Benki tatu kuwekwa chini ya uangalizi: Hii ni sawa na kusema baada ya miezi hiyo zitafungwa

CHAMA CHAMA

Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
77
Reaction score
58
Siku chache zilizipita , BOT imezifungia benki tano na kuziweka chini ya uangalizi benki nyingine tatu ambazo ni Kilimanjaro corperative Bank, Tanzania Women's Bank and Tandahimba Community Bank Limited.

Nimejaribu kutafakari nini maana ya kusema to the public kuwa unaziweka chini ya uangalizi. Hii ni kusema kuwa umezipa muda wa miezi sita tu then zifugwe. Naona bado hujanielewa, nina maana kuwa hakuna mtu ambaye mwenye deposit kule alafu akaacha hela zake kule zimekaa tu na wakati hapo hapo BOT imesema katika Benki zilizofungwa kiwango cha juu cha kurudishiwa hela kwa wale wenye deposit kule ni TZS 1,500,000/= tu.

Sasa sina uhakika kama watanzania wenye deposit kule au Benki nyingine zenye deposit zitaacha hela zao kule. Kwahiyo baada ya Miezi sita sina uhakika sana kama hizi benki zitaendelea kuwepo.

Unashauri BOT ingetumia ushauri gani katima bank hizi tatu. Toa maoni yako
 
Huku ndiko kuishi kama shetani!!
Sababu ni serikali kukaza vyuma na kusema kweli hivi vibenki vidogo vidogo ndio vilikuwa mkombozi kwa mwanachi wa chini licha ya Riba kuwa kubwa kiasi.
 
Hapo hakuna ushauri wala mshauriwa.

Zaidi, Katoe hela zako tu kwenye hizo benk tajwa la sivyo utakuwa na 70m yako huko benk ila ikifirisiwa wamesema utapata 1.5m regardless ya kiwango cha fedha ulichokuwa nacho.

Akili kum kichwa.
 
Kwakweli inabidi maamuzi yanayochukulia na viongozi wetu lazima watafakari impact yake baadae. Ila labda uamuzi wao ni kuziondoa sokoni , so kama huo ndo uamuzi wao basi maamuzi waliyochukua yatafanikisha uamuzi wao, kama sivyo basi nadhani ni muda muafaka wa kujifunza impact itakayotokea
 
Lakini sasa iko chini ya usimizi wa BOT. Sio habari njema hii, don't u think?

Brother Jero ,
Mkuu,
Banks zote huwa chini ya uangalizi wa BOT from stage zero (initial ) to their maturity stages though BOT keeps its wide eyes on monitoring and evaluating the financial cycling.

Ila sasa, majanga rasmi huja pale inapotangazwa kama hicho kilichotangazwa mbele za umma kuwa sasa rasmi bank fulani na fulani zitakuwa chini ya uangalizi na usimamizi wa BOT.

Kwa kifupi, hatua hiyo inapotangazwa ni kwamba asilimia za kufutwa na kufirisiwa huwa ni 90%.
Kupona kutoka kwenye hilo panga la BOT huwa ni 10% tu.

Vijana waongeze maombi sasa ili nao wasijeishi kama mapepo na mashetani baada ya kufutwa benk zao.
 
Huku ndiko kuishi kama shetani!!
Sababu ni serikali kukaza vyuma na kusema kweli hivi vibenki vidogo vidogo ndio vilikuwa mkombozi kwa mwanachi wa chini licha ya Riba kuwa kubwa kiasi.
Itakuwa ni vita vya kiuchumi mbona uchumi unakuwa au nao ni wapiga dili kama wale wakulima wa mbaazi.Kuucheza mpira ni rahisi sana ukiwa nje.
 
ningekua ninamzigo huko baada ya tamko account yangu ya huko ingekua inasoma 5000/- tu nyinhine zote ninhehamisha muda huohuo
Mimi ingesoma zero (0). Bora hata wewe unawajali kuwaachia 5,000/=
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…