Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Songea chakula cha kueleweka kinaanzia elfu 3. Bado wapo sahihi.
Hapana, kanuni ya kula..."Tunakula ili tuishi"😃, zingine mbwembwe. Ukienda alikozaliwa spika wa bunge huko mbeya tukuyu Rungwe...hiyo elfu 7 inabakia na chenji, maisha mazuri siku nzima unatumia chini ya elfu 5. 😄....kungekuwa na chuo kikuu wanafunzi wangefurahia sana maisha...bumu wangejenga na nyumba zao za kuishi🤣🤣
 
Hapo kwenye umasikini kupindikia ndo kidogo hapana uhalisia sana



Hivi mnajua 7,834 ni nyingi kutumia kwa siku kwa mtu mwenye umasikini kupindikia!?. Kwasabab ni 235,020 per month. Hebu niambie wangap wanafanya kazi wanalipwa hela hiyo?..je ni masikini wa kupindikia?.



Pia 7,834 ni hela ya kawaida kwa mtu mmoja kutumia kwa siku kwa nchi yetu. Si hela ndogo sana kutumia mtu mmoja kwa siku...chakula hichi cha 2,000 au 3,000 kwa mama ntilie!...inatosha kabisa mbona
 
Sato mmoja wa kutosha familia ya watu watano kwa mlo mmoja tu ni sh 30,000, Nyama kilo ni tsh 10,000, yai moja ni sh 400. Haujaweka nishati, afya, usafiri, kodi n.k
Kwani kila siku wewe unakula sato au nyama? Hizi takwimu haifai kuzipigia kwa kuangalia matumizi ya juu kabisa!
 
Waongo hawa jamaa! Hicho kiwango waseme kinatagemea na context ya nchi husika! Sehemu nyingi kwa Tanzania elfu 7 unakula na chenji inabaki!
 
Waongo hawa jamaa! Hicho kiwango waseme kinatagemea na context ya nchi husika! Sehemu nyingi kwa Tanzania elfu 7 unakula na chenji inabaki!
Hiyo elfu 7 sio kula tu, ni wastani gharama zako zote za kuishi mtu masikini kwa siku.
 
Wasitupangie maisha. Tumeshazoea ugali na mlenda
 
umaskini uko mwingi sana hapa kwetu!
Asubuhi 1k mchana buku ugali na mboga zake usiku mihogo ya jero
 
Jero haitumi kwa airtel money mkuu.
Tupambane tu kwa kweli maana sote ni mafukara😅😅
kuna sehem nina kibubu kwaio naichokonoa hadi ianguke,,sema nimeshaitumia kununua u-fresh😌😌
 
Je wewe uko katika kundi hili? Je ni Watanzania wangapi wapo katika kundi hili?
 
Ila iyo konyagi ni 135,000 Kwa mwezi mkuu😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…