Benki gani yaweza kunipa huu mtaji?

ba nso

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2012
Posts
668
Reaction score
225
habari ndugu zangu. Mimi ninamiliki nyumba mbili mabibo dar. Eneo ni zuri na barabarani kabisa, nahitaji kubomoa hizi ili nijenge ghorofa Moja floor tatu kwaajili ya apartments. kwakua eneo ni kubwa eneo litakalo baki ntafanya parking ya biashara. I am sure this is a good businesses.. Je Kuna anaejua kama hii itakubalika kwa bank?
 
Kajaribu CRDB kama una hati au leseni ya makazi
 
Kaka nadhani kuna mambo mengi yakuangalia kabla ya kufikia huko unakofikia,

1. Kwa harakaharaka, kwa nyumba kama hiyo unayosema unahitaji si chini ya milion 500 kuisimamisha
2. Kuwa na nyumba ya kuweka Dhamana sio guarantee ya bank kukupa mkopo, cha muhimu wanaangalia utarudishaje huo mkopo, namaanisha hivi una njia gani nyingine (kazi, Biashara) halali ambayo inakupa kipato kitakacholingana na mkopo unaotaka?
3. kwa soko lililopo una uhakika unaweza kulipa deni kwa muda muafaka?
 
ni Kweli ninahitaji 500 m, mimi ni mfanyakazi na kipato cha kazini hakiendani na mkopo huo. Soko lililopo ni la uhakika kwa Sasa ninavyumba 14 na napangisha 50. I have a good business proposal
 
ni Kweli ninahitaji 500 m, mimi ni mfanyakazi na kipato cha kazini hakiendani na mkopo huo. Soko lililopo ni la uhakika kwa Sasa ninavyumba 14 na napangisha 50. I have a good business proposal

Hata mm nina shida kama yako mkopo wa 500 mln kwa hesabu ya haraka ya calculator utalipa kwa miaka 9 kwa sh 10 mln @ mwezi kama jumla billion 1, je return zako zitamudu hayo marejesho ? km chini ya hapo itakuwa zaidi ya miaka 15
 
returns ya 10m kwa mwezi ni nyingi mno, ka ntalipa for 20 yrs Itakua angalau, niliskia crdb wanakopesha za ujenz hadi kwa miaka 30 japo sjui kwa kina
 
Jamani naomba ufafanuzi kwa wenye uzoefu na zitto kabwe foundation niliiona huku kwenye jf nikajaza fomu Yao ya kutaka mkopo sasa ninatakiwa nilipe tag 84000nipate mkopo ni kweli? Naomba mnishauri naogopa utapeli
 
hiyo ya zitto kabwe foundation ni utapeli na hata zitto mwenyewe ameshaliongelea
 
mkuu ulifuta nilichokushauri mbona nimerudi sijakiona?
 
kupata hata mil 800 inawezekana shida ni kwamba kwa hiyo hela unayotaka marejesho utakwama tu ndugu maana kurejesha 10m Kila mwezi itakusumbua sana.mwenzio nina mil 40 NMB narejesha kwa mwaka mmoja..hilo rejesho linanitoa jasho..na biashara ilivyo ngumu..sasa mpaka hiyo nyumba ikamilike marejesho utakua unatoa wap?hebu nenda crdb maana hata mimi nlishaisikia hiyo ya marejesho kwa miaka 30 unaweza kupata maelezo kwa kina..nimekutamani na mpangp wako mzuri..Mungu akufanikishe lengo lako litimie!
 
Amen, nitarib kwenda crdb niwaskie, hongera pia kuwa na mkopo hapo nmb. mikopo haikwepeki ndugu.
 
nilisikia mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe. mungu akusaidie akutimizie haja zako
 
Jamani naomba ufafanuzi kwa wenye uzoefu na zitto kabwe foundation niliiona huku kwenye jf nikajaza fomu Yao ya kutaka mkopo sasa ninatakiwa nilipe tag 84000nipate mkopo ni kweli? Naomba mnishauri naogopa utapeli

hao ni matapeli kimbia usiangalie nyuma.
 
pale mwanza kuna jengo la gorofa lipo mtaa wa lumumba.
jamaa ni Muha aliingia ubia na mwarabu yeye akatoa kiwanja mwanrabu akatoa pesa za ujenzi wakagawana sehemu za upangishaji baada ya miaka kadhaa mwarabu kupata pesa za upangaji ataondoka na atamwachia jamaa jengo lake.
_kama vipi fanya hivyo kuepukana na stress za bank.
_watakupa miaka 20~30 Ila utakuwa kama mtumwa wao kila mwezi rejesho,na je una garantee gani kuwa miaka hiyo ishirini utakuwa hai na mzima na utakuwa unapata income ya kulipa huo mkopo?
_pia wakati unakopa kuna hela utatakiwa utoe kama valuation,mchanganuo wa mahesabu,garama za mkopo wa bank,rushwa ya maafisa mkopo.....
_kama utaamua kukopa tafakari kwa kina na upate ushauri haswa!
 
Cheki na Covenant Bank for Women (CBW) ni benki inayokuja kasi, mimi nimechukua mkopo hapo last week.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…