✔️
 
Hivi Kiemba hata Kama amesomea ukocha amefundisha timu gani, Julio hakuwa na timu huyo Morocco rekodi zake za ufundishaji zikoje Senegal na Morocco wanatumia makocha wazawa viwango vya makocha wao ni vya juu kabisa wanaweza kufundisha Hadi timu za ulaya.
 
Wajinga hao waendelee fungwa maisha yote
 
Kwa mfano Mzize anacheza fowadi akitokea pembeni au mbele (9) akiwa Yanga, Dickson Job anacheza beki wa kati au kulia namba hizo hizo ndizo wanazocheza timu ya taifa. Halafu mchezaji kubadilishiwa namba na kocha timu ya taifa ni kitu cha kawaida.
Kaka tumeshinda lakini tujiulize tumeshindaje? Waliosababisha tushinde ni safu bora ya ulinzi. Fei na Mudadhir zilikuwa juhudi zao binafsi. Hatuna kocha, tusije tukajichanganya na matokeo haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…