Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Hizi ni fiction, nilifikiri hiko kijiji kweli kipo, uliharibu uliposema wanalima pamba🤣, vijiji vinavyolima mazao ya biashara pure barter trade walishaachana nayo kabisa. Labda ungesema hicho kijiji wanalima hata uwele na ulezi.
Kijiji kipo na pamba hawalimi wote kijijini ni mtu mmoja mmoja na kwa sasa sidhani kama yupo tena.

Hoyo zamani tulilima pamba nikiwa primary, miaka mingi nimetoka huko.

It is real, not a fiction, kama unavyotaka iwe. Na sitasema ni wapi ndio maana ya hizi ID fake.
 
Of course hakuna mahali utakuta kijiji kizima watu wote wanalima Pamba, chai, kahawa, tumbaku, sio kwa mazao haya pure kwa biashara, labda ingekuwa mahindi, maharage n.k
 
Benki ya Dunia (WB) imetangaza marekebisho ya kiwango cha kimataifa cha umaskini, ikipandisha kiwango cha chini kutoka Dola 2.15 za Marekani kwa siku (sawa na TSh 5,614) hadi Dola 3.00 (TSh 7,834) kwa siku.

View attachment 3396592
Kwa muktadha huo, mtu yeyote anayeishi kwa kutumia kiasi cha chini ya TSh 7,834 kwa siku sasa atahesabika kuwa anaishi katika umasikini uliokithiri, kulingana na viwango vipya vya kimataifa vilivyotangazwa Juni 2025.

Marekebisho haya yamefuatia kutolewa kwa takwimu mpya za uwezo wa kununua (PPP) Mei 2024, kupitia Mpango wa Ulinganifu wa Kimataifa (ICP), ambao hulinganisha bei za bidhaa na huduma kati ya nchi tofauti ili kuweka kipimo cha bei kinachowiana kwa nchi zote duniani.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mabadiliko haya yamelenga kuendana na mabadiliko ya viwango vya bei duniani na kutoa picha halisi zaidi ya kiwango cha chini cha maisha, hasa katika nchi za kipato cha chini.

PPP mpya zilizotolewa mwaka 2024 zilitokana na ukusanyaji wa data za mwaka 2021, bei za bidhaa za msingi kama chakula, mavazi na makazi zilionesha kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Viwango vipya vya PPP hutumiwa kubadili sarafu mbalimbali kuwa katika kipimo kimoja cha kulinganisha, hivyo kurahisisha tathmini ya hali ya umaskini duniani.

Tangu kutambulishwa kwa kipimo cha 'dola moja kwa siku' mwaka 1990, Benki ya Dunia imekuwa ikihuisha kiwango hiki mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya hali ya kiuchumi na kijamii duniani.
Kama kweli ccm wako serious hili ndo eneo walitakiwa kulifanyia kazi kwa nguvu za kike na za kiume
 
Of course hakuna mahali utakuta kijiji kizima watu wote wanalima Pamba, chai, kahawa, tumbaku, sio kwa mazao haya pure kwa biashara, labda ingekuwa mahindi, maharage n.k
Pale kijijini hata sijui siku hizi panalimwa nini labda viazi, maana wanalia mvua hazinyeeshi kila mwaka , na wanadai mazao hufia mashambani misimu imebadirika.

Njaa kila siku ndio kilo chao.
 
Pale kijijini hata sijui siku hizi panalimwa nini labda viazi, maana wanalia mvua hazinyeeshi kila mwaka , na wanadai mazao hufia mashambani misimu imebadirika.

Njaa kila siku ndio kilo chao.
Hiyo ndio tafsiri halisi ya chini ya $3 kwa siku. Sasa nimekuelewa uliposema hizo $3 mbona kuna watu hawazioni🤣.
 
Tangu kutambulishwa kwa kipimo cha 'dola moja kwa siku' mwaka 1990, Benki ya Dunia imekuwa ikihuisha kiwango hiki mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya hali ya kiuchumi na kijamii duniani.
kumbe na MIMI ni fukara wa kutupwa? duh ngoja nijitahidi
 
Hizi ni hujuma za mabeberu kwa mama
Mama gani? Rais mnamwitaje mama? Rais ni rais tu. Ndio maana anafanya mengine ya kimama, nyie ndio chanzo. Tumuite rais na tuache kumdogosha. Tukimdogosha, atajidogosha na tutalalamika.
 
Wazungu ni wapumbavu wakati mwingine! Bora hiyo dolar 3 wangekuwa wanasema kwa household. Hivi inawezekana vipo kwenye familia mpo watu watano na watoto ndani yake muwe na matumizi yanayolingana? Yaani dola 3 x 5 = dola 15! Hakuna familia ya kawaida inayoweza kumaliza dola 15 kwa siku!
 
Inawezekana kupima nackuwa na kipimo cha wastani wa kipato na umaskini wa jamii YOYOTE au kundi LOLOTE la watu hata kama kuna gharama tofauti za mahitaji ya watu. Mjini kunahitaji nguvu na pesa, kijijini pia kunahitaji nguvu na pesa au barter trade. Watu wengi wa mjini wanategemewa na wanatuma pesa vijijini kwa wazazi na ndugu zao.
Kwahio hapo ushamuongezea mbangaizaji wa Mjini hata kama anapata 50K kwa siku gharama ya kutunza extended family ambayo katika equation yangu unazidi kumuongezea matumizi. Na zile nyanya na maharage mtu wa kijijini anazopata shambani huyu huku ananunua sababu hata akitaka hawezi kuwa na shamba ghetto (ambalo huenda anadaiwa miezi mitatu kwa kujaribu to make ends meet)...; Hence unaweza kupima kundi la watu wa sehemu fulani wenye mazingira sawa na sio kundi la watu tofauti wenye mazingira tofauti (Jibu haliwezi likawa moja); Na kwa kulifahamu hilo kwamba issue ipo kwenye gharama ya matumizi ndio maana kuna siku nilisema...

Wazungu ni wapumbavu wakati mwingine! Bora hiyo dolar 3 wangekuwa wanasema kwa household. Hivi inawezekana vipo kwenye familia mpo watu watano na watoto ndani yake muwe na matumizi yanayolingana? Yaani dola 3 x 5 = dola 15! Hakuna familia ya kawaida inayoweza kumaliza dola 15 kwa siku!
Sato mmoja wa kutosha familia ya watu watano kwa mlo mmoja tu ni sh 30,000, Nyama kilo ni tsh 10,000, yai moja ni sh 400. Haujaweka nishati, afya, usafiri, kodi n.k
 
Kwahio hapo ushamuongezea mbangaizaji wa Mjini hata kama anapata 50K kwa siku gharama ya kutunza extended family ambayo katika equation yangu unazidi kumuongezea matumizi. Na zile nyanya na maharage mtu wa kijijini anazopata shambani huyu huku ananunua sababu hata akitaka hawezi kuwa na shamba ghetto (ambalo huenda anadaiwa miezi mitatu kwa kujaribu to make ends meet)...; Hence unaweza kupima kundi la watu wa sehemu fulani wenye mazingira sawa na sio kundi la watu tofauti wenye mazingira tofauti (Jibu haliwezi likawa moja); Na kwa kulifahamu hilo kwamba issue ipo kwenye gharama ya matumizi ndio maana kuna siku nilisema...

Ni kitu gani usichoelewa kuhusu wastani au average?? Kwa hiyo wewe unavyoelewa mtu mwenye watoto, housegirl na huyo tegemezi huko kijijini gharama zote anabebeshwa yeye anayehudimia ndio inapatikana hiyo $3 kwa siku??
 
Kuna sehemu zingine hapa Tanzania mtu anayetumia elfu saba kwa siku siyo masikini hata kidogo. Kwa mfano familia ya watu sita inayotumia elfu 42 kwa siku utasema ni masikini kupindukia?
 
Ni kitu gani usichoelewa kuhusu wastani au average?? Kwa hiyo wewe unavyoelewa mtu mwenye watoto, housegirl na huyo tegemezi huko kijijini gharama zote anabebeshwa yeye anayehudimia ndio inapatikana hiyo $3 kwa siku??
Aisee kweli kuna tatizo mahali kubwa sana ngoja nijaribu kuwa basic...,

Moja gharama ya mlo anaokula mtu wa masaki ni sawa na mtu wa Gamboshi ? Hio moja pili hivi unasahau unachoandika kila ukiweka nukta ?, Sio wewe uliyesema huyu mtu wa town ndio anamtumia mtu wa kijijini pesa za matumizi ? Na mimi nikasema kwahio huyu wa town hata akipewa 50K kwa siku bado atakuwa ni masikini wa kutupwa sababu kila anachopata hakitoshi....

Kumbuka mtiririko wote huu umekuja baada ya mimi kuchukua mifano hai ya Mbangaizaji wa Dar na average Joe kijijini; with everything being equal katika yale mahitaji muhimu (chakula, malazi na mavazi) nani ni fukara ingawa wa Mbangaizaji wa Dar anapata hata 20k kwa siku na Average Joe hana hata wallet na simu yake haijawahi kusoma hata 30k at any given time.
 
Life sio fair, tutafute hela jamani, matumimizi chini ya shillingi 7438 ni maskini kupindukia, tujiondoe kwenye kundi hili

IMG-20250707-WA0000.jpg

IMG-20250707-WA0001.jpg
 
Na hata hivyo kuna ukweli just imagine chai chakula cha mchana na usiku hapo hujaweka mafuta ya kupika na usafiri

Binafsi nawaunga mkono hoja
 
Kwahiyo unataka kuniambia hiyo average waliipata bila kuhusisha matumizi ya fedha ya mkopo?,amini usiamini debt inachukua sehemu kubwa zaidi kwenye matumizi kuliko cash
Debt si inalipwa? Hakuna MTU anayeweza kuishi kwa kutumia mkopo muda wote,
 
Hela inatafutwa kivipi fafanua,

Binafsi nauchukia Sana huu mtindo wa kusema tafuta pesa.

Duniani nzima nature iko hivyo hatuwezi kuwa matajiri wote
 
Back
Top Bottom