Papa benedicto wa tisa alizaliwa katika mji wa roma mwaka 1020 na jina lake la kuzaliwa anaitwa Theophily Tesculu, mtoto wa Ableric wa tatu ambaye alikuwa ni mpwa wa papa benedict wa nane na papa john wa kumi na tisa. Papa benedict alikuwa papa mwaka 1032 akiwa na miaka kumi na mhwili tu. Ni papa wa 145 katika orodha ya mapapa wote Alipata cheo hicho kwa njia zisizo sahihi kwa kuwa alikuwa katika familia ya kipapa. Mtangulizi wake alikuwa papa john wa kumi na tisa. Katika utawala wake ni machafuko matupu. Na mwishowe alitaka cheo hicho ili apate pesa. Mwaka 1044 aliondolewa kwa amri ya kaisari. Aliyemfuata baada ya hapo ni papa sylvester wa tatu