Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Hayo yote nimesema hapo juu, chumvi wanabadirishana yani butter trade, yale mjini mnaita makopa kule tunaita udaga kwa chumvi, nguo na matandio na mengineyo ni kwa kuuza mazao hayo kama udaga, mtama mahindi au usubiri msimu wa pamba.

Ni hii ni kweli siyo story, nimeona kwa macho yangu.

Mahitaji makubwa watauza Ng'ombe au mbuzi kama wapo.

Vigezo vyao huwa standard inayo fit wote.
World Bank inajua wapo Wahadzabe pia, Khoisan, Basarawa, raia wa misituni DRC n.k hao wote wamezingatiwa kupata huo "wastani".
 
Benki ya Dunia (WB) imetangaza marekebisho ya kiwango cha kimataifa cha umaskini, ikipandisha kiwango cha chini kutoka Dola 2.15 za Marekani kwa siku (sawa na TSh 5,614) hadi Dola 3.00 (TSh 7,834) kwa siku.

View attachment 3396592
Kwa muktadha huo, mtu yeyote anayeishi kwa kutumia kiasi cha chini ya TSh 7,834 kwa siku sasa atahesabika kuwa anaishi katika umasikini uliokithiri, kulingana na viwango vipya vya kimataifa vilivyotangazwa Juni 2025.

Marekebisho haya yamefuatia kutolewa kwa takwimu mpya za uwezo wa kununua (PPP) Mei 2024, kupitia Mpango wa Ulinganifu wa Kimataifa (ICP), ambao hulinganisha bei za bidhaa na huduma kati ya nchi tofauti ili kuweka kipimo cha bei kinachowiana kwa nchi zote duniani.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mabadiliko haya yamelenga kuendana na mabadiliko ya viwango vya bei duniani na kutoa picha halisi zaidi ya kiwango cha chini cha maisha, hasa katika nchi za kipato cha chini.

PPP mpya zilizotolewa mwaka 2024 zilitokana na ukusanyaji wa data za mwaka 2021, bei za bidhaa za msingi kama chakula, mavazi na makazi zilionesha kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Viwango vipya vya PPP hutumiwa kubadili sarafu mbalimbali kuwa katika kipimo kimoja cha kulinganisha, hivyo kurahisisha tathmini ya hali ya umaskini duniani.

Tangu kutambulishwa kwa kipimo cha 'dola moja kwa siku' mwaka 1990, Benki ya Dunia imekuwa ikihuisha kiwango hiki mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya hali ya kiuchumi na kijamii duniani.
Watakuwa USA na Umoja wa Ulaya hao.Sisi huku uchumi wetu upo juu na tunawazidi mbali sana.Vipi,wanataka tuwaidhinishie misaada? They don't have to worry much,Watapata.
 
Kuna watu hata hiyo dollar 1 kwa siku hawaipati, na wanaishi sijui hao wao wako kundi gani.

Nilikotoka mimi watu wanalima kutwa, wanakula ugali na mboga za majani hakuna shughuli zozote za kibiashara.

Mtu akiumwa upewa tiba za kienyeji, wamama hujifungulia majumbani na sikuwahi kusikia vifo vya mama na mtoto.

Hakuna umeme, wala maji ya bomba.

Maji tunategemea mto, visima na ziwa.

Lakini ni wafugaji na wanafuraha sana na maisha yao.

Biashara yao ni kubadirishana, chumvi kwa mahindi.

Msimu wa pamba ndio watu hununua baiskeli, nguo, viatu, matandiko na mahitaji megine.

Hawa wako kundi gani la umasikini au ndio wameshakufa kabisa hawa?
Ukiona binadamu anaishi maisha hayo halafu unasema anafuraha huyo ni mjinga anaesubiri kufa na sio kuenjoy dunia Hana tofauti na nyani maana nyani nao huwa wanafuraha sana
 
World Bank inajua wapo Wahadzabe pia, Khoisan, Basarawa, raia wa misituni DRC n.k hao wote wamezingatiwa kupata huo "wastani".
Mbona hatuzioni huku au wanazipiga juu kwa juu?
 
Kwani wao ni akina nani mpk wapange,acha kusikiliza vitu vya kipiizi
 
Sasa hawa watu wanaosema wanasurvive kwa elfu 7 and below wanaishije, bado nawaza...ndio maana nikasema kwenye mchango wangu labda ni hawa young ages ambayo hawana majukumu and they don't pay bills.
Ata kwa hao young ages...anaangaliwa 'bread winner' tu
 
Yoda Inafikirisha kwa kweli, nimeshangaa baadhi ya wachangiaji humu wakisema wanaweza kusurvive kwa $3 and below like how?? Nikwamba living cost ya Tz ndio imekuwa chini hivyo, paying gas, Internet, transport meals and drinks na bado mambo kibao.
Hiyo $3 ni thamani ya mahitaji muhimu ya binadamu kwa siku, sio lazima iwe cash.
Halafu uko unakotoka watu hawasafiri kabisa ? hawanunui nguo ? Mahindi wanasagia kwenye mawe? watoto hawaendi shule? Watu hawanuni sukari, chumvi, ngano, sabuni, viberiti, mafuta, vitunguu, nyanya, mchele, matunda??
 
Huwezi ukaweka a blanket figure wakati matumizi yanatofauti kubwa sana.., UK ka apartment mtu unakaa kama njiwa na bila pesa ya kununua gesi unaganda kwa baridi inawezekana hata ukilipwa dollar 400 kwa wiki huenda ukawa ni masikini wa kutupwa; wakati mmasai ambaye housing its cheaper to free (na kuna sehemu hata nyumba ni tupu) na akitaka chakula akienda gengeni mlo mmoja wa mchana wa mtu wa UK yeye anaweza akala mwezi mzima....

Hence huwezi ukatumia matumizi ya kiasi fulani cha pesa kuonyesha fulani kama ni masikini au hapana....; Hususan hakuna sehemu watu wanaishi sustainably kama vijijini na wanapata all their basic needs na kuishi a fulfilling life
$3 kwa siku ni kwa nchi masiki, kwa nchi za kipato cha kati ni $6.85, nchi tajiri hiko kipimo hakiwahusu.
 
Benki ya Dunia (WB) imetangaza marekebisho ya kiwango cha kimataifa cha umaskini, ikipandisha kiwango cha chini kutoka Dola 2.15 za Marekani kwa siku (sawa na TSh 5,614) hadi Dola 3.00 (TSh 7,834) kwa siku.

View attachment 3396592
Kwa muktadha huo, mtu yeyote anayeishi kwa kutumia kiasi cha chini ya TSh 7,834 kwa siku sasa atahesabika kuwa anaishi katika umasikini uliokithiri, kulingana na viwango vipya vya kimataifa vilivyotangazwa Juni 2025.

Marekebisho haya yamefuatia kutolewa kwa takwimu mpya za uwezo wa kununua (PPP) Mei 2024, kupitia Mpango wa Ulinganifu wa Kimataifa (ICP), ambao hulinganisha bei za bidhaa na huduma kati ya nchi tofauti ili kuweka kipimo cha bei kinachowiana kwa nchi zote duniani.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mabadiliko haya yamelenga kuendana na mabadiliko ya viwango vya bei duniani na kutoa picha halisi zaidi ya kiwango cha chini cha maisha, hasa katika nchi za kipato cha chini.

PPP mpya zilizotolewa mwaka 2024 zilitokana na ukusanyaji wa data za mwaka 2021, bei za bidhaa za msingi kama chakula, mavazi na makazi zilionesha kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Viwango vipya vya PPP hutumiwa kubadili sarafu mbalimbali kuwa katika kipimo kimoja cha kulinganisha, hivyo kurahisisha tathmini ya hali ya umaskini duniani.

Tangu kutambulishwa kwa kipimo cha 'dola moja kwa siku' mwaka 1990, Benki ya Dunia imekuwa ikihuisha kiwango hiki mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya hali ya kiuchumi na kijamii duniani.
Nashukuru nimeepuka kikombe cha ufukara huo.
 
hapana, mbona tanzania imepiga maendeleo kuliko marekani? bimkubwa kasema.
 
Yoda Inafikirisha kwa kweli, nimeshangaa baadhi ya wachangiaji humu wakisema wanaweza kusurvive kwa $3 and below like how?? Nikwamba living cost ya Tz ndio imekuwa chini hivyo, paying gas, Internet, transport meals and drinks na bado mambo kibao.
Kuna waongo na wengine hawaelewi hiyo $3 inamaanisha nini, mfano huko vijijini boda zimejaa ndio usafiri mkubwa sehemu nyingi na watu wanalipa hadi buku 3 kwa tripu moja, wananunua mafuta ya taa kila siku n.k
 
Yani huyo Akuamkie jamni eela ngumu sana na ukiishika ni shwaa sijaamin jana nimejifanya kupika pilau kilakitu kipo ni nyama na viungo Elf 9 shwaa nikasema nn nikaanza kisearch chenji ufukara tabu sana 😂😂😂
Naona hutaki effective utilisation of resource (money) 🤣🤣🤣
 
Natumia zaidi lakin inategemea na siku na vyakula vipo ndani kunasiku sifikii. Hiyo mfano nikiamua nisinunue vitu nje au mgahan nilliko ugali buku 😀 tunazungumzia kula Tu lakin
Unajua life sometime linatufanya sisi tunajiona smart 🤣 kwani kusomba vitu vya ndani ndo umekwepa matumizi ni umepunguza ruti za rejareja ila tabu iko pale pale on every month tena matumizi ni zaidi mama chanja kodi ya kichwa ibaki mezani hata kama stoo imejaa 😄
 
Really? Interesting! Una familia? Unafanyaje fanyaje, ebu tupe experience yako kama hutojali.
Ndio nina familia, vile nafanya kwa kweli ndio mshangao wenyewe, ila formula yangu kubwa ni two in one kwenye mlo wa siku, na wakati mwingine two in three.
 
$3 kwa siku ni kwa nchi masiki, kwa nchi za kipato cha kati ni $6.85, nchi tajiri hiko kipimo hakiwahusu.
Chukulia Tanzania, na mdau ambaye ni above average tuseme anapata 20k kwa siku akienda kupiga issue zake za u day worker...; huyu jamaa nikiweka usafiri kwenda na kurudi, nikiweka maji ya kunywa hata kama akipiga ndefu mchana na tuseme hata nyumba huko anakopanga tuseme anamzingua mwenye nyumba na ni mtu wa kukimbia na madeni (hapo nikiweka bili ya maji na umeme) tunaongelea mtu ambaye anakopa mwezi ujao ili alipe madeni ya mwezi uliopita (in short yupo kwenye absolute poverty na kipato chake cha 20k kwa siku)

Chukulia average Joe mmoja yupo huko Bush, yeye mitikasi yake hata kwa miguu anatembea maji anaweza kunywa hata ya mtoni au ya mvua amekinga (after all sewage system haijachafuliwa kama ya mjini ambapo typhoid ni nje nje) huyu mtu hata akilipa luku ni Tshs 100 per unit (tariff zero) kupika anaweza kutumia kuni, starehe zake ni ngoma na kukutana nawadau kijiweni; mjomba wake akimtumia hata 10k huenda ikamaliza miezi mitatu kwa kununua local brew....

Kwa mfano wa hao wawili wa pili anaishi a fulfilling happier sustainable life without stress ingawa hata wallet hana na mpesa yake haijawahi kusoma zaidi ya 30k at any given time....

i.e. "Each case must be considered on its own merits"
 
Huyo average Joe mmoja wa huko Bush yeye chakula anakitoa wapi? Au anaishi kwa kula matunda pori na wanyamapori wa serikali?? Haumwi na akiumwa hatibiwi hospitali? Hanywi pombe wala kufanya mapenzi? Wastani wa miaka ya kuishi ya average Joe ni miaka mingapi??
 
Back
Top Bottom