Benki ya Dunia yachelewesha tena kuipa Tanzania mkopo wa Dola 500M

Tupo kwenye rait trakt..sisi ni dona kantri..mabeberu wanatuonea wivu..mana tunapaaa kama mwewe..tembeeni vifua mbele...bogaz kabisa.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora kuachana na huo mkopo.. Huwezi idhinisha umalaya kwa wanafunzi kisa dola milioni mia tano.
Kutunga sheria ya kuidhinisha umalaya kwa wanafunzi kutaharibu mabinti zetu wanaojitunza.
Bye bye WB.. U can keep your money.
Watu weusi tuna changamoto sana kwenye Dunia hii.

Hili swala halina tofauti na lile la ushoga, uwezo wetu ni kuhemuka tu badala ya kukaa chini na kutafakari.

Wanachowashauri Wenzenu hao a.k.a Mabeberu kama mnavyowaita ni msiendelee kuwaadhibu wale waliokwishaathirika..sasa mfanye nini wasifikie huko ni juu yenu..nchi ni yenu sio ya Mzungu.

Kama Mtoto ameshakuwa shoga tafuta ni nini chanzo pambana nacho, kama Mtoto ameshapata mimba tafuta ni nini chanzo pambana nacho na sio kutafuta shortcut kwa kuhangaika na Victims.

Kulalamika kwamba mnatakiwa muidhinishe umalaya, ni sawa na kuwajibu kwamba sisi hatuna akili zenye uwezo huo wa kuzuia.

Huyo Mzungu hana shida na taifa lako, nchi ni yenu na raia ni wa kwenu...kama mnaweza kuwa na taifa lisilo na mimba za Wanafunzi basi ni vema..sasa nini kifanyike wasipate mimba ndio tumieni akili zenu mlizoumbwa nazo.
 
Kwani baada ya kukosa pesa za MCC unaionaje mirafi ya REA. Kwetu REA. III ilikuwa ikamilike 2017 April. Leo hata alama za nguzo zilishaliwa na mchwa na hakuna kiongozi yeyote anathibutu kuzungumzia kilichotokea.
 
Tatizo serikali haioni ukubwa wa hili tatizo, imagine mtoto kapewa mimba...baba wa mtoto kafungwa miaka 30..mtoto wa kike kafukuzwa shule. Je ni nani atakaekuja kumsaidia huyu mtoto aliezaliwa.

Kumzuia mtt wa kike kusoma kwa sababu ya mimba kuna athari kubwa zaidi
 
Imegoma ai imechelewesha (delays) upigaji kura?

Ndiyo maana Mkapa huwa anawapakia nyie makanjanja.

Mkisema ukweli itakuwa nini?
Sasa mbona umepaniki bibie...

Soma hapa

"(CNN)The World Bank has postponed its decision on granting Tanzania a $500 million loan, following pressure from activists who oppose the country's policy of banning pregnant girls and young mothers from attending state school."
 
Mikopo Chefuchefu, Hao mabinti zenu kama wanajitunza hata umalaya ungeruhusiwa wangejitunza, hakuna mtu ataacha mambo yake akufundishie mtoto wako maadili, maadili yatoke kwako mzazi, mtoto akipata mimba isiwe ndo mwisho wa elimu, hapo hapana, akipata mimba tuweke taratibu maalumu ya adhabu (adhabu mbadala na iwe inaumiza somehow ikiwezekana hata wazazi walipe faini kubwa).

Hata kama itachukua 5 years ila adhabu ikiisha arudi shule , adhabu itasaidia sana mzazi Ku deal na mwanae, na mtoto ataogopa jinsi mzazi akilipishwa faini kubwa maana lazima kipigo kitamuhusu na mambo mengine yataharibika ndani ya familia. Lengo sio kuharibu familia, lengo ni kumfanya kila mzazi a-take responsibility kwa mtoto wake na pia isimnyime mtoto wakike elimu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafahamu maana ya neno" postponed"?
 
Hii yote ni dalili tosha kwamba sisi bado ni masikini sana pamoja na viongozi wetu kujimwambafai kwamba sisi ni matajiri. Kwa nini tunaendelea kuwabembeleza watupe mkopo kwa masharti ambayo kwetu hayakubaliki ????
 
Ni kweli kabisa, maana akienda shule za waliopo fresh sidhani kama atakubali achapwe viboko wakati naye ni mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…