Kwa ujumla umaskini wa Tanzania, kwa wananchi walio wengi, ni wa kutisha.
Huko vijijini, hasa baadhi ya kanda usiseme. Kuna sehemu huko Tabora, wilayani Nzega, kijijini tulismama. Wakaja watoto, wanatia huruma kweli. Tulikuwa na ndizi kwenye gari, nikasema wapeni hao watoto. Akawepo na mama mzee mtu mzima. Akapewa ndizi 2. Cha ajabu alikula pale pale, baada ya kumaliza zile ndizi, akachukua na maganda ya ndizi, akayala yote, akitupa kile kikonyo cha mwishoni tu. Mtu yule inaonekana alikuwa na njaa sana!! Niliamua kumpa elfu 10, aende akanunue chochote. Akawa ameduwaa, midomo tu inaweweseka huku akinitazama na kushukuru tena na tena.
Na huenda wa hivyo, kwa nchi nzima wapo wengi. Wengine wanalalamikia maisha magumu kwa sababu bei ya mafuta ya kuweka kwenye vitz zao na Ist ipo juu, lakini kuna watu hata kula tu ni shida hasa.