Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Bendera ya Israel ndani ya magari ya Dar ni siasa tu au kuna la zaidi?

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Waungwana kuna mambo maishani huwa yanapotazamwa humuachia mtazamaji kila aina ya tafakuri kichwani mwake. Ndani ya miaka kadhaa ya hivi karibuni, kumezuka tabia ya watu kuitundika bendera ya Israel kwenye sehemu ya chini ya kioo cha ndani ya gari, kile ambacho dereva hukitumia kutazama magari yanayokuja kutokea nyuma ya gari.

Mwanzoni nilidhani ni mahaba binafsi ya mtu mmoja, lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo mashabiki wa bendera hiyo maarufu duniani, walivyozidisha tabia hiyo.

Huwa najiuliza kama Waisrael na wao wanayo tabia ya kuitundika bendera ya Tanzania, katika sehemu ile ile ambayo sisi tunaitundika bendera yao ndani ya magari yetu. Huwa najaribu kujiuliza iwapo Mtanzania anayekatiza katika mitaa ya Jerusalem au Tel Aviv anaweze kukutana na gari ambalo ndani yake kuna bendera ya Tanzania imetundikwa, na muisrael akiendesha gari huku akiufurahia uwepo wa bendera yetu.

Haya ni mawazo yangu, kwani tabia hii imenifanya nijiulize iwapo upendo unaotoka mioyoni mwetu kuelekea kwa Waisrael, unaweza na wenyewe kuwa unathaminiwa na Waisrael bila ya sisi Watanzania kujua ni jinsi gani tunavyothaminiwa.
images
 
Huwa najiuliza kama Waisrael na wao wanayo tabia ya kuitundika bendera ya Tanzania, katika sehemu ile ile ambayo sisi tunaitunduka bendera yao ndani ya magari yetu. Huwa najaribu kujiuliza iwapo Mtanzania anayekatiza katika mitaa ya Jerusalem au Tel Aviv anaweze kukutana na gari ambalo ndani yake kuna bendera ya Tanzania imetundikwa, na muisrael akiendesha gari huku akiufurahia uwepo wa bendera yetu.

Haya ni mawazo yangu, kwani tabia hii imenifanya nijiulize iwapo upendo unaotoka mioyoni mwetu kuelekea kwa Waisrael, unaweza na wenyewe kuwa unathaminiwa na Waisrael bila ya sisi Watanzania kujua ni jinsi gani tunavyothaminiwa.
Bado hujaijua Israel mpaka sasa, hilo ni taifa pekee duniani lenye uwezo wa kujitegemea kwa kila kitu na limezungukwa na majirani maadui, bendera ni ishara ya upendo
 
kun
Waungwana kuna mambo maishani huwa yanapotazamwa humuachia mtazamaji kila aina israeya tafakuri kichwani mwake. Ndani ya miaka kadhaa ya hivi karibuni, kumezuka tabia ya watu kuitundika bendera ya Israel kwenye sehemu ya chini ya kioo cha ndani ya gari, kile ambacho dereva hukitumia kutazama magari yanayokuja kutokea nyuma ya gari.

Mwanzoni nilidhani ni mahaba binafsi ya mtu mmoja, lakini kadri siku zinavyokwenda ndivyo ambavyo mashabiki wa bendera hiyo maarufu duniani, walivyozidisha tabia hiyo.

Huwa najiuliza kama Waisrael na wao wanayo tabia ya kuitundika bendera ya Tanzania, katika sehemu ile ile ambayo sisi tunaitundika bendera yao ndani ya magari yetu. Huwa najaribu kujiuliza iwapo Mtanzania anayekatiza katika mitaa ya Jerusalem au Tel Aviv anaweze kukutana na gari ambalo ndani yake kuna bendera ya Tanzania imetundikwa, na muisrael akiendesha gari huku akiufurahia uwepo wa bendera yetu.

Haya ni mawazo yangu, kwani tabia hii imenifanya nijiulize iwapo upendo unaotoka mioyoni mwetu kuelekea kwa Waisrael, unaweza na wenyewe kuwa unathaminiwa na Waisrael bila ya sisi Watanzania kujua ni jinsi gani tunavyothaminiwa.
nadhani ni kasumba tu kwa baadhi ya wafuasi wa yesu kudhani bendera ya kizayuni ya israeli inawakilisha israel ya ndani ya biblia takatifu. israel ya leo ni nchi ya mazayuni wabaguzi wakubwa. ni nchi sawa na apartheid south africa.
 
Looh..Aisaee kama ndo hivyo nami naona niweke BENDERA la Babu yangu enzi hizo !! Kama kweli Utaifa unahusika!!
 
Ni ishara kuwa wanakubaliana na itikadi yao au ni wadau wa itikadi za Israel, kama nao Israel ni wadau wa itikadi za kitanzania ni ruksa kuweka bendera, sio israel kama taifa, ni ITIKADI.
Nakubaliana na wewe kwamba kuna watu kama wewe ambao mnaikubali tabia yake ya ubabe wake huko mashariki ya Kati.Lakini pia ukubali kwamba kuna watu wanaiona Israel kama "taifa teule" na hapa kuna utata kwani ni zaidi ya Itikadi za kisiasa bali tunakwenda hadi kwenye Itikadi za kidini.

Kuna watu wanaodhani kwamba Waisrael ni wakristo (kwa maana ya asilimia) lakini waisrael kwa asili hawaamini kama Yesu ni Masihi Mpakwa mafuta wa Bwana Mungu Yehova. Ndiyo maana wakati kuna baadhi ya Wakristo wanakwenda Hija Israel waisrael wenyewe wanawashangaa na kuwaona kama ni watalii wa kawaida wanaokwenda kutalii maeneo ya Kihistoria yasiyo na mashiko ya Kiimani.

Kama ambavyo kuna mtizamo hasi kwamba Wapalestina wote ni waislam, wakati wapalestina wapo na wakristo na wao pia wanaporomoshewa mabomu na waisrael kama wanavyopromoshewa wenzao waislam kwenye nchi yao!!
 
Mkuu ni kweli kabisa bendera ya Israel imepepea kwenye magari mengi lakini kumbuka Israel ni Taifa teule kama vitabu vitakatifu vinavoeleza wakati Tanzania au hispania ni mataifa ya kawaida
Na hapo ni ndipo ninaposhindwa kumshangaa mungu wenu anayewapanga watu kwa magroup.. Kwamba huyu in first class mja na huyu ni second class mja.. Tena huwapanga hivyo wala so kwa uchamungu wao ! Bali ni kutokana na kuzaliwa by chance katika taifa hilo tu ! What a miracle ![emoji57]
 
Alaaniwe atakaye ilaani Islael na Abarikiwe atayeibariki Islael...
-Period..kama ni mkristo haya maneno utayakuta kwenye Biblia hata mtu ungewaita eti wanadharau wanajisikia,mara ni wabaguzi haisaidii nani sio mbaguzi??nani hajisikii?? nani hana dharau??tuanzie hapo.Wala tusiwasingizie hapa kwetu vipi hakuna hayo??mara'' aaah hawa tutafanya makosa makosa yote lakini si kuwapa ikulu''hiyo ni nini??''hawa ni hizbu zanzibar ni ya weusi''hayo mambo mwanadamu kaumbiwa lakini ayashinde.Lile ni taifa teule lilivushwa bahari ya shamu kwa muujiza wa kutisha na Mungu,kuna taifa lilishawahi kufanyiwa hivyo hapa duniani???kwanza hilo neno Israel tu wamepewa si na mwanadamu bali ni Mungu mwenyewe aliwapa kwa nini wasijisikie fahari??
 
Huna haja ya kijiuliza sn, historia ya Taifa la Israel ndio pekee inajulikana toka kuumbwa kwa dunia hii,, wakati historia ya Tanzania imeanzia hapo juzi wakt wa Mjerumani,,

Pia kwenye Biblia imeandikwa kila Ailaanie Israel nae Atalaaniwa na kila Aibarikie Israel naye pia Atabarikiwa , hivyo watu kutundikwa kwa bendera za Israel watu wanatafuta Baraka ndio maana unaziona kwa watu waliobarikiwa zikiwa ndani ya Magari,,

Bendera hizi huzikuti kwenye Bar, Casino, au kwenye Guest house bali unazikuta kwenye uwepo wa Mungu pale watu wanapohitaji ukaribu wa Mungu uwe nao wawapo safarini nk.
 
Mbona hao waisraeli hawabebi bendera za Tanzania. Na haya mambo yanafanyka kwenye nchi za kiafrika maana Marekani PAMOJA NA ushosti wote na Israeli huwezi ona raia wake wakitembea na hizo bendera never ni sisi tu wafuata mkumbo bila kuelewa.
Halafu kuna kitu nakishangaa kwa hawa wakristo wanaobeba hizi bendera maana sio wote. Wanasena wanamuamini YESU Kristo but wanapeperusha bendera za watu wasiomuamini YESU kristo
 
Na hapo ni ndipo ninaposhindwa kumshangaa mungu wenu anayewapanga watu kwa magroup.. Kwamba huyu in first class mja na huyu ni second class mja.. Tena huwapanga hivyo wala so kwa uchamungu wao ! Bali ni kutokana na kuzaliwa by chance katika taifa hilo tu ! What a miracle ![emoji57]

It wasn't by chance
 
Back
Top Bottom