LUTULWITU
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 584
- 983
Bro unawajua loan board/bodi ya mikopo?wewe inaonesha ni pumbavu mikopo ya kijingajinga kama ada ni upuuzi kwa nchi kama Tanzania
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bro unawajua loan board/bodi ya mikopo?wewe inaonesha ni pumbavu mikopo ya kijingajinga kama ada ni upuuzi kwa nchi kama Tanzania
Mwanafunzi, hauna mwanafunzi haupati mkopo, hapa sasa itabidi tutafute hela ya kulewea.Dhamana ya mkopo ni nini
Jitahd ku balance stories , mshahara wa ki tz hasa za wa wajiriw wa kawaid si kipato/mshahar stamilivu kbsa.Ni kweli kuna ku save then kuna mambo yanapo ingiliana unatumia akiba inapofika mda unaona akiba haitosh what next?
Hongoreni CRDB wale wateja wa DCB na TPB wanalalamka kidigitali hawaeleweki na kianalogia hivyo hiyo sasa wateja wao sijui wanakopaje hasa watumishi. Wenzenu wanachangamka nyie mnalalahii ni indicator ya umaskini uliopo Tanzania. kwamba watu hawana uhakika wa kulipa hadi karo za wanafunzi.
Halafu rais anasifiwa kwenye kila kitu hadi ujinga
Ilikua shillingi ngapi?Nimeona sms Mimi nikasema ngoja nikope nigungulie genge naambiwa niweke control number ya mwanafunzi. Imeniuma , pesa nimeona kabisa.
Siwezi kukopa kwaajili ya ada ya mtoto wakati shule ni bure. Kiingereza tu ambacho rasi Simba anakifundisha kwa laki 2 tu ndicho mzazi ukilipie milioni 10 ndani ya miaka 4?
Nimesoma na hao waliosoma private schools hawana maajabu yoyote.
Kwahiyo mnaficha umaskini kwa kuanzisha credit economy ?Hujielewi nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani watu wanaishi kwa credit card kila kitu wanakopa
Tatizo lako ulofa na huna exposure ya nje maskini mkubwa wewe na utakufa lofa na kingereza chako cha indicator
Hivi huko hawana taarifa kuwa hakuna ada? Ama huwa hawamsikilizi mama?
Dar es Salaam. Tarehe 7 Januari 2025: Katika kuukaribisha mwaka mpya 2025, Benki ya CRDB imezindua mikopo ya ada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini kote. Mikopo hiyo inayoitwa Ada Fasta ni mwendelezo wa juhudi za Benki ya CRDB kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto za kifedha wanakokabiliana nazo.
Akizindua mikopo hiyo inayotolewa kupitia Programu ya SimBanking, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo amesema kila mzazi au mlezi mwenye uhitaji anaweza kupata mkopo huo ili kumruhusu mwanafunzi kuendelea na masomo kulingana na ratiba ya muhula husika.
![]()
“Mteja anaweza kukopa mpaka shilingi milioni 3 ambazo atazirudisha ndani ya miezi sita. Riba ya mkopo huu ni asilimia 13 tu mwaka, gharama ndogo zaidi ukilinganisha riba iliyopo sokoni. Nawakaribisha wazazi wote kuitumia fursa hii kuhakikisha watoto wetu wanasoma bila tatizo lolote la ada,” amesema Nshekanabo.
Mkurugenzi huyo amesema wameizindua huduma hiyo kipindi hiki wakitambua kuwa Januari ni mwezi wenye changamoto nyingi za kifedha zinazotokana na mahitaji makubwa yanayokuwepo ikiwamo ada za wanafunzi, kodi ya nyumba na mahitaji mengine muhimu hasa baada ya kila mtu kuwa ametumia kiasi kikubwa cha fedha kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka.
Ikiwa Benki inayomsikiliza mteja na kumweka mbele katika mikakati ya biashara, amesema wakati wote wanabuni huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja na Januari hii wamekuja na jambo jipya mahususi kwa kila mzazi au mlezi wa mwanafunzi nchini.
Zaidi ya muongo mmoja Benki ya CRDB ilizindua nakuutambulisha Mfumo wa Makusanyo ya Ada Shuleni yaani School Fees Management System ambao mpaka sasa unatumiwa na zaidi ya shule 1,000 nchini kote ambazo sasa wanafunzi wake watanufaika na mikopo hii iliyozinduliwa.
“Hii ni fursa kwa shule zote binafsi nchini kujiunga na mfumo huu wa makusanyo ya ada ii kutoa fursa kwa wazazi kukopa ada wakati wowote watakapohitaji ili watoto waendelee na masomo yao. Wazazi wote waliopo kwenye shule zinazoutumia mfumo huu wawe ni wateja wetu ama la, wanayo fursa ya kunufaika na mikopo hii,” amesema Nshekanabo.
Mzazi au mlezi atakayeomba mkopo huu, amesema atapata fedha husika zitakazoingizwa kwenye akaunti ya shule moja kwa moja na yeye kupata risiti ya uthibitisho kwamba amelipa ada inayotakiwa kwa ajili ya mtoto wake.
Kwa kuwawezesha wazazi na walezi kulipa ada kwa wakati, Nshekanabo amesema wana imani watakuwa wamesaidia kuboresha elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo yao bila vikwazo huku shule zikiweza kujiendesha na kutoa maarifa bora yanayohitajika kwa watoto wa Kitanzania.
Kwa mzazi au mlezi ambaye ameajiriwa na mshahara wake unapitia Benki ya CRDB, anaweza kupata mkopo wa ada kwa kuingia kwenye Programu ya SimBanking kisha akabofya sehemu ya mikopo ambako atatakiwa kuingiza ‘control number’ aliyotumiwa na shule kwa ajili ya malipo ya ada na programu itamwonyesha kiasi cha juu anachoruhusiwa kukopa.
Baada ya hapo, mteja atatakiwa kuingiza kiasi anachokitaka na kupendekeza muda anaotaka kulipa deni hilo ndani ya miezi sita ili kukamilisha maombi yake. Akishafanya hivyo, Benki ya CRDB itaingiza fedha zilizoombwa kwenye akaunti ya shule anakosoma mtoto hivyo kumruhusu asome kwa utulivu.
Ukiacha faida zilizopo kwa pande zote mbili yaani shule na mzazi au mlezi, mfumo wa makusanyo ya ada wa Benki ya CRDB ni rahisi kuutumia kwani mteja anaweza kulipa ada kupitia SimBanking, CRDB Wakala au kutembelea tawi la Benki ya CRDB.
Vilevile, mteja anaweza kulipa ada ya mwanafunzi kupitia M-pesa, Tigopesa, Airtel Money au Halopesa bila kulazimika kupeleka risiti ya malipo shuleni kwani taarifa huwa zinafika huko moja kwa moja. Kwa upande wa shule, faida iliyopo ni kwamba inakusanya ada kwa wakati na kupata taarifa papo hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mikopo ya ada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini kote (Ada Loan) iliyozinduliwa na Benki ya CRDB ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake kwa kuwawezesha mkopo ili kukabiliana na changamoto za kifedha hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka. Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Benki hiyo, jijini Dar es salaam leo.
![]()
Rais wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu nchini (TAPIE), Mahmod Mringo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mikopo ya ada kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini kote (Ada Loan) iliyozinduliwa na Benki ya CRDB ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake kwa kuwawezesha mkopo ili kukabiliana na changamoto za kifedha hasa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka. Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Benki hiyo, jijini Dar es salaam leo.
😀😀😀😀Habari,
Hawa ndiyo CRDB BANK PLC wamezindua ADA LOAN ambayo haipo:-
"UMEKWAMA ADA YA SHULE AU CHUO? Pata mkopo wa ada hadi Milion 12 kupitia SimBanking App> Chagua Mkopo> ADA Loan > Namba ya malipo > Kiasi. BenkiniSimBanking"
Hivi tatizo ni nini hasa kuzindua huduma ambayo haiko tayari??
Hivi
Ni ya kweli sema watu hawajapenda issue ya control no basi hasira tupu! Walitaka wadake wakapige gambe😀😀😀😀
CRDB waongo waongo flani hivi
Hamkosagi lawama wabongo..khaaa...Nashauri tu mfumo wakulipa ada wangelipa ada ya mwanafunzi mwaka mzima na marejesho mzazi alipe mwaka mzima hadi muda wa kukopa ada ya mwaka unaofata. Riba hata ingekuwa 20% sio mbaya.