Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Benki ya Dunia: Wanaotumia chini ya Tsh. 7,834 kwa siku ni maskini kupindukia

Hujadadavua vizuri sababu unaweza kua kwenye mazingira ambayo vyakula vingi unavuna shambani au kama upo mjini unakuta unayo akiba ya vitu vingi ndani.

Hii hesabu imepigwa kwa ujumla wa mahitaji ya mtu mmoja kwa siku
Natumia zaidi lakin inategemea na siku na vyakula vipo ndani kunasiku sifikii. Hiyo mfano nikiamua nisinunue vitu nje au mgahan nilliko ugali buku 😀 tunazungumzia kula Tu lakin
 
Wafanyakazi wa viwandani hapo dar wanalipwa shingapi kwa siku
Mimi sipo dar mkuu, sijawahi kufanya kazi ya kiwanda na wala sijui wanalipwa pesa ngapi labda wajuvi wa mambo watakusaidia.
 
Haya mambo ya kutokuangalia sehemu husika ni upuuzi (Monaco hata ukiwa na uwezo wa kutumia 100usd kwa siku bado ni masikini wa kutupwa)..,. It's about income ya ku sustain maisha yako na kubakia na disposable ya mambo mengine...; Hii ndio ilinikumbusha article moja ya Wakenya wanasema wananyonywa kwa kulipa USD 2 USD kwa saa...

 
Benki ya Dunia (WB) imetangaza marekebisho ya kiwango cha kimataifa cha umaskini, ikipandisha kiwango cha chini kutoka Dola 2.15 za Marekani kwa siku (sawa na TSh 5,614) hadi Dola 3.00 (TSh 7,834) kwa siku.

View attachment 3396592
Kwa muktadha huo, mtu yeyote anayeishi kwa kutumia kiasi cha chini ya TSh 7,834 kwa siku sasa atahesabika kuwa anaishi katika umasikini uliokithiri, kulingana na viwango vipya vya kimataifa vilivyotangazwa Juni 2025.

Marekebisho haya yamefuatia kutolewa kwa takwimu mpya za uwezo wa kununua (PPP) Mei 2024, kupitia Mpango wa Ulinganifu wa Kimataifa (ICP), ambao hulinganisha bei za bidhaa na huduma kati ya nchi tofauti ili kuweka kipimo cha bei kinachowiana kwa nchi zote duniani.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mabadiliko haya yamelenga kuendana na mabadiliko ya viwango vya bei duniani na kutoa picha halisi zaidi ya kiwango cha chini cha maisha, hasa katika nchi za kipato cha chini.

PPP mpya zilizotolewa mwaka 2024 zilitokana na ukusanyaji wa data za mwaka 2021, bei za bidhaa za msingi kama chakula, mavazi na makazi zilionesha kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Viwango vipya vya PPP hutumiwa kubadili sarafu mbalimbali kuwa katika kipimo kimoja cha kulinganisha, hivyo kurahisisha tathmini ya hali ya umaskini duniani.

Tangu kutambulishwa kwa kipimo cha 'dola moja kwa siku' mwaka 1990, Benki ya Dunia imekuwa ikihuisha kiwango hiki mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya hali ya kiuchumi na kijamii duniani.
Kwa Sisi watumishi wa serikali especially wa halmashauri assurance ni kwamba 95% wanaishi kwenye dimbwi la umasikini
 
Inatosha na chenchi inabaki, umewahi kusikia supu ya ngozi au bia za kupima
Nimepata kuona pombe Kali za kupima kama shots za koniagi na kvant/valeur ila bia za kupima hapana mkuu, hii supu ya ngozi ndio makongoro?
 
Hahaha hakika maisha ya watanzania wengi ni vitendawili, leo pangu pakavu kesho tumbo juu kwa kuvimbilwa huku wakinyoosha mikono "Mitano tena" alafu baada ya hapo yanabaki manung'uniko tu😀😀
Usijari laaziz Aaliyyah Mwenye enzi atajaalia na mengine yatabaki historia.
😂😂😂😂nna mambo mengi. Alafu age go yani kunavit nikivimaliza nitarelax yani nitafanya na kasherehe now acha tu niwe fukara mahesabu ni muhimu sana
 
Mostly 7000 per day
With meals inclusion au wanajitegemea? Nadhani pia watakuwa hawaishi mbali na viwanda husika kwa maana ya kusave pesa ya transport and I guess mostly of them are young girls and boys ambayo hawana majukumu pia.
 
Sidhani kama ni kula tu ..
Chakula
Umeme
Maji
Transport
Mengineyo (10% ya mahitaji)
Nadhani ni kama mtu akuambie naomba budget yako ya siku, huwez kutaja msosi tu
 
With meals inclusion au wanajitegemea? Nadhani pia watakuwa hawaishi mbali na viwanda husika and mostly are young girls and boys ambayo hawana majukumu pia.
Watu wazima na familia zao
 
Hawa wa chini ya $3 wako wangapi Tanzania ? ChoiceVariable
Kuna watu hata hiyo dollar 1 kwa siku hawaipati, na wanaishi sijui hao wao wako kundi gani.

Nilikotoka mimi watu wanalima kutwa, wanakula ugali na mboga za majani hakuna shughuli zozote za kibiashara.

Mtu akiumwa upewa tiba za kienyeji, wamama hujifungulia majumbani na sikuwahi kusikia vifo vya mama na mtoto.

Hakuna umeme, wala maji ya bomba.

Maji tunategemea mto, visima na ziwa.

Lakini ni wafugaji na wanafuraha sana na maisha yao.

Biashara yao ni kubadirishana, chumvi kwa mahindi.

Msimu wa pamba ndio watu hununua baiskeli, nguo, viatu, matandiko na mahitaji megine.

Hawa wako kundi gani la umasikini au ndio wameshakufa kabisa hawa?
 
Acha watu waishi bhana ,hizo Takwimu zenu hazina uhalisia..Mtu kazaliwa maskini na ataiufa hivyo hivyo ...Maisha yaendele
 
Nimepata kuona pombe Kali za kupima kama shots za koniagi na kvant/valeur ila bia za kupima hapana mkuu, hii supu ya ngozi ndio makongoro?
Tembea uone ni Tanzania hii haya mambo yapo, watu wanakula ngozi sio kongoro na bia zinapimwa kwa glass hiki sio kichekesho au kumdharau mtu ila ndio ukweli wa maisha.
 
Natumia zaidi lakin inategemea na siku na vyakula vipo ndani kunasiku sifikii. Hiyo mfano nikiamua nisinunue vitu nje au mgahan nilliko ugali buku 😀 tunazungumzia kula Tu lakin
Inaonekana hisabati ya hili shirika haijakamilika... Ukadiriaji wao hawajajumlisha pombe na starehe zingine.

Kwa upande wako ni sawa kabisa ikiwa hunywi pombe, huhongi na huna chochoro nyingine ya kupoteza hela zako
 
Back
Top Bottom