Bendera ya Taifa iongezwe rangi nyekundu

Hiyo rangi nyekundu itaongeza ajira,kuboresha miundombinu,kukuza kilimo n.k?
Sio vema kuwasahau watu waliotufanyia mema. Mungu kupitia damu zao Kuna kitu atafanya kitakachotuongezea ajira na kupata uchumi wa kujengea miundo mbinu yetu.

Ogopa Sana damu ya mtu iliyomwagika kwaajili yako kisha ukamsahau mtu huyo. Kuacha kuweka alama nyekundu kwenye bendera yetu Ni jitihada za kuwakana waliokufa kwaajili ya kulipigania taifa na maisha yetu.
 
Simba walimwaga damu wapi mbona wana rangi nyekundu kwenye bendera yao
Ndiyo maana timu zenye jezi nyekundu ama alama nyekundu huwa zinapata mafanikio Sana, fanya utafiti. Mchezo wa mpira Ni wa kuvuja jasho na damu uwanjani. Wako wanaovunjika, wanaokwaruzana, wanaokufa viwanjani. Rangi nyekundu kwenye jezi Ni kuunga mkono kazi za wachezaji hata wanapopata majeraha na kuvuja jasho zao
 
Si ndo maana kuna siku ya mashujaa! Watakumbukwa hapa
 
Rangi ya bendera haisaidii kama hata waliopigania nchi ambao bado wapo hai hamuwajali.

Mpaka wafe ndio sifa zinatoka kibao .
 
Rangi ya bendera haisaidii kama hata waliopigania nchi ambao bado wapo hai hamuwajali.

Mpaka wafe ndio sifa zinatoka kibao .
Hahaha!; hao waliohai tuko nao pamoja, tunafaidi wote kupita kwenye flyovers, shida Ni wale waliopoteza uhai. Angalau Basi kuwe na kitu kinachowafanya wakumbukwe kila inayoitwa leo. Mtu anaposema nchi yetu imepata Uhuru bila kumwaga damu anatudanganya pakubwa. Uhuru wa taifa hili ulianza tangu siku ya kwanza wakoloni na wageni wengine walipowasili nchini. Wako watu waliopinga kutawaliwa na kuishia kuuawa, kufungwa na kuteswa vibaya.
 
๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ๐Ÿ‡น

Chagua katika eneo gani la hizo bendera rangi nyekundu iwekwe??
Zinawekwa hats nyotร  tano za rang nykundu upande wa blue kulia
 
Mkwawa hakuwa shabiki wa Simba kwa hiyo hiyo rangi anzisha bendera yako binafsi na uitungie katiba yake ambayo sehemu ya utawala itaishia hapo nyumbani kwenu bila kuathiri katiba na sheria za nchi!
 
Bendera ya sasa mbaya sana. Bora ile ya Tanganyika kuliko hii ya Tanzania
 
Zinawekwa hats nyotร  tano za rang nykundu upande wa blue kulia


๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ป๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ญ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฒ Angalia hapo, nyota huwa haiwekwi nyekundu huwa ni nyeupe.
 
Swala la msingi hilo nyerere alikosea kuweka rangi za ccm katika bendera.
 


Bendera ya taifa iwe nyeupe tupu au nyeusi tupu kama kaniki ili kuepusha unnecessary complications.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ