Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa mfano Mzize anacheza fowadi akitokea pembeni au mbele (9) akiwa Yanga, Dickson Job anacheza beki wa kati au kulia namba hizo hizo ndizo wanazocheza timu ya taifa. Halafu mchezaji kubadilishiwa namba na kocha timu ya taifa ni kitu cha kawaida.Gamondi (anaejua) kampa ujuzi wa kucheza namba hii, kocha wa timu ya taifa (asiyejua) anataka ambadilishie namba, wataelewana?
Kwani makocha wazawa si wanatoka duniani humuhumu.... Kompany kaanzaje Leo yupo Bayern Munich!?? .... Tuendeleee la Morroco mpaka tukomeee...kocha mzawa hatutoboi, hatuna kocha mzawa mwenye mafanikio kisoka, ni mabifu tu na wachezaji. Wenzetu wanaleta makocha wa kidunia sisi tunachukua makocha ambao hawajawahi kuchukua hata kombe la mbuzi kwenye timu zao walizofundisha.
Chibe Chibindu, Mwaikimba ....Swali zuri sana.
Lkn muulize na hili pia.
Je,umewahi kuona Tanzania kama taifa limewekeza katika KUZALISHA,KUKUZA NA KUENDELEZA VIPAJI VYA MICHEZO KWA LENGO LA MIAKA YA MBELENI KUFUZU FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA AU LA DUNIA? UNAWEZA UKAWATAJA KAMA WAPO?
Kocha hana uwezo. Unapombadilishia mchezaji namba yake anayocheza kwenye timu yake ni kucheza kamari. Kocha anang'ang'ana Fei TOTO acheze dk 90 hata kama unaona punzi yake imekata.Upo sahihi mkuu! Makocha wetu hawana exposure! Just imagine mchezaji kama Mzize, Job na hadhi zao wanakuja kufundishwa na Morocco kocha type ya Namungo🤣🚮
Uko sahihi kabisa.Taifa stars ifundishwe na walimu wenye ubora na uzoefu mkubwa kuliko wachezaji wanakotoka kwenye timu zao. Hii itachechemua fikra za wachezaji kuhusu timu yao ya Taifa. Mwanafunzi wa chuo kikuu kufundishwa na mwalimu wa secondari haiamshi hamasa ya mwanafunzi kutaka kujifunza. Timu yetu ya Taifa inafundishwa na walimu wenye CV na uzoefu hafifu sana wa mechi za kimataifa, hatutoboi hata kidogo kama tutaebdelea hivi.
Sio tu wachezaji lakini hata mashabiki hawako tayari kwenda kuona timu inayofundishwa na kocha ambae hana uzoefu wa kuifikisha timu hata nafasi ya nne za juu kwenye ligi ya nchi yoyote duniani. Timu inafundishwa na makocha wa low profile kuliko makocha wa timu za wachezaji, hii inaleta mtafaluku kwenye kikosi, hakuna nidhamu au kunakuwa na nidhamuya woga tu ya wachezaji kuogopa bifu na visilani vya kutokuitwa timu ya taifa.
Lazima tupate mwl ambae amewahi kuifikisha timu kwenye nusu au finali au kuchukua kombe la Afcon, CAF au world cup, sio vinginevyo.
Very true ✔️1. Hayupo kocha wa kibongo aliyewahi walau kupata kandarasi ya kufundisha nje ya mipaka ya Tanzania...
2..Ndaragije (Mrundi) alifundisha Mbao na Azam, Moses Basena (Mganda) alifundisha Simba na kagera, Razak Siwa (Mkenya) alizi-coach Yanga & mtibwa
Chamangwana (mlawi) alifundisha Yanga nk...mbona wakwetu hawauziki nje.
3.Tofauti na kuzungumza Kiswahili makocha wetu hawana lolote la kumwongezea Dismas Novatus Miroshi anayecheza ligi kuu ya uturuki..au samatta aliyekutana na makocha bora toka Genk, Aston Villa, Royal Antwerp au Paok.
4..Makocha wazawa hatujaanza kuwatumia Leo...Tulishawaamini toka enzi za Mziray, Mkwasa, Kayuni, Kinanda,mpaka salum Mayanga, Amy Ninje au Oscar milambo...
Hatujawahi kupata achievement yeyote chini yao tofauti na cecafa challenge cup ya 1994.
5..Wewe fikiria Kocha Jemedari Said anaweza kumpa nini Himid Mao aliyecheza clubs 5 chini ya makocha tofauti tofauti pale Egypt..
6..Suala sio cheti...kama ni cheti mimi Naamini Oscar Milambo Anaweza kuwa na vyeti begi zima...kamzidi mbali hata Vicent kompany...
7.Hivi huyu Hemed Moroko aliichezea timu gani kwanza, na lini...Ana achievement zipi? Nini kinamtofautisha kaseja.
8..Ifike mahali tuache ku-politisize soka..mtu anapewa timu simply kwasabu ya kubalance Muungano.
Kaka tumeshinda lakini tujiulize tumeshindaje? Waliosababisha tushinde ni safu bora ya ulinzi. Fei na Mudadhir zilikuwa juhudi zao binafsi. Hatuna kocha, tusije tukajichanganya na matokeo haya.Kwa mfano Mzize anacheza fowadi akitokea pembeni au mbele (9) akiwa Yanga, Dickson Job anacheza beki wa kati au kulia namba hizo hizo ndizo wanazocheza timu ya taifa. Halafu mchezaji kubadilishiwa namba na kocha timu ya taifa ni kitu cha kawaida.