Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Benki ya Dunia imesema ipo tayari kutoa mitaji, dhamana na usaidizi wowote ili kuhakikisha Sekta binafsi inakuwa kipaumbele hususani katika kuwasaidia Vijana wa Afrika kufikia ndoto zao na maono yao kwa kuwekeza kwenye Sekta ya nishati.
Akiongea wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati Jijini Dar es saaama leo January 28,2025, Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga, amesema “Sekta binafsi ni Wadau muhimu wanapaswa kuwekeza katika mazingira ambayo watajiamini katika uwekezaji wao, wanahitaji kuwekeza katika mazingira yenye uwajibikaji”
“Benki ya Dunia tupo tayari kutoa mitaji, dhamana na usaidizi wowote ule ili kuhakikisha Sekta binafsi inakuwa kipaumbele kwasababu pekee yenu hamuwezi kufanikiwa, tunatarajia kupata fedha kwa ajili ya kuwezesha kwa miaka mitano au sita ijayo, Benki ya Dunia itawekeza fedha nyingi, kama tutaweka Dola bilioni 100 katika miradi hii, fedha hizi zikiwekezwa katika jitihada hizi kuwasaidia Wananchi wa Afrika, Vijana katika kufikia ndoto zao na maono yao hiki ndicho kipaumbele kikubwa”
“Hiki ni kitovu cha mwelekeo wetu kuwekeza katika nishati na gesi asilia kama tulivyowekeza katika kilimo na afya, sekta hizi ni muhimu kama zikifungamanishwa na umeme”