Benin vs Tanzania, Madagascar vs DR Congo on African Qualifiers - FIFA World Cup Qatar 2022

Dondosha Kura yako hapo, Mechi ya Benin vs Tanzania.

  • Tanzania itashinda

    Votes: 6 60.0%
  • Benin itashinda

    Votes: 4 40.0%
  • Suluhu/sare

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    10
  • Poll closed .

De Opera

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
780
Reaction score
1,664
Tanzania(Taifa stars) kupambana tena na Benin kwa mara hii wakiwa ugenini Siku ya Jumapili Oktoba 10 kuanzia saa 10 za jioni, katika mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar.
Stars ilipoteza nyumbani dhidi ya Benin kwa kufungwa bao 1 kwa 0 katika mchezo uliopigwa dimba la Mkapa jijini Dar es salam.

Madagascar watakuwa wakiikaribisha Dr Congo siku hiyo hiyo kuanzia majira ya saa moja za usiku.

MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA

Tanzania
0 - 1
Benin
DR Congo​
2 - 0
Madagascar​

MSIMAMO WA KUNDI J​

TEAMMPWDLGFGAGDPts
Benin32103127
DR Congo31204225
Tanzania31114404
Madagascar300326-40

MECHI ZIJAZO​

Benin​
Vs​
Tanzania​
Jumapili Oktoba 10 2021, 16:00 EAT
Madagascar​
Vs​
DR Congo​
Jumapili Oktoba 10 2021, 19:00 EAT
 
Huu mtanange vijana wakitulia tunashinda huu mchezo juzi tulicheza vizuri zaidi yao tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga ila washambuliaji walituangusha nadhani ni bahati haikuwa upande wetu.

Binafsi naona kwa miaka ya hivi karibuni naona T Stars hii mpira wanaocheza unaeleweka.

Mola ibariki TANZANIA.
 
Hakika nafasi ipo kabisa.
 
Kila mtu na mtazamo wake lakini binafsi hata kama tungeshinda Benin walikuwa juu kwa viwango vya wachezaji.

Walikuwa na mipangilio zaidi na hata pasi zao zilikuwa za uhakika zaidi.

Kama Taifa tujiulize wenzetu hufanya nini kuwa na wachezaji na timu zenye viwango kama ilivyo huko Afrika ya Magharibi?
 
"Bahati haikuwa upande wetu", mambo ya kiswahili kabisa. Football ⚽ means results and not brilliant footwork. Tanzania has never been a footballing country.
 
Ni ngumu kumfunga benin!!sisi tutakalia hivyo hivyo kuwa tulicheza vizuri zaidi, mala bahati haikuwa yetu, Ni maneno ya mwenye uwezo mdogo!!mtu anayejua mpira anacheza kwa kutumia akili nyingi, badala ya nguvu nyingi, ndio maaana nafasi chache, goli, nyie nafasi kibao hakuna goli!!tufanye mambo mengine tu kwa ni lazima iwe mpira tu?!!
 
Wachezaji wetu hawana muda wa wao wenyewe kujiongezea skills.Wanashinda kwenye mitandao ya kijamii kushindana na mashabiki.
Wachezaji wengi wakubwa kisoka sio umri 😆... unakuta yuko uwanjani amepangilia vile vikopo vya kupimia mahindi kama chizi anatafuta skills.Sasa hawa wa kwetu mwalimu akiugua shule haipo tena.
 
"Bahati haikuwa upande wetu", mambo ya kiswahili kabisa. Football ⚽ means results and not brilliant footwork. Tanzania has never been a footballing country.
😅 Hii misemo ya "Bahati haikuwa upande wetu" mara ooh "Hata hivo wamejitahidi" .Mimi kama mwanaharakati siipendi sana.
 
Ni ngumu kumfunga benin!!sisi tutakalia hivyo hivyo kuwa tulicheza vizuri zaidi, mala bahati haikuwa yetu, Ni maneno ya mwenye uwezo mdogo!!mtu anayejua mpira anacheza kwa kutumia akili nyingi, badala ya nguvu nyingi, ndio maaana nafasi chache, goli, nyie nafasi kibao hakuna goli!!tufanye mambo mengine tu kwa ni lazima iwe mpira tu?!!
Hapa Bongo ukisema hivo utasikia kuna mburula zinasema Ingia wewe ukacheze. 😄😄
 
Muda huu mchezo unaendelea. congo kala kimoko tayari kwa madagasca.. Mpira hautabiriki... ndo manana kuna sport betting..
 
Congo akishinda Stars anatolewa ama?
Akishinda congo atakuwa anaongoza kundi akiwa na alama 8 huku Tanzania tukiwa nafasi ya pili kwa alama 7. Anayeenda hatua inayofuata ni anayeongoza kundi. Hivyo Tanzania tutakuwa tumebakiza mechi ya Dar dhidi ya Congo na mechi ya ugenini dhidi ya Madagascar
 
Muda huu mchezo unaendelea. congo kala kimoko tayari kwa madagasca.. Mpira hautabiriki... ndo manana kuna sport betting..
Na Madagascar ni wamoto atare yaani Congo analala leo.
 
Back
Top Bottom