Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Benki ya Dunia, inaeleza kuwa watanzania waliokuwa wakiishi katika hali ya umasikini sana, chini ya dollar moja ya kimarekani, imeongezeka kutoka watanzania milioni 14 mwaka 2018 hadi kufikia zaidi ya watanzania milioni 17 mwishoni maa mwaka 2023.

Taarifa hiyo inapingana vikali na taarifa za (kupikwa) zinazotolewa kila mwaka na serikali hii ya CCM, kuwa hali ya maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka!
Mwigulu anasemaje na zile namba E za magari, harusi na blabla nyinginezo, PhD yake inamsaidia nini yeye na jamii anayoitumikia
 
Acha kuwatetea chief. Kiuhalisia hali ni mbaya sana mitaani,gharama za maisha zipo juu sana. Uchumi wetu ungekuwa juu Hali isingekuwa hivi ilivyo chief
Unaijua Hali mbaya sana? Tanzania Ina watu wangapi na ripoti imetaja watu wangapi?
 
Mwigulu anasemaje na zile namba E za magari, harusi na blabla nyinginezo, PhD yake inamsaidia nini yeye na jamii anayoitumikia
Huyo Mwigulu, anatuona sisi watanzania kuwa ni watu wajinga sana wa kuweza kutudanganya wakati wote!
 
huna haja ya kuhurumia waTanzania wenye bidii wanaoendelea kuchapa kaz zao halali za kijipatia kipato kwa Amani...

hakuna umaskini huo unao uhubiri Tanazani tuko vizuri, uelekeo wa kiuchumi ni mzuri zaidi....
Safi sana Bwana Mwigulu. Msalimie chupikizi wa Feza
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku, ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake , hakuna Chai wala uji asubuhi

Nakulilia Tanzania
Hii niliwahi kuiona Kwa Matajiri flani WA Kiarabu Mkoa Fulani .Zinanunuliwa dagaa zile za Mwanza Debe mchana kila siku dagaa WA kukaushwa na mafuta na chumvi Tu na ugali jioni linachemshwa sufuria kubwa la chai ya rangi. Sukari na kitafunwa chochote juu yako. Kila siku.
 
Hiyo Temeke na Mbagara ni kawaida
 
Temeke kwa sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku, ugali mtupu kwenye familia unapikwa saa 10 jioni , kila mtu atafute mboga yake , hakuna Chai wala uji asubuhi

Nakulilia Tanzania
Huu ni uongo aisee
😆😆😆
 
Wewe
Acha uongo na chuki zako dhidi ya serikali, kweli mlo mmoja ili khali debe la mahindi kwa sasa ni sh 8000!!!!?
Unadhani kwa kuwa wewe unawezapata hiyo sh 8000 kwamba wengine nao wanaweza? Au kwa kuwa u miongoni au uko upande wa wasiofahamu umaskini wa Tanzania ccm ndiyo waona furaha.
 
umeandika kishabiki na ki chuki sana dhidi ya ccm, kwa taarifa yako hiyo ripoti siyo ya kweli kwanza lete sorce yake imetoka wapi? licha ya hivyo haohao wanaosema hivyo ndiyo wanaoletaga hizo taarifa sasa wanasema na kujipinga wenuyewe? wewe utakuwa na matatizo ya akili hakuna kitu kama hicho pia ukiona idadi inaongezeka ya maskini ujue pia idadi ya watu sasa hivi ni kubwa sana
Maelezo yako haya ni takataka ila sishangai maana tayari umedhihirisha kuwa wewe ni miongoni mwa wanufaika wa wanufaika wa umaskini wa mtanzania.

Kwamba akili yako inakwambia watu wakiongezeka umaskini unaongezeka? Kweli hii ni rubbish.

Vipi china idadi yao?
 
Kwa ujumla umaskini wa Tanzania, kwa wananchi walio wengi, ni wa kutisha.

Huko vijijini, hasa baadhi ya kanda usiseme. Kuna sehemu huko Tabora, wilayani Nzega, kijijini tulismama. Wakaja watoto, wanatia huruma kweli. Tulikuwa na ndizi kwenye gari, nikasema wapeni hao watoto. Akawepo na mama mzee mtu mzima. Akapewa ndizi 2. Cha ajabu alikula pale pale, baada ya kumaliza zile ndizi, akachukua na maganda ya ndizi, akayala yote, akitupa kile kikonyo cha mwishoni tu. Mtu yule inaonekana alikuwa na njaa sana!! Niliamua kumpa elfu 10, aende akanunue chochote. Akawa ameduwaa, midomo tu inaweweseka huku akinitazama na kushukuru tena na tena.

Na huenda wa hivyo, kwa nchi nzima wapo wengi. Wengine wanalalamikia maisha magumu kwa sababu bei ya mafuta ya kuweka kwenye vitz zao na Ist ipo juu, lakini kuna watu hata kula tu ni shida hasa.
 
Hali inatisha mno!🙆
 
Back
Top Bottom