Benki sasa zinaishiwa shilingi, hii tunaitaje kiuchumi?

Benki sasa zinaishiwa shilingi, hii tunaitaje kiuchumi?

Baada ya benki kuishiwa Dola, Sasa benki nyingi zinaishiwa shilingi.

Nini maana yake?

Je, watu wanahamisha mitaji kwenda kuitafuta Dola?

Je, mzunguko wa shilingi umezuiwa na Dola?

Je, Wafanyabiashara hawauzi bidhaa na kupata shilingi?

Je, Wafanyabiashara Sasa wanapokea dola kutoka kwa wateja Ili waweze kuagiza mizigo, kwa sababu kuagiza mzigo China lazima uwe na Dola?
Usijipe hofu ndgu Kasomea Kitabu kinachoitwa The power of now E Tole Hela zenyewe hatujawahi pata
 
Benki kuna uhaba wa hela,cashier mmoja wa benki nimeisahau jina ameniambia kwa siku walikuwa wanapokea Bilioni 2 wanatoa Milioni 500 sasa hivi wanatoa bilioni wananapokea Milioni 500
 
Ww ndio huna pesa kwenye account yako kiongozi.
Eti jina la Bank kasahau ila alie mwambia n jamaa yake.
Asante.
 
Nawashauri kununua dhahabu na kuficha.....achana na benki na shilingi na bla blah
 
Kwahilo sishangai maana kipindi hiki sio fedha tu hata akili hatuna. 🤣
 
Benki kuna uhaba wa hela,cashier mmoja wa benki nimeisahau jina ameniambia kwa siku walikuwa wanapokea Bilioni 2 wanatoa Milioni 500 sasa hivi wanatoa bilioni wananapokea Milioni 500
Kama Bank wana pokea kiasi kidogo kuliko wanachotoa ni jambo zuri kwa uchumi. Pesa haipaswi kuishi bank, pesa inatakiwa ifanye kazi mtaani, na kwa wale wanao weza wanawekeza kwenye masoko ya hisa, na pesa inaendelea kuzungushwa na makampuni kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa au kununua hisa za makampuni mengine na hili ni endelevu.
Bank pia wananwekeza na kununua hisa na kuweka kwenye miradi kwa riba kubwa zaidi, ukiona pesa haikai bank ujue wanannchi tumeanza kuelewa matumizi ya pesa.
 
Back
Top Bottom