Benchi la Ufundi Simba SC

Benchi la Ufundi Simba SC

Ulitaka ataje hiyo sababu.?

Manara pia aliondoka Simba kwa Sababu za kimamlaka dhidi yake na Barba. Hii shida ipo pale Msimbazi. Fungua macho yako
Juma Mkaamia naye aliondoka kwa madai kama hayo na akamsikitikia Kassim Dewj kwamba anapata taabu sana.
 
Sijui mnahangaika kutafuta kitu gani!!? Jambo limeshafafanuliwa lakini bado tu mnatafuta sababu za kusadikika!!

Kwanza Kocha hakutaka kutoa ufafanuzi. Ameombwa sana. Yeye anaona ni mavitu ya ajabu tu
 
Mbali na hizo changamoto za mwamuzi, lakini benchi la ufindi Simba linachangamoto ya nidhamu na utendaji kwa makochaa wakuu. Ni historia ya muda mrefu na Yule uchebe alishawahi kulalamikia hili swala na kuwaita wasaidizi IGNORANTS.

Gomez nae anaamini katika hii shida. Kwamba wakati mwingine kunakosekana ile kitu inaitwa Chain of Command na hii ndio sababu Simba kutolewa klabu bingwa Africa japokuwa mpaka kipindi cha pili Simba ilikuwa na agg ya goli tatu bila . Hii pia ni Sababu Pablo jana alipeleka ujumbe kwa kificho cha mwamuzi , lakini ni dhahiri hakupenda gesture y’a Matola kuingilia majukumu ambayo sio yake . Makocha wengi pale msimbazi hawamalizi vyema na matola pamoja na wasaidizi wengine , hii ni ishara ipo shida ya Mamlaka kwenye bench la ufundi Simba SC, na Lisiposhughulikiwa haraka , itakuwa ni hatari. Kuna vitu vingi sana Pablo anavishangaa sana pale msimbazi , na ninaona kabisa ipo siku anaweza vunja mkataba kama hii shida ya wasaidizi na nidhamu zao hazijafanyiwa kazi .

Ali kamwe alishawahi zungumzia ishu ya MAMLAKA kwa benchi la ufundi Simba.

Hakuna chain of command ; uhalisia upo hivi , match inapoanza hakuna yoyote anaeruhusiwa kusimama kwenye pitch except Head Coach , na Kama yupo atakaesimama basi ni kwa idhini ya Head Coach, hii nidhamu ina miss pale msimbazi.

Matola au yule msaidizi anaweza kwenda mbele ya pitch huku head coach yupo na hajatoa hiyo idhini, kwa namna moja au nyingine, haya mambo Pablo yanamshangaza maana soka alilotoka nidhamu ya mpira haipo hivyo.

Mfano jana Matola alienda hadi kwenye pitch kutoa maelezo kwa mwamuzi na mchezaji huku kocha Mkuu yupo nyuma na mbali kabisa; kwenye mpira yale ni matusi kwa kocha mkuu na ni ishara ya kukosekana mamlaka na ownership kwa kocha Mkuu dhidi ya kikosi chake, hata kama matola alifanya kwa nia njema ya kumsaidia kocha Mkuu, yale ni makosa ya nidhamu kwa aliye juu yako.

Ukifuatilia maelezo ya Pablo leo, utaona pia anazungumzia nidhamu hasa timu inaposhinda, matola na wasaidizi walipoteza control ya Kimamlaka baada ya kuona timu ipo okay , kocha Mkuu akarukwa ... huyoooo matola anaonekana kwenye pitch , haijulikani alitoa wapi hiyo idhini. Ni nidhamu mbovu ya kimamlaka kwenye miiko ya mpira na njia moja wapo ya kuua uhusiano na kocha Mkuu.

Nadhani Bodi ya Simba ifanye Orientation ya Job responsibilities za hawa wanaoitwa wasaidizi wa kocha Mkuu .lakini pia wafundishwe nidhamu ya chain of command, Otherwise kwa staili za kina matola, tutapata shida kupata makocha wa maana.

Tunaweza kujifunza nidhamu ya benchi la ufundi la Ahly kule misri. Once game inapoanza hakuna anaesimama kwenye pitch except kocha Mkuu kwa sababu zozote zile.

Bodi ya Wakurugenzi Simba, review hii kitu, ipo shida kwenye mamlaka ya Head Coach, Gomezi siku zote anaamini alihujumiwa na hizi tabia na hakuondoka vyema na hawa watu. Msipolifanya kazi kwa kutoa training ya majukumu, Ipo siku Pablo ataamka Asubuhi na kuvunja Mkataba, anaonekana ana zero tolerance kwenye mambo ya kiswahili
Inawezekana. Lack of chain of command.

Hawa akina Matola ndio walisababisha tutolewe na jwannang Galaxy.
 
... Hii shida ipo pale Msimbazi. Fungua macho yako
1640458500543.png
 
Tulia wewe kolo acha unazo.. Suala la jamaa kuwa Shabiki wa Yanga sio dhambi Ila kikubwa kaandika fact ndo kitu tunaconsider.
Uchambuz ni mzuri toka kwa jamaa tena uliotukuka
 
Pamoja na kuwekewa video ya kiswahili ili muielewe iwapo tatizo ni lugha, bado mnalazimisha sababu ambayo wala haijatajwa mahali popote. Basi tufanye upo sahihi [emoji16][emoji16][emoji16]
Mimi nimepata pointi moja kwake, je, ni sahihi kwa makocha wote kusimama na kutoa maelekezo kwa wachezaji?


Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri jamaa amechambua uhalisia wa jambo jinsi lilivyo na namna ambavyo head coach anavyokuwa hasa katika match za Ulaya na kwingineko.Ametolea mfano hata Aly Ahly namna head coach anavyo-perfom majukum yake match inapoanza.

Kama mwandishi ni mpenzi wa Yanga,basi ameliona tatizo na kama kweli hao wasaidizi wa head coah hawasimami kwa idhini ya kocha mkuu basi maelezo yake ni sahihi sana bila kuangalia mrengo wake katika ushabiki wala kuhusianisha na tukio la match iliyopita.Uhalisia ubaki kama ulivyo,kwamba;

1.Assistance coach anaweza kusimama kutoa maelezo bila idhini ya head coach?
2.Je,hatuawahi kusikia kocha mkuu analalamika kuingiliwa majukumu na kocha msaidizi pale Simba?

Kuna jambo la kulirekebisha pale Simba.
 
Wewe ni utopolo, umekazana kuipa ushauri Simba eti iwe vizuri. Tangu lini utopolo akatoa ushauri wa kujenga kwa Simba? Umeng'ang'ania tu kushauri, si ukawashauri KMC au Mtibwa? Nakuonyesha post yako moja hapa kuwa wewe ni utopolo, yaani nyani na mbwa kwa mujibu wa Luc Eymael:
I think ungejikita na content sio anae toa hoja mfano hii hoja ingetolewa na shabiki wa Simba ungekubaliana nayo au nae ungemuita Nyani?
 
Wewe ni utopolo, umekazana kuipa ushauri Simba eti iwe vizuri. Tangu lini utopolo akatoa ushauri wa kujenga kwa Simba? Umeng'ang'ania tu kushauri, si ukawashauri KMC au Mtibwa? Nakuonyesha post yako moja hapa kuwa wewe ni utopolo, yaani nyani na mbwa kwa mujibu wa Luc Eymael:
Hivi unajisikia aje kumuita mwezako Nyani, Mbwa kisa tu mpira haya maneno si ya kibaguzi ambayo watu weusi tuna lalamika kila siku wanapo itwa wenzetu huko Europe and Asia? Football is fair game behave like a man
 
Back
Top Bottom