Nilitazama mchezo wa Yanga vs Mtibwa Fc niliona kabisa alipaswa kuondoka na Clean sheet bila wasi wasi lakini kilichotokea alifungwa goli la kizembe/la kujitakia.
Mashabiki /wadau wa mpira hawakupiga kelele kwa kua Yanga iliibuka na ushindi mnono wa goli 4 kwa 1.
Ukitazama goli la Mtibwa sugar mfungaji alilifunga akiwa katikati ya uwanja baada yakuona Diara katoka golini akapiga mpira wakapata goli la kufutia machozi.
Hii siyo Mara ya kwanza Diara amekua na Tabia ya kutoka golini ipo siku timu itakosa point tatu muhi kwa uzembe/kujiamini sana kwa Diara.
Mfungaji wa goli la Mtibwa alisema "madhaifu ya kipa Diara ni kujiamini sana na ndiyo maana nilipiga mpira golini nikafunga"
Nichukue Fursa hii kuliambia benchi la ufundi la Yanga Sc kuwa waongee na Diara apunguze over confidence ipo siku ataikost timu kimasihara sihara.
Nawasilisha hoja.
View attachment 2849810