Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

Mwigulu anasemaje na zile namba E za magari, harusi na blabla nyinginezo, PhD yake inamsaidia nini yeye na jamii anayoitumikia
 
Acha kuwatetea chief. Kiuhalisia hali ni mbaya sana mitaani,gharama za maisha zipo juu sana. Uchumi wetu ungekuwa juu Hali isingekuwa hivi ilivyo chief
Unaijua Hali mbaya sana? Tanzania Ina watu wangapi na ripoti imetaja watu wangapi?
 
Mwigulu anasemaje na zile namba E za magari, harusi na blabla nyinginezo, PhD yake inamsaidia nini yeye na jamii anayoitumikia
Huyo Mwigulu, anatuona sisi watanzania kuwa ni watu wajinga sana wa kuweza kutudanganya wakati wote!
 
Unaijua Hali mbaya sana? Tanzania Ina watu wangapi na ripoti imetaja watu wangapi?
Sasa kati ya watanzania milioni 60, taarifa ya Benki ya Dunia imesena watu zaidi ya milioni 17, walikuwa wanaishi chini ya Dollar moja ya marekani kila siku.

Hiyo ni hali mbaya kupita maelezo!
 
huna haja ya kuhurumia waTanzania wenye bidii wanaoendelea kuchapa kaz zao halali za kijipatia kipato kwa Amani...

hakuna umaskini huo unao uhubiri Tanazani tuko vizuri, uelekeo wa kiuchumi ni mzuri zaidi....
Safi sana Bwana Mwigulu. Msalimie chupikizi wa Feza
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku, ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake , hakuna Chai wala uji asubuhi

Nakulilia Tanzania
Hii niliwahi kuiona Kwa Matajiri flani WA Kiarabu Mkoa Fulani .Zinanunuliwa dagaa zile za Mwanza Debe mchana kila siku dagaa WA kukaushwa na mafuta na chumvi Tu na ugali jioni linachemshwa sufuria kubwa la chai ya rangi. Sukari na kitafunwa chochote juu yako. Kila siku.
 
Hiyo Temeke na Mbagara ni kawaida
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku, ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake , hakuna Chai wala uji asubuhi

Nakulilia Tanzania
Huu ni uongo aisee
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Mshukuru sana Mungu kama anakuwezesha kula milo mitatu
Huyo atakuwa miongoni ya wale chawa wa Mama, ambao wao ni wanufaika wakubwa wa mfumo huu wa utawalaπŸ˜…
 
Wewe
Acha uongo na chuki zako dhidi ya serikali, kweli mlo mmoja ili khali debe la mahindi kwa sasa ni sh 8000!!!!?
Unadhani kwa kuwa wewe unawezapata hiyo sh 8000 kwamba wengine nao wanaweza? Au kwa kuwa u miongoni au uko upande wa wasiofahamu umaskini wa Tanzania ccm ndiyo waona furaha.
 
Maelezo yako haya ni takataka ila sishangai maana tayari umedhihirisha kuwa wewe ni miongoni mwa wanufaika wa wanufaika wa umaskini wa mtanzania.

Kwamba akili yako inakwambia watu wakiongezeka umaskini unaongezeka? Kweli hii ni rubbish.

Vipi china idadi yao?
 
Kwa ujumla umaskini wa Tanzania, kwa wananchi walio wengi, ni wa kutisha.

Huko vijijini, hasa baadhi ya kanda usiseme. Kuna sehemu huko Tabora, wilayani Nzega, kijijini tulismama. Wakaja watoto, wanatia huruma kweli. Tulikuwa na ndizi kwenye gari, nikasema wapeni hao watoto. Akawepo na mama mzee mtu mzima. Akapewa ndizi 2. Cha ajabu alikula pale pale, baada ya kumaliza zile ndizi, akachukua na maganda ya ndizi, akayala yote, akitupa kile kikonyo cha mwishoni tu. Mtu yule inaonekana alikuwa na njaa sana!! Niliamua kumpa elfu 10, aende akanunue chochote. Akawa ameduwaa, midomo tu inaweweseka huku akinitazama na kushukuru tena na tena.

Na huenda wa hivyo, kwa nchi nzima wapo wengi. Wengine wanalalamikia maisha magumu kwa sababu bei ya mafuta ya kuweka kwenye vitz zao na Ist ipo juu, lakini kuna watu hata kula tu ni shida hasa.
 
Hali inatisha mno!πŸ™†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…