MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Sikumbuki mara ya mwisho kuona mashindano yoyote makubwa ya riadha au matumizi yoyote ya zile running tracks zilizopo katika dimba la Mkapa.
Sanasana imekuwa sehemu ya viongozi kuzunguka kupungia mkono wananchi pindi wanapoapishwa.
Ukiingia uwanja wa Mkapa kutazama mechi kama haukai walau VIP A itakulazimu kutumia darubini kuweza kuwaona vyema wachezaji na movement za mpira, Hata timu pinzani zinapokuja kucheza kwa Mkapa wananufaika sana na umbali uliopo kati ya pitch na mashabiki.
Katika ulimwengu wa sasa ambapo mchezo wa soka unakuwa sana, nchi zilizoendelea katika soka hawatumii olympic stadiums, ni mara chache sana kukuta timu kubwa zikicheza katika viwanja vyenye running tracks.
Tanzania inahitaji walau uwanja mmoja mkubwa mahsusi kwa ajili ya football. Mambo ya Olympic stadiums yameshapitwa na wakati.
Ndiyo maana mashabiki wanalazimika kubeba mavuvuzela ili walau sauti za kushangilia zifike mbali kwa sababu distance ya siti zilipo mpaka pitch ilipo ni mbali.
Mashabiki hawawezi kuimba kwa hamasa na umoja kama tunavyoona mashabiki wa timu zingine za huko ulaya au nchi za North Africa kwa sababu ya umbali kati yao, hakuna umoja na ukaribu uwanjani, wanaishia kupuliza mavuvuzela. Jambo ambalo kiujumla ni faida kwa timu za upinzani zinapokuja kucheza Tanzania.