Msosi ushakuwa anasa kwenye nchi hii
- ma LC300 kila kona ya nchi kwa kila kiongozi kuanzia level ya idara serikalini
- Discovery ni kwa wale wote walioibukia kipindi cha mama na Forester, CRV, Volvo TC, Highlander, Vanguard, Lexus, Harrier kalio la ngedere, ML, BMW X1, 3 na 5 n.k ikiwa ndo watumishi wenye mianya yao na wafanyabiashara wa kawaida!
- Dualis, Rumion, IST, n.k imekuwa ni kwa wale waliokosa namna ndani ya kizimkazi
Sasa hilo kundi hapo juu, halizidi watu milioni moja kwa Dar es salaam na milioni 5 kwa nchi nzima.
Watu zaidi ya milioni 50 wa hili pande la ardhi, ndio hao wanasubiri ruzuku na makombo yanayobakia mezani baada ya hao wezi kusaza.
Nimesikia kiongozi wao kasema, mihela yote inaelekezwa kuhonga wapiga kura kwenye hizi siku 731.5 sijazo.
Ukiingia kwenye data zao, inflation haijawahi kufika 5, ukiangalia bidhaa moja kubwa inayoadhiri kila kitu, ime-inflate kwa takribani mara mbili na kusababisha kila kitu kitikisike, bado wasomi wanasema inflation ni 3.5%....nadhani mwenzao aliposema kule wanakopewa hayo maarifa ni jalalani, alikuwa 99.99% sawia.