Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 6,559
- 12,518
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema haondoi uwezekano wa kumuua kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, akisema hiyo ndio namna ya kuumaliza mzozo baina ya Israel na Iran ambao ni mahasimu wakubwa.
Netanyahu amesema hayo kwenye mahojiano na kituo cha utangazaji cha ABC News alipoulizwa kuhusu ripoti kwamba Rais Donald Trump wa Marekani amezuia mpango wa kumuua kiongozi huyo kutokana na mashaka kwamba utazidisha machafuko.
"Iran inataka vita visivyokwisha", na wanatusogeza kwenye vita vya nyuklia," alisema Netanyahu. "Na inachokifanya Israel ni kuzuia hilo, kumaliza uvamizi, kukomesha uchokozi huu, na tunaweza kufanya hivyo tu kwa kusimama dhidi ya nguvu za uovu."
Akiwa ziarani kwenye kambi moja ya Israel, Netanyahu aidha amesema wanakaribia kufanikisha malengo yao mawili ya kuondoa vitisho vya makombora na nyuklia na kuongeza kuwa "Ikiwa tutadhibiti anga ya Tehran, tutavishambulia vituo vya utawala huu."
Aidha ameishutumu Iran kwa kuwashambulia watu na kuongeza kuwa "Tunawaambia raia wa Tehran: Ondokeni hapo!" kisha tuchukue hatua.
DW