Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

Benki ya Dunia imefichua ukweli kuwa lindi la umasikini linaongezeka kwa watanzania!

upotoshaji ni hatua mbaya sana ya kukosa hoja,
lakini zaidi sana imani potofu kwa watu wa nje, eti wao ndio wanatathmini, kipima na kutuambia sisi ni maskini na jamaa mvivu anaamini na kuchukua jambo hilo eti ndio hoja 😀

Tanzania hatujafukia na wala hatutafukia liwango cha umaskini kama ambavyo kimepotoshwa na wapotoshaji wanao sapotiana apo juu...

that is useles and none sense...
Peperusha benderaaaa Mkuu
20240314_012107.jpg
 
Umasikini ndio mtaji mkuu kwa CCM, yaani bila umasikini kusingekuwa na CCM, na pia kumbuka hawako tiyali kuona umasikini unaisha.

Angalia maeneo yenye umasikini mkubwa CCM ilivyo na nguvu
Kwa nini Chadema isitumie umaskini wa Watanzania kama kete ya kupata kura? Au nyie mnategemea itakuaje labda? 😁😁

Wale ambao Huwa mnawasomba kwenye maandamano na mnapigwa na picha ni maskini au matajiri?
 
Yule jamaa juzi kasema tuko vizuri tumejaza Namba E za Magari

Yule jama hana PhD fake kweli?
Wewe hujamuelewa maana yake.

Namba E kwenye chakula ni msosi wa mwisho yaani ugali na mboga mboga au uji Na ndizi kiufupi Ni msosi wa shambani
 
Tofauti na propaganda za serikali ya wanaccm za kila mwaka, kuwa uchumi wa watanzania unakuwa kwa asilimia kubwa kila mwaka, benki ya Dunia imewashushua waendesha propaganda hizo kwa kueleza ukweli kuwa hali ya maisha ya watanzania walio wengi, hususani wale wa hali ya chini, inazidi kudorora, jinsi miaka inavyokwenda mbele.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na Benki ya Dunia, inaeleza kuwa watanzania waliokuwa wakiishi katika hali ya umasikini sana, chini ya dollar moja ya kimarekani, imeongezeka kutoka watanzania milioni 14 mwaka 2018 hadi kufikia zaidi ya watanzania milioni 17 mwishoni maa mwaka 2023.

Taarifa hiyo inapingana vikali na taarifa za (kupikwa) zinazotolewa kila mwaka na serikali hii ya CCM, kuwa hali ya maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka!

Wakati watanzania kila mwaka wanaendelea kulalamika kuhusu gharama za maisha kupanda, serikali ya CCM, imeendelea kutupiga propaganda kuwa hali za maisha ya watanzania inazidi kuboreka kila mwaka.

Katika hali halisi, ingawa benki ya Dunia, imekiri kuwa kuna ongezeko la ukuaji wa uchumi nchini wa asilimia kama 5 hivi, lakini imetahadharisha kuwa ongezeko hilo linawafaidisha watanzania wachache ambao ni matajiri.

Kwa hiyo Benki ya Dunia imetutegulia kitendawili cha muda mrefu kilichokuwa kinawasunbua watanzania walio wengi kuwa maisha ya watanzania yanazidi kudorora jinsi siku zunavyozidi kusonga mbele.
Nchi ya Tanzania inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno
 
Msosi ushakuwa anasa kwenye nchi hii

  • ma LC300 kila kona ya nchi kwa kila kiongozi kuanzia level ya idara serikalini
  • Discovery ni kwa wale wote walioibukia kipindi cha mama na Forester, CRV, Volvo TC, Highlander, Vanguard, Lexus, Harrier kalio la ngedere, ML, BMW X1, 3 na 5 n.k ikiwa ndo watumishi wenye mianya yao na wafanyabiashara wa kawaida!

- Dualis, Rumion, IST, n.k imekuwa ni kwa wale waliokosa namna ndani ya kizimkazi

Sasa hilo kundi hapo juu, halizidi watu milioni moja kwa Dar es salaam na milioni 5 kwa nchi nzima.

Watu zaidi ya milioni 50 wa hili pande la ardhi, ndio hao wanasubiri ruzuku na makombo yanayobakia mezani baada ya hao wezi kusaza.

Nimesikia kiongozi wao kasema, mihela yote inaelekezwa kuhonga wapiga kura kwenye hizi siku 731.5 sijazo.

Ukiingia kwenye data zao, inflation haijawahi kufika 5, ukiangalia bidhaa moja kubwa inayoadhiri kila kitu, ime-inflate kwa takribani mara mbili na kusababisha kila kitu kitikisike, bado wasomi wanasema inflation ni 3.5%....nadhani mwenzao aliposema kule wanakopewa hayo maarifa ni jalalani, alikuwa 99.99% sawia.
Ukiona hayo hapo Juu ndio maendeleo yenyewe.

Inflation haikokotolewi Kwa bidhaa 1 Bali Kwa selected commodities na Kuna bass line.

Nilitegemea Machado muwe mnakuja na takwimu tofauti Sasa Kwa kuwa nyie ni mbumbumbu mnaleta blaa blaa.

Machadomo yamejaza wanasheria na mbulula wengine kujihami na kesi ila hakuna Wasomi na fani zingine 🤪🤪
 
Tutakapoacha kupokea misaada ndipo tutaanza kuendelea.
Misaada inawanufaisha wazungu zaidi kuliko waafrika.
Wanatupa misaada ili kuchukua baraka zetu,wao wakiendelea sisi tukiachiwa laana ya tuzidi kuwa masikini.
Wanajua wasipotusaidia tutaendelea tukiendelea watashindwa kutunyonya.
 
Lucas mwashambwa na ChoiceVariable watakuja hapa waseme wananchi wanabubujikwa machozi ya furaha kwa kazi nzuri ya sa100. Wakati watu wanashindia mlo mmoja, purchasing power iko chini, yaani ukienda sokoni unakuta mwanaume mzima ananunua nyanya za jero, vitunguu vya jero, hoho za jero, dagaa za buku..halafu unasema uchumi umekuwa.
Futseke zenu.!!
 
Ukweli usemwe kwamba GDP per capita na Purchasing power kwa Tanzania ndiyo vinavyotuangusha na ndo hasa maana ya uchumi kushuka..
Bado nauliza swali langu unaelewa maana ya uchumi kukua?

Ukitaja hizo parameters nitakwambia zimeongezeka na Sasa tuko kwenye wastani wa 2.8mln per year ambayo ni Juu ya wastani wa umaskini ndio maana tuko uchumi wa Kati wa Chini.

Swala liwe Je kiwango hicho kinatosha swali ni Bado hakitoshi more juhudi zinatakiwa.
 
Umasikini wa mtu,nchi ni matokeo ya fikra na sio mazingira
 
Lucas mwashambwa na ChoiceVariable watakuja hapa waseme wananchi wanabubujikwa machozi ya furaha kwa kazi nzuri ya sa100. Wakati watu wanashindia mlo mmoja, purchasing power iko chini, yaani ukienda sokoni unakuta mwanaume mzima ananunua nyanya za jero, vitunguu vya jero, hoho za jero, dagaa za buku..halafu unasema uchumi umekuwa.
Futseke zenu.!!
Watu wangapi hao wanaoshindia mlo mmja? Na wapi huko? Nitajie
 
Ufisadi wizi na upigaji ni asili ya mwafrika ni vile TU wewe haujapata nafasi hio ya kuiba
 
Watu wangapi hao wanaoshindia mlo mmja? Na wapi huko? Nitajie
Tema mate chini pana watu wanakula mara tatu kwa wiki unasema nini wewe yaani akila Leo kesho anapitisha kavu Hadi kesho kutwa angalau ili asife.
Ukishiba ni rahisi kuamini kila mtu anashiba
 
Tatizo watz wengi ni maskini ila lipo kundi la dogo la watu wenye vipato imara.
 
Nitolee takwimu zako uchwara hapa, purchasing power ya mtanzania iko chini sana, vipato vya watu havikidhi gharama za uendeshaji maisha.
Iko chini sana kulinganisha na wakati gani au na nani labda? Ingekuwa chini sana Uchumi unge collapse.

Nyie punguani wa chadomo mnachojua ni mambo ya sheria na kesi ,huku kwenye uchumi nyie nyumbu na mbumbumbu tuu.
 
Back
Top Bottom