Benki ya CRDB yafanya kufuru, yatoa mikopo hadi mil 50 bila riba

Benki ya CRDB yafanya kufuru, yatoa mikopo hadi mil 50 bila riba

Salahan

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
2,963
Reaction score
3,685
Akizungumza na Nipashe iliyotaka kupata ufafanuzi juu ya huduma hiyo jana, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tuli Mwambapa, alisema kiwango cha chini cha mikopo hiyo ni Sh. 500,000 na cha juu ni Sh. milioni 50."Kiwango cha juu ni Sh. milioni 20 kwa Mastercard Gold Credit (wateja wa kawaida) na kwa wale wenye kadi za Mastercard World Reward (wateja wakubwa) ni Sh. milioni 50," alisema.

Mkurugenzi huyo alisema mikopo kwa wateja wote wenye Mastercard Gold Credit itatolewa bila riba kwa siku 45 za mwanzo wakati kwa wateja wenye Mastercard World Reward itatolewa bila riba kwa siku 50 za kwanza.Mwambapa alisema huduma hiyo ilianza kutolewa rasmi na CRDB Februari 21.

Hata hivyo, kwa kipindi kinachozidi siku hizo kabla ya mkopo kumalizika kurejeshwa mteja atatozwa riba ya asilimia tano, alisema Mwambapa. Mama Mwambapa alitaja sifa za kupata kadi hizo kuwa ni mteja wa CRDB anayelipwa mshahara kupitia benki hiyo.

"Sifa nyingine ni wateja ambao kampuni zao zina mkataba wa makubaliano na CRDB kuhusu mikopo binafsi, na wateja wenye vikundi vya wajasiriamali wadogo na wa kati na kampuni kubwa ambazo zina ubia na CRDB," alisema.

Mkurugenzi huyo pia alisema ili mteja apate mkopo, anatakiwa ajaze fomu ya maombi ambayo yatafanyiwa tathmini kwa taratibu za benki kupitia idara ya mikopo.
Alisema mteja atakayekidhi vigezo atapewa mkopo na anaweza kutoa fedha kupitia kadi yake ya ATM au kwa kufanya muamala kwa njia ya mtandao.

"Katika kiasi anachopewa mteja kama mkopo, asilimia 30 anaweza kuchukua fedha taslimu kupitia ATM wakati asilimia 70 anatakiwa kutumia mashine maalum za malipo.

FROM IPP NIPASHE
 
Benki ya CRDB inatoa mikopo ya kuanzia Sh. Laki 5 hadi Sh. Milioni 50 isiyo na riba ndani ya siku 50 za kwanza, kwa wateja wenye kadi zake mpya za kutolea fedha za Mastercard Gold Credit na Master Card World Reward

Huduma hiyo ilianza kutolewa rasmi Februari 21, mikopo hiyoitaanza kutozwa riba ya asilimia 5 baada ya siku 50 za mwanzo kupita

IMG-20180316-WA0019.jpg
 
Si rahisi kivihivyo!!

Ni vizuri kusoma kwa makini mkataba wa kupewa mkopo kabla ya kuukubali na kuusaini kisa tu umevutiwa na lugha tamu ya kibiashara kama hii.
 
Ndiyo credit card zinavyofanya kazi. Ila zina gharama nyingi sana za mitego. Hii ya mkopo wa "bure" ni hook ya kukufanya mteja uingie na uwe teja, baada ya hapo ni maumivu kwa kuenda mbele
 
Safi sana,ndiyomaana simenti imeshuka sana bei,sabuni,mafuta ya kupikia,bati nk.Tanzania bana ni vicheko tu.
 
Waangalia akaunti yako imetuna kiasi gani. kama una akiba ya kutosha na hela za kwenye akiba yako wanaweza kukopesha wateja wengine kwa riba kubwa basi wanakupa "dakika 20 za bure" ukilipa tsh 1000 tu.
 
Tuwekeeni gharama za matumizi ya MasterCard tafsdhali ili tuciingie kichwax2
 
!
!
Huo mkopo haukawii kuitwa "mkopo wa maghufuli" .

Subiri tu muone.

Maana awamu hii watu wamejifunza kucheza kulingana na mdundo.

Just Praise Me
 
Bank wakiwa wanatoa mkopo wanakuwaga kama malaika, Siku wanataka pesa yao huja kama majambazi fyuuuu ndukiiii sizitaki mbichi hizi.
 
Hii ni mastercard credit services ..it has come to the right time atleast it will boost cashless spending and boost in the economy.Majority will be able to pay on P.O.S machine on that 70% remaining balance.I think even baclays bank has this services but CRDB in a way are very good in marketing
 
Back
Top Bottom