Bendera ya Taifa iongezwe rangi nyekundu

Bendera ya Taifa iongezwe rangi nyekundu

Duuu wewe jamaa unaona mbali sana kuliko darubini
Wako watu kama akina Mkwawa, Kinjekitile, Isike na wengine ambao waliomwaga damu zao wakati wa kuitetea nchi hii. Kupinga dhuluma na fedheha za kutawaliwa. Lakini wapo Watanzania hadi leo ambao wanamwaga damu zao kuilinda nchi hii na kupinga dhuluma na kutetea misingi ya kidemokrasia na utawala bora.

Kuna ubaya gani kama bendera yetu ikiwatambua mashujaa hao kwa kuongeza rangi nyekundu japo kwenye kamba ya kupandisha na kushushia bendera au Basi hata kwenye mlingoti wa bendera?
 
Bendera itabadilishwa baada ya CCM kupigwa chini, Katiba mpya ya Warioba kupitishwa na Muungano kuvunjiliwa mbali..
Na Tanganyika kupata Uhuru na
Kubadilisha jina lake..
Hizo ndiyo duwa za watanzania walio wengi
 
Ndiyo maana hawataki kabisa kusikia habari za tume huru maana wanajua wakitoka madarakani lazima watakuwa na wakati mgumu sana
Tatizo la nchi hii ni CCM. Kwa mfano katiba mpya iliyokula mabilion ya watanzania wameiweka kabatini.
 
Hakuna popote wadai uhuru wakapata uhuru bila kupigana hata kidogo
Huko ni kuipindisha historia ya ukombozi wa taifa hili. Ukombozi wa taifa hili haukuzia na TANU Kama tunavyodhani. Wako waliopoteza maisha yao kupinga ukoloni. Anaetufundisha kuwa tuliupata Uhuru bila kumwaga damu anatupotosha kwa manufaa yake.
 
Wako watu kama akina Mkwawa, Kinjekitile, Isike na wengine ambao waliomwaga damu zao wakati wa kuitetea nchi hii. Kupinga dhuluma na fedheha za kutawaliwa. Lakini wapo Watanzania hadi leo ambao wanamwaga damu zao kuilinda nchi hii na kupinga dhuluma na kutetea misingi ya kidemokrasia na utawala bora.

Kuna ubaya gani kama bendera yetu ikiwatambua mashujaa hao kwa kuongeza rangi nyekundu japo kwenye kamba ya kupandisha na kushushia bendera au Basi hata kwenye mlingoti wa bendera?
Wazo zuri sema nchi na vilivyomo ni mali ya Mwenyekiti wa CCM wengine wote ni wapangaji.
 
Hiyo rangi nyekundu itaongeza ajira,kuboresha miundombinu,kukuza kilimo n.k?
 
Wana Simba buana! Tuwekee rangi yenu kisa rangi za Yanga zipo! Yanga ndo nchi nyie tulieni hivyo hivyo
 
Asante Mungu mpaka sasa upinzani hawajafankiwa kushika dola, kwa mawazo kama haya hatma ya Taifa hili ingewekwa rehani.
 
Na ukizingatia timu mabingwa wa nchi ni wekundu wa msimbazi.[emoji321][emoji3590]
 
Bendera itabadilishwa baada ya CCM kupigwa chini, Katiba mpya ya Warioba kupitishwa na Muungano kuvunjiliwa mbali..
Na Tanganyika kupata Uhuru na
Kubadilisha jina lake..
Jina halitabadilika nchi itaitwa Jamhuri ya Tanganyika ilivyoitwa kabla ya Muungano bandia au Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (United Republic of Tanganyika and Zanzibar, Tanzania). Jina lenye maana siyo la sasa ambalo halina maana yoyote kwa kuwa halionyeshi ni nchi gani zimeungana. Katika Awamu hii polisi imeua watu wengi zaidi kwa kisingizio cha ujambazi kuliko wakati wowote toka Uhuru, polisi wengi wameuawa kuliko wakati wowote, wananchi wamepotea bila taarifa wengi kuliko, wengi wametekwa na maiti nyingi zilizochinjwa kuokotwa kwenye viroba, kwa hiyo si vibaya kukumbuka damu iliyomwagika Awamu hii.
 
Back
Top Bottom