Benchi la ufundi Simba

Benchi la ufundi Simba

Wakuu,

Ni muda mrefu sasa nina mashaka na uwezo wa benchi la ufundi la Simba. Hata ushindi tunaopata ni juhudi binafsi zaidi kuliko maelekezo ya kiufundi.

Mechi ya leo ni mfano bora kabisa. Huwezi kuanza kwa kumtumia kiungo kama Kahata ambaye anacheza staili inayofanana na viungo wa Yanga! Mechi ya leo ilihitaji viungo wenye kasi zaidi.

Hata timu inapoonesha kulemewa hakuna mabadiliko ya haraka! Timu inacheza vile vile wakati plan zimeshafeli. Mkude alihitaji msaidizi wa kukaba sababu ya staili yake ya uchezaji lakini kumpanga na watu slow na wasio wakabaji kama Kahata na Chama ilifeli mapema toka mechi ianze na kulikuwa na hatari ya kupata hata kadi nyekundu ilipaswa benchi la ufundi ku change plan haraka!

Simba ina chief coach ambaye hana experience na kufundisha club zaidi ya kupatia experience Simba. Wachezaji wanatoa kila walichonacho lakini plan mbovu kwa mechi za kimbinu kama hizi zinawaangusha.

Simba ina timu bora kabisa, tunahitaji pia benchi la ufundi bora ili kitumia vipaji vilivyopo vizuri.

Nimeandika hili baada ya kufatilia mechi nyingi zaidi ya mechi ya leo na pengine ushindi hututia upofu lakini zipo mechi nyingi makocha wa timu pinzani wanafanikiwa kimbinu lakini wanazidiwa na experience ya wachezaji wa Simba kimbinu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika mkuu. Tactically coach wa simba ana mapungufu mengi sana. Ukitazama mechi zote ambazo simba anakutana na wapinzani wenye kupush timu inakuwa haina utulivu, No urgency,. Unamuacha chama anacheza dk 90, huku unaanza na kiungo mkabaji mmoja...poor game plan
 
Aaaaaaah! unatudanganya, haya ungeyaongea toka mechi kabla ya Yanga,Na tulishakubaliana kabla ya mechi msije mkamsema vibaya mchezaji yoyote wala coaching team endapo mtapoteza mchezo, sasa imekuaje tena?[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakika mkuu. Tactically coach wa simba ana mapungufu mengi sana. Ukitazama mechi zote ambazo simba anakutana na wapinzani wenye kupush timu inakuwa haina utulivu, No urgency,. Unamuacha chama anacheza dk 90, huku unaanza na kiungo mkabaji mmoja...poor game plan
Kwani haya umeyajua leo, mechi za Ndanda mboma hamkuongea haya, acheni mambo hayo bhana, mlikuwa mnajimwambafai mtashinda 4-1, zikwapi sasa????? endeleeni kupiga ramli uhalisia wa mpira upo uwanjani.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tena mechi dhidi ya Azam kocha akaonekana bonge la kocha, na hadi Mwenyetimu (Mo Dewji) akampa kongole kocha baada ya mechi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani haya umeyajua leo, mechi za Ndanda mboma hamkuongea haya, acheni mambo hayo bhana, mlikuwa mnajimwambafai mtashinda 4-1, zikwapi sasa????? endeleeni kupiga ramli uhalisia wa mpira upo uwanjani.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mapungufu ya benchi hasa kimbinu kwa head coach wa simba yapo wazi , labda kama sio mfuatiliaji wa mpira
 
Wakuu,

Ni muda mrefu sasa nina mashaka na uwezo wa benchi la ufundi la Simba. Hata ushindi tunaopata ni juhudi binafsi zaidi kuliko maelekezo ya kiufundi.

Mechi ya leo ni mfano bora kabisa. Huwezi kuanza kwa kumtumia kiungo kama Kahata ambaye anacheza staili inayofanana na viungo wa Yanga! Mechi ya leo ilihitaji viungo wenye kasi zaidi.

Hata timu inapoonesha kulemewa hakuna mabadiliko ya haraka! Timu inacheza vile vile wakati plan zimeshafeli. Mkude alihitaji msaidizi wa kukaba sababu ya staili yake ya uchezaji lakini kumpanga na watu slow na wasio wakabaji kama Kahata na Chama ilifeli mapema toka mechi ianze na kulikuwa na hatari ya kupata hata kadi nyekundu ilipaswa benchi la ufundi ku change plan haraka!

Simba ina chief coach ambaye hana experience na kufundisha club zaidi ya kupatia experience Simba. Wachezaji wanatoa kila walichonacho lakini plan mbovu kwa mechi za kimbinu kama hizi zinawaangusha.

Simba ina timu bora kabisa, tunahitaji pia benchi la ufundi bora ili kitumia vipaji vilivyopo vizuri.

Nimeandika hili baada ya kufatilia mechi nyingi zaidi ya mechi ya leo na pengine ushindi hututia upofu lakini zipo mechi nyingi makocha wa timu pinzani wanafanikiwa kimbinu lakini wanazidiwa na experience ya wachezaji wa Simba kimbinu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa, hata kesho akiingia na game plan kama ya leo mbele ya Yanga tunafungwa.

Mkude hawezi kucheza defensive midfield peke yake kwenye mpira wa kasi na nguvu kama wa Yanga.

Nyuma yake alitakiwa kuwepo Fraga. Mkude hata hivyo ana bahati sana alitakiwa apewe kadi nyekundu kwa faulo iliyosababisha goli, ambayo haikuwa na sababu yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja 100%.

Dilunga, Kanda walitakiwa kuanza mapema kabisa, then either Boko au Kagere mmoja aanzie benchi plus Kahata. Game tungeimaliza mapema sana.

Kocha wa Simba bado mchanga, ila simlaumu kwa ile CV yake, hao viongozi waliompa kazi sijui waliona nini kwake, na nikikumbuka walimuacha Aussems uuuh!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sven na Aussems wote hawajui kubadili mbinu uwanjani, wanacheza namna moja wakati wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba wamesawazisha ndugu wasikilizaji[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

kilicho akilini kitumie
 
Kwa upande wangu kufungwa leo Ni kosa la benchi la ufundi. Tulikwisha ambiwa Yanga wamewatumia wasauzi kufanya analysis za mapungufu ya simba. Na timu yetu haijawahi kubadilisha mfumo. Hivyo kocha alitakiwa ajue kwamba benchi la yanga lilikuwa limefanya Nguvu kubwa kuharibu mbinu ya timu.

Nilitegemea kumuona kocha akibadili plan na hata kubadilisha kikosi kwa kuwaacha nje baadhi ya wachezaji.

Yanga walituzidi kimbinu, pasi fupifupi zilituua sana, mabeki na viungo wa Yanga walikuwa wanapata nafasi ya kurudi na kukaba. Tulipoamua kupiga mipira mirefu tulikuwa tukifika golini.

POOR AND INEXPERIENCED COACH

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa lilikuwa katikati Mkude Alizidiwa Kocha na kocha alitakiwa aongeze Holding Midfilder..

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ndiyo ubovu wa kocha, Hana plan ya ziada na akizidiwa hawezi ku badirisha chochote. Mkude alizidiwa kwa sababu viungo wote wa juu walikuwa slow. Kwenye mechi zingine inaweza isionekane tatizo ila mechi inayohitaji mbinu kama leo lazima kocha ubadirike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom