Benki kuuza nyumba ya mteja iliyowekwa dhamana kwa bei ya kutupwa

Benki kuuza nyumba ya mteja iliyowekwa dhamana kwa bei ya kutupwa

Omnabuzegwe

Member
Joined
Aug 16, 2018
Posts
95
Reaction score
73
Ndugu zangu wataalamu wa Sheria ninaombeni mnisaidie kunifafanulia suala hili;

Kuna jamaa yangu alichukua mkopo wa Tshs. 10m kwenye moja ya benki hapa nchini, ambapo aliweka nyumba yake anayoishi na familia. Mkataba ulikuwa ni wa mwaka mmoja. Miezi miwili baada ya kupata mkopo huo,jamaa alivamiwa na majambazi na alinyang'anywa fedha zote.(alikuwa na biashara ya M-Pesa).

Hivyo jamaa alikwama kurejesha kwa wakati. Benki iliamua kuuza nyumba yake hata bila notisi (kwa maelezo yake). Ile nyumba iliuzwa tshs 9.9m tu lakini ni nyumba kubwa sana. Yeye mwenyewe anadai wakati anakopa kwenye mkataba maafsa wa benki waliikadiria kwa tshs. 50m, na wakat wanauza deni lake la mkopo lilikuwa tshs. 7.8m na waliuza nyumba miezi 4 kabla ya mkataba kuisha. Baadaye walikuja kumtoa nje kwa fujo na uharibifu wa vyombo vyake vingi sana.

Je,kwa mazingira hayo huyu jamaa afanye nini au ndiyo nyumba imeondoka hivyo?

Msaada wenu tafadhali ndugu zangu.
 
Anaweza akawafungulia kesi hiyo bank kuwa hawakufata proper procedure adi walipouza hiyo nyumba, then aiombe mahakama ibatilishe uuzwaji huo.
 
Anaweza akawafungulia kesi hiyo bank kuwa hawakufata proper procedure adi walipouza hiyo nyumba, then aiombe mahakama ibatilishe uuzwaji huo.
Ahsante sana Mkuu kwa ushauri wako. Lakn hapohapo nikuulize tena,hili suala ni la tokea 2016.
- Je,bado sheria inaruhusu kufungua shauri?
- Je hata ikitokea mahakama ikabatilisha mnada,atalazimika kulipa riba na faini kwa muda huo wote ambao shauri litasikilizwa hadi kufikia uamuzi?
Mkuu endelea kunisaidia ili hata mimi nimsaidie huyu ndugu kwani ni kama anaenda kupoteza nyumba yake.
 
Hata kama akiwa out of time mahakama inaweza kumpa leave ya kufungua shauri nje ya muda ikiwa atafanya application ya ombi hilo na kama atatoa sababu zenye mashiko mbele ya mahakama. Kuhusu swala la riba obvious benki yoyote Ipo kwa maslahi yake binafsi so as long as pesa Ipo kwa mteja wanaamini unafanya biashara. Endapo mahakama itabatilisha uuzwaji anaweza akaenda kuongea na bank wapange upya jinsi ya kulipa hilo deni au aamue kuuza nyumba yake mwenyewe pasipo kutumia madalali wa mahakama then atawalipa bank pesa yao.
 
Mkuu mpeleke kwa mwanasheria huyo jamaa huko atapata msaada wa kitaalamu zaid
 
Hata kama akiwa out of time mahakama inaweza kumpa leave ya kufungua shauri nje ya muda ikiwa atafanya application ya ombi hilo na kama atatoa sababu zenye mashiko mbele ya mahakama. Kuhusu swala la riba obvious benki yoyote Ipo kwa maslahi yake binafsi so as long as pesa Ipo kwa mteja wanaamini unafanya biashara. Endapo mahakama itabatilisha uuzwaji anaweza akaenda kuongea na bank wapange upya jinsi ya kulipa hilo deni au aamue kuuza nyumba yake mwenyewe pasipo kutumia madalali wa mahakama then atawalipa bank pesa yao.
Nimekusoma sana Mkuu.
Lakini nyumba alishapewa yule aliyeiokota(maana kununua nyumba kubwa ya vyumba 4 vya kulala,choo,bafu,sitting room na yenye vigae na ikiwa na umeme na maji ndani pamoja na boma lingine la vyumba 2 na sebule kwenye uwanja kwa tshs 9.9m ni kuokota)...sheria itaruhusu anyang'anywe huyo aliyemo?
 
Mahakama ikibatilisha tu uuzwaji ananyang'anywa inarudi kwenye possession bank cuz ya mkopo but ownership inabaki kwa huyo ndugu/frnd wako. Alieuziwa ata-deal na bank baada ya kunyang'anywa na mahakama.
 
Mkuu nivumilie uendelee kunisaidia...
Kisheria mahakama inapobatilisha mnada uliofanyika,ni mahakama inaingia kusimamia urejeshwaji wa mkopo hadi uamuzi utakapokuwa umetekelezwa au jukumu litarejeshwa mikononi mwa benki husika?
Gharama za uendeshaji wa kesi zitakula kwake aliyeenda kufungua shauri?
Mkuu nauliza hayo kwa sababu inaweza kutokea hata km mahakama itamrudishia nyumba,ikipigwa hesabu ya mkopo + riba na faini + gharama za mkopo inaweza kujikuta hiyo thamani ya 50m tshs inatumbukia.
 
Mahakama kazi yake ni kutoa maamuzi kulingana na ulivyoomba ikizingatia sana ushahidi wa wadaawa, HIVYO basi kama itaamua uuzwaji ni batili mahakama haitahusika tena kwenye usimamizi wa urudishwaji wa mkopo hilo linabaki kwa ndugu yako na bank.
Kuhusu fedha kuzidi kama akirudishiwa ndugu yako anatakiwa ajiridhishe kabla ya kufungua kesi dhidi ya bank coz mwishoni anaweza akaja kupata hasara yeye.
 
NI MAKOSA KISHERIA TAASISI YA FEDHA KUUZA NYUMBA YA DHAMANA KWA BEI YA KUTUPA.

Image result for MNADA NYUMBA MKOPO

NA BASHIR YAKUB-

Kumekuwa na tabia ya taasisi za fedha kuuza nyumba au viwanja vya watu walivyoweka rehani na kushindwa kulipa mkopo kwa bei ya kutupa. Kwakuwa taasisi za fedha huamini kwamba wana deni na mtu na ameshindwa kulipa hela zao na pengine kwakuwa tayari wamekamilisha taratibu zote za kisheria za kuuza basi huamua kuuza mali ya mtu kwa bei ambayo ni ndogo kiasi cha kustaajabisha.

Ni kawaida kukuta nyumba ya milioni mia ikiuzwa hata milioni kumi na tano ili kulipia deni la milioni kumi na mbili au kumi na tano. Watu wanapaswa kuelewa kuwa hili si sawa na sheria imekataza jambo hili. Thamani ya nyumba au kiwanja iko palepale hata kama mtu ameshindwa kulipa mkopo. Si kweli kuwa kwakuwa sheria imeruhusu kuuza mali ya mtu anaposhindwa kulipa mkopo basi imeruhusu kuuza bei yoyote ile ilimradi muuzaji amepata kiasi anachodai. Hili si kweli kama tutakavyoona hapa chini.

1.WAJIBU WA TAASISI YA FEDHA KATIKA KUUZA NYUMBA YA DHAMANA. .

Kwa kujua hili la kuuza mali za watu bei ya kutupa Sheria ya ardhi kifungu cha 133 ( 1 ) kikasema kuwa muuzaji wa nyumba iliyowekwa rehani ana wajibu mkubwa na wa hali ya juu kuhakikisha anachukua tahadhari na anakuwa mwangalifu kwa kiwango cha juu kuhakikisha wakati anapouza ardhi ya mtu anaiuza kwa bei nzuri na bei ambayo inakubalika kuwa bei inayostahili kwa wakati husika. Huu ni wajibu wa kisheria alionao muuzaji au mnadishaji wa ardhi ya dhamana. Kifungu hicho kinasema kuwa suala la kuuza mali ya dhamana kwa bei inayokubalika ni haki ambayo aliyeshindwa kulipa deni anamdai muuzaji/mnadishaji. Kwa hiyo wewe unayedaiwa unamdai huyo mnadishaji anayetaka kuuza nyumba yako haki ya kuuza hiyo nyumba katika bei inayokubalika ( reasonable price).

2. NYUMBA/KIWANJA KIUZWE BEI GANI KWA MUJIBU WA SHERIA ?

Sheria ya ardhi haikutaja moja kwa moja ni kiasi gani nyumba ya mtu au kiwanja kinatakiwa kuuzwa. Hii ni kutokana na utofauti wa thamani wa mali hizo na hivyo isingekuwa rahisi kusema kuwa bei ya mwisho ya nyumba au kiwanja ni kiasi fulani. Ili kuliweka sawa hili kifungu hichohicho cha 133( 2 ) kikasema kuwa nyumba/kiwanja cha mtu hakitakiwi kuuzwa 25% ya bei ya soko ya nyumba au kiwanja hicho kwa wakati huo au chini yake.

Hii ina maana kuwa ikiwa eneo lako litauzwa kwa njia ya mnada baada ya kushindwa kulipa deni halafu likauzwa asilimia 25 au chini yake kulinganisha na bei ya soko ya eneo hilo kwa wakati huo basi wauzaji na mdai deni aliyewatuma wote kwa pamoja watakuwa wametenda kosa la kisheria. Kwa umuhimu mkubwa narudia kusisitiza kuwa nyumba/kiwanja hakitakiwi kuuzwa asilimia 25 ya bei ya soko ya wakati huo au chini ya asilimia 25 ya bei ya soko ya eneo ya wakati huo, hii ni kwa mujibu wa sheria.

3.NINI UFANYE IWAPO NYUMBA/KIWANJA CHAKO KIMEUZWA 25% AU CHINI YAKE.

Kifungu hichohicho cha 133( 2 ) kinatoa mwarobaini wa kuponesha kidonda cha ardhi yako kuuzwa 25% au chini yake . Kinasema kuwa ikiwa ardhi ya mdaiwa deni imeuzwa kwa bei ya 25% ya bei ya soko au chini yake basi mdaiwa huyo anaruhusiwa kuiomba mahakama kubatilisha mauzo hayo. Hii ni kwasababu mdai amekiuka wajibu wake wa kisheria na hivyo kuyafanya mauzo hayo kuwa haramu.

Nahimiza kwa kusema kuwa watu ambao wamefanyiwa kitendo kama hiki wachukue hatua stahiki haraka za kuiomba mahakama kubatilisha mauzo ya mali zao ikiwa ziliuzwa kinyume na nilivyoeleza hapa. Usiseme au ukadhani umechelewa kwani hili linawezekana hata kama imepita miaka kumi tangu nyumba/kiwanja chako kiuzwe kwa kuwa sheria ya ardhi imetoa mpaka zaidi ya miaka kumi kwa aliye na lalamiko kulipeleka mahakamani. Hivyo chukua hatua sasa wala usiseme umechelewa katika hili.

MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
 
UNAPASWA KUFAHAMU YAFUATAYO YALIYOKIUKWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA ARDHI Na 4, 1999 , CAP 113;

1) MDAIWA ANAPOSHINDWA KUREJESHA FEDHA BAADA YA MWEZI MMOJA KUISHA TOKA MUDA WA MAKUBALIANO UFIKE TAMATI; MKOPESHAJI ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO;

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kuhusu deni husika na uvunjifu wa makubaliano ambapo atampatia muda wa MIEZI MITATU kulipa deni au kutimiza makubaliano kabla hajamchukulia hatua zaidi. (ikiwemo kupiga nyumba mnada)

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kuhusu madhara ya kutokulipa deni na kwamba MKOPESHAJI atamchukulia hatua baada ya kipindi cha miezi mitatu kuisha toka NOTISI ilipotolewa.

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kumueleza kuwa ana haki ya kwenda mahakamani kama hajaridhishwa na madai ya MKOPESHAJI wake.

SWALI, JE, HIZI NOTISI ZOTE ULIPATIWA?

2) KIFUNGU NAMBA 131 CHA SHERIA YA ARDHI, No 4 , 1999 , CAP 113; Kinamtaka mkopeshaji , kama hajalipwa deni, kupiga mnada nyumba husika.

Lakini kabla ya kupiga nyumba mnada, sharti AMPATIE MDAIWA NOTISI kuhusu kupigwa mnada kwa nyumba, na HATARUHUSIWA kuipiga nyumba mnada mpaka SIKU AROBAINI zipite toka NOTISI itolewe.

Je, ulipatiwa hizo notisi?

3) KIFUNGU NAMBA 132 CHA SHERIA YA ARDHI Na 4 , 1999 , CAP 113; Kinamtaka MKOPESHAJI kupiga nyumba mnada KWA BEI SAHIHI.

Nyumba inapopigwa mnada kwa bei ya kutupwa ; mwenye nyumba anaweza kwenda mahakamani kushitaki.

4) BENKI HAITAPEWA FIDIA YOYOTE endapo imekiuka taratibu za upigaji mnada wa nyumba. (132 -(4))

5) MNUNUZI WA NYUMBA atalipwa fidia stahiki endapo MAHAKAMA ITETENGUA UPIGAJI MNADA BATILI WA NYUMBA HUSIKA, NA MUUZAJI ATAWAJIBIKA KULIPA FIDIA HIYO.(134)

Petro E. Mselewa
 
UNAPASWA KUFAHAMU YAFUATAYO YALIYOKIUKWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA ARDHI Na 4, 1999.

1) MDAIWA ANAPOSHINDWA KUREJESHA FEDHA BAADA YA MWEZI MMOJA KUISHA TOKA MUDA WA MAKUBALIANO UFIKE TAMATI; MKOPESHAJI ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO;

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kuhusu deni husika na uvunjifu wa makubaliano ambapo atampatia muda wa MIEZI MITATU kulipa deni au kutimiza makubaliano kabla hajamchukulia hatua zaidi. (ikiwemo kuuza nyumba)

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kuhusu madhara ya kutokulipa deni na kwamba MKOPESHAJI atamchukulia hatua baada ya kipindi cha miezi mitatu kuisha toka NOTISI ilipotolewa.

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kumueleza kuwa ana haki ya kwenda mahakamani kama hajaridhishwa na madai ya MKOPESHAJI wake.

SWALI, JE, HIZI NOTISI ZOTE ULIPATIWA?

2) KIFUNGU NAMBA 131 CHA SHERIA YA ARDHI, No 4 , 1999 ; Kinamtaka mkopeshaji , kama hajalipwa deni, kuuza nyumba husika.

Lakini kabla ya kuuza nyumba, sharti AMPATIE MDAIWA NOTISI kuhusu kuuzwa kwa nyumba, na HATARUHUSIWA kuiuza nyumba husika mpaka SIKU AROBAINI zipite toke NOTISI itolewe.

Je, ulipatiwa hizo notisi?

3) KIFUNGU NAMBA 132 CHA SHERIA YA ARDHI Na 4 , 1999 ; Kinamtaka MKOPESHAJI kuuza nyumba KWA BEI SAHIHI.

Nyumba inapouzwa kwa bei ya kutupwa ; mwenye nyumba anaweza kwenda mahakamani kushitaki.

4) MKOPESHAJI hatapewa fidia yoyote endapo atakiuka taratibu za uuzaji wa nyumba. (132)

5) MNUNUZI WA NYUMBA atalipwa fidia stahiki endapo MAHAKAMA ITETENGUA UPIGAJI MNADA BATILI WA NYUMBA HUSIKA, NA MUUZAJI ATAWAJIBIKA KULIPA FIDIA HIYO.(134)
Kwa haya maelezo naaamini muulizaji wa hoja umeridhika, yamejitosheleza sana.

Cha kuongezea kukusaidia ni hapo katika hio Namba 3 (alioandika mkuu hapa), pindi mkopeshaji akiuza nyumba/mali kwa bei ya kutupa unaweza kwenda mahakamani;

1) Kuweka pingamizi la uuzaji nyumba.

2) Kama imeshauzwa, basi anaweza kwenda mahakamani kuomba kubatilisha mauzo/mkataba. (Kigezo kikuu kiwe nyumba imeuzwa kimyume na sheria/chini ya thamani.)

NB Hapa ili urahisishe kushinda case basi atafute WATATHMINI WA ARDHI (LAND EVALUATORS) wapo wizara ya ardhi, unawapa fees yao waje kuitathmini thamani ya ardhi/nyumba na watakupa documents za thamani ya nyumba hio. Halafu mahakama itapitia uwiano kati ya bei iliouzwa na thamani halisi ya nyumba. Na kama mahakama itajiridhisha kua nyumba imeuzwa chini ya thamani, basi kuna mawili;
a) atalipwa hela iliobakia.
b) mkataba wa mauzo ya nyumba utavunjwa, na atarudishiwa nyumba yake.

*inategemea na atakacho omba mahakama impatie wakati anadungua case.

3) Pia kama ana mke ambae haku sign document za mkopo bank anaweza akaweka pingamizi la hayo mauzo, mkopo kua batili kwasababu nyumba ni ya familia, na si yake peke yake (matrimonial property).
 
Ahsante sana Mkuu kwa ushauri wako. Lakn hapohapo nikuulize tena,hili suala ni la tokea 2016.
- Je,bado sheria inaruhusu kufungua shauri?
- Je hata ikitokea mahakama ikabatilisha mnada,atalazimika kulipa riba na faini kwa muda huo wote ambao shauri litasikilizwa hadi kufikia uamuzi?
Mkuu endelea kunisaidia ili hata mimi nimsaidie huyu ndugu kwani ni kama anaenda kupoteza nyumba yake.
Hiyo riba na faini inatoka kwa nani kwenda kwa nani, na kwasababu zipi?

Benki haikufuata taratibu stahiki za upigaji nyumba mnada, hivyo haina haki ya kupata fidia yoyote.

Endapo mahakama itatengua uuzwaji wa nyumba, hiyo nyumba itarudi kwenye umiliki wa muhusika.

Infact, muhanga wa uuzwaji wa nyumba, katika hali hii, ndio anapaswa kulipwa fidia. (if any)

Mortgage inaweza kurudi katika nafasi ya awali, na muhusika atapaswa kurejesha fedha kwa utaratibu sahihi.
 
Kwa haya maelezo naaamini muulizaji wa hoja umeridhika, yamejitosheleza sana.

Cha kuongezea kukusaidia ni hapo katika hio Namba 3 (alioandika mkuu hapa), pindi mkopeshaji akiuza nyumba/mali kwa bei ya kutupa unaweza kwenda mahakamani;

1) Kuweka pingamizi la uuzaji nyumba.

2) Kama imeshauzwa, basi anaweza kwenda mahakamani kuomba kubatilisha mauzo/mkataba. (Kigezo kikuu kiwe nyumba imeuzwa kimyume na sheria/chini ya thamani.)

NB Hapa ili urahisishe kushinda case basi atafute WATATHMINI WA ARDHI (LAND EVALUATORS) wapo wizara ya ardhi, unawapa fees yao waje kuitathmini thamani ya ardhi/nyumba na watakupa documents za thamani ya nyumba hio. Halafu mahakama itapitia uwiano kati ya bei iliouzwa na thamani halisi ya nyumba. Na kama mahakama itajiridhisha kua nyumba imeuzwa chini ya thamani, basi kuna mawili;
a) atalipwa hela iliobakia.
b) mkataba wa mauzo ya nyumba utavunjwa, na atarudishiwa nyumba yake.

*inategemea na atakacho omba mahakama impatie wakati anadungua case.

3) Pia kama ana mke ambae haku sign document za mkopo bank anaweza akaweka pingamizi la hayo mauzo, mkopo kua batili kwasababu nyumba ni ya familia, na si yake peke yake (matrimonial property).
Asante, KAKA MSOMI.

Endapo muhusika alipata mkopo kwa kuweka rehani nyumba bila ridhaa ya mkewe, nadhani hii kitu itakuwa batili tangu mwanzo.

Yote yaliyofuata baada ya hapo nayo ni batili.

Kwa mujibu wa kifungu namba 126 cha sheria ya ardhi, muhusika anaweza kufunguliwa mashitaka binafsi.
 
Ndiyo maana najivunia kuwa member wa JF kwani kimsingi kuna watu makini wenye majibu sahihi kwenye maswali magumu kwa wakati sahihi.
Niwashukuruni saana wataalamu wangu,ktk hili mmenikidhia haja yangu na huyu ndugu yangu. Ni kesho tu namwandamanisha kwa wanasheria tuianze safari ya kuitafuta haki,maana kuna mijitu(MUNGU anisamehe) imekuwa michovu ya kutafuta mali kwa njia halali na badala yake imebaki kusubir watu waliopata matatizo tu ili yaweke dhuluma..!
 
Mshauri aendelee na maisha yake, maana aliye nje ndio mwenye makosa, life goes on maana alie ndani ata endelea ku apeal tu!
Vipesa kiduchu alivyo baki navyo heri atafute cha kufanya maana asipo kuwa mwangalifu mawakili watazimaliza zote walahi!
D51FCFEB-FC78-4DED-AFEF-668991AE7DBC.jpeg
 
UNAPASWA KUFAHAMU YAFUATAYO YALIYOKIUKWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA ARDHI Na 4, 1999 , CAP 113;

1) MDAIWA ANAPOSHINDWA KUREJESHA FEDHA BAADA YA MWEZI MMOJA KUISHA TOKA MUDA WA MAKUBALIANO UFIKE TAMATI; MKOPESHAJI ANAPASWA KUFANYA YAFUATAYO;

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kuhusu deni husika na uvunjifu wa makubaliano ambapo atampatia muda wa MIEZI MITATU kulipa deni au kutimiza makubaliano kabla hajamchukulia hatua zaidi. (ikiwemo kupiga nyumba mnada)

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kuhusu madhara ya kutokulipa deni na kwamba MKOPESHAJI atamchukulia hatua baada ya kipindi cha miezi mitatu kuisha toka NOTISI ilipotolewa.

-Kumpatia NOTISI mdaiwa kumueleza kuwa ana haki ya kwenda mahakamani kama hajaridhishwa na madai ya MKOPESHAJI wake.

SWALI, JE, HIZI NOTISI ZOTE ULIPATIWA?

2) KIFUNGU NAMBA 131 CHA SHERIA YA ARDHI, No 4 , 1999 , CAP 113; Kinamtaka mkopeshaji , kama hajalipwa deni, kupiga mnada nyumba husika.

Lakini kabla ya kupiga nyumba mnada, sharti AMPATIE MDAIWA NOTISI kuhusu kupigwa mnada kwa nyumba, na HATARUHUSIWA kuipiga nyumba mnada mpaka SIKU AROBAINI zipite toke NOTISI itolewe.

Je, ulipatiwa hizo notisi?

3) KIFUNGU NAMBA 132 CHA SHERIA YA ARDHI Na 4 , 1999 , CAP 113; Kinamtaka MKOPESHAJI kupiga nyumba mnada KWA BEI SAHIHI.

Nyumba inapopigwa mnada kwa bei ya kutupwa ; mwenye nyumba anaweza kwenda mahakamani kushitaki.

4) BENKI HAITAPEWA FIDIA YOYOTE endapo imekiuka taratibu za upigaji mnada wa nyumba. (132 -(4))

5) MNUNUZI WA NYUMBA atalipwa fidia stahiki endapo MAHAKAMA ITETENGUA UPIGAJI MNADA BATILI WA NYUMBA HUSIKA, NA MUUZAJI ATAWAJIBIKA KULIPA FIDIA HIYO.(134)
Boss kama nilitaka msaada hapa umenipa zaidi,yaani hadi darasa la sheria umenipa tena lililojaa kisawasawa. Nimekuelewa mkuu!
 
Back
Top Bottom