Mbali na hizo changamoto za mwamuzi, lakini benchi la ufindi Simba linachangamoto ya nidhamu na utendaji kwa makochaa wakuu. Ni historia ya muda mrefu na Yule uchebe alishawahi kulalamikia hili swala na kuwaita wasaidizi IGNORANTS.
Gomez nae anaamini katika hii shida. Kwamba wakati mwingine kunakosekana ile kitu inaitwa Chain of Command na hii ndio sababu Simba kutolewa klabu bingwa Africa japokuwa mpaka kipindi cha pili Simba ilikuwa na agg ya goli tatu bila . Hii pia ni Sababu Pablo jana alipeleka ujumbe kwa kificho cha mwamuzi , lakini ni dhahiri hakupenda gesture y’a Matola kuingilia majukumu ambayo sio yake . Makocha wengi pale msimbazi hawamalizi vyema na matola pamoja na wasaidizi wengine , hii ni ishara ipo shida ya Mamlaka kwenye bench la ufundi Simba SC, na Lisiposhughulikiwa haraka , itakuwa ni hatari. Kuna vitu vingi sana Pablo anavishangaa sana pale msimbazi , na ninaona kabisa ipo siku anaweza vunja mkataba kama hii shida ya wasaidizi na nidhamu zao hazijafanyiwa kazi .
Ali kamwe alishawahi zungumzia ishu ya MAMLAKA kwa benchi la ufundi Simba.
Hakuna chain of command ; uhalisia upo hivi , match inapoanza hakuna yoyote anaeruhusiwa kusimama kwenye pitch except Head Coach , na Kama yupo atakaesimama basi ni kwa idhini ya Head Coach, hii nidhamu ina miss pale msimbazi.
Matola au yule msaidizi anaweza kwenda mbele ya pitch huku head coach yupo na hajatoa hiyo idhini, kwa namna moja au nyingine, haya mambo Pablo yanamshangaza maana soka alilotoka nidhamu ya mpira haipo hivyo.
Mfano jana Matola alienda hadi kwenye pitch kutoa maelezo kwa mwamuzi na mchezaji huku kocha Mkuu yupo nyuma na mbali kabisa; kwenye mpira yale ni matusi kwa kocha mkuu na ni ishara ya kukosekana mamlaka na ownership kwa kocha Mkuu dhidi ya kikosi chake, hata kama matola alifanya kwa nia njema ya kumsaidia kocha Mkuu, yale ni makosa ya nidhamu kwa aliye juu yako.
Ukifuatilia maelezo ya Pablo leo, utaona pia anazungumzia nidhamu hasa timu inaposhinda, matola na wasaidizi walipoteza control ya Kimamlaka baada ya kuona timu ipo okay , kocha Mkuu akarukwa ... huyoooo matola anaonekana kwenye pitch , haijulikani alitoa wapi hiyo idhini. Ni nidhamu mbovu ya kimamlaka kwenye miiko ya mpira na njia moja wapo ya kuua uhusiano na kocha Mkuu.
Nadhani Bodi ya Simba ifanye Orientation ya Job responsibilities za hawa wanaoitwa wasaidizi wa kocha Mkuu .lakini pia wafundishwe nidhamu ya chain of command, Otherwise kwa staili za kina matola, tutapata shida kupata makocha wa maana.
Tunaweza kujifunza nidhamu ya benchi la ufundi la Ahly kule misri. Once game inapoanza hakuna anaesimama kwenye pitch except kocha Mkuu kwa sababu zozote zile.
Bodi ya Wakurugenzi Simba, review hii kitu, ipo shida kwenye mamlaka ya Head Coach, Gomezi siku zote anaamini alihujumiwa na hizi tabia na hakuondoka vyema na hawa watu. Msipolifanya kazi kwa kutoa training ya majukumu, Ipo siku Pablo ataamka Asubuhi na kuvunja Mkataba, anaonekana ana zero tolerance kwenye mambo ya kiswahili