Benki ya Dunia yaidhinisha Mkopo wa Shilingi Trilioni oni 1.8 kwa Tanzania kwa ajili ya Sekta ya Afya na kuimarisha Uchumi

Benki ya Dunia yaidhinisha Mkopo wa Shilingi Trilioni oni 1.8 kwa Tanzania kwa ajili ya Sekta ya Afya na kuimarisha Uchumi

Mimi hadi sasa kwa utendaji wa mhe. Rais Samia anafanya vizuri sana tatizo hulka yake inamponza mpole na anamuhali sana..

Mafisi yanamuonea sana
Upole sioinshu mbona mwinyi ni mpole lakin chek anavyo wanyoosha watendaj wanaozingua,ye kama hawez ampe meno wazilimkuu,shida anahofia ata mzid umaaruf ikawa kama ya kikwete na lowasa.
 
Mkopo wa Serikali Ni 73
Screenshot_20221214-115149.png
T na sio hiyo unayosema wewe 👇
 
Kukopa jambo moja na mchakato wa kupewa hizo pesa ni jambo lingine...

Ndelea kula mtori nyama utazikuta chini.
Mkuu unamaana gani?
mi najua tangazo likiwa bayana kama hivyo kimango kinakuwa tayali BOT
 
Mkuu unamaana gani?
mi najua tangazo likiwa bayana kama hivyo kimango kinakuwa tayali BOT
Nyingine ni ahadi tu..zinachukua muda
Ni kama wewe unashida umeenda kukopa kwa jamaa au rafiki anakwambia kesho nitakupa kesho tena atakwambia nilitegemea leo ila subiri kesho nitakuwa nimepata teyar..the same to national level
 
Salaam,
TAARIFA KWA UMMA

DODOMA, 22 Desemba, 2022 – BENKI ya Dunia imeiidhinishia Tanzania, mkopo wenye masharti nafuu pamoja na msaada vyote vikiwa na thamani ya dola za Marekani milioni 775 (Sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 1.8), kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa bajeti, kuboresha uchumi na huduma za afya.

Mchanganuo wa fedha hizo unaonesha kuwa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (IDA) litatoa mkopo wa dola za Marekani milioni 500 (sawa na shilingi trilioni 1.1) kwa ajili ya kufufua uchumi ulioathiriwa na UVIKO-19 na Vita vinavyoendelea baina ya Ukraine na Urusi, vilivyosababisha kusinyaa kwa shughuli za kiuchumi na kupanda kwa bei ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje yakiwemo mafuta na bidhaa nyingine.

Dola milioni 250 (sh. bilioni 581) zitatumika kwa ajili ya program ya afya ya mama na mtoto kwa njia ya kupima matokeo (PfoR) inayotekelezwa Tanzania Bara na dola za Marekani milioni 25 (sh. bilioni 58.1) zilizotolewa kama msaada na Mfuko wa Dunia wa kusaidia wanawake, vijana na watoto zitatumika kwa ajili ya mradi wa uwekezaji kiuchumi (IPF) kwa upande wa Zanzibar.

“Tumekubaliana na Benki ya Dunia kwamba fedha hizo ambazo zitaanza kuingia nchini kuanzia kesho (Ijumaa) zitaelekezwa katika kuiwezesha sekta binafsi kushiriki katika kukuza uchumi, kuziwezesha sekta za fedha kuwa na uwezo wa kukopesha sekta hiyo, kuimarisha uwazi na uwajibikaji Serikalini, kuboresha kilimo pamoja na kutatua changamoto za afya ya mama na mtoto” alisema Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania.

Benki ya Dunia imetoa fedha za msaada wa kibajeti baada ya kipindi cha miaka 8 ambapo mara ya mwisho Tanzania ilinufaika na mpango huo mwaka 2014, baada ya kuridhishwa na utekelezaji na usimamizi mzuri wa sera za kiuchumi na kifedha, uwazi na uwajibikaji, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania.

Katika Taarifa yake Benki ya Dunia, imeipongeza Tanzania kwa usimamizi makini wa uchumi wake licha ya kuwepo kwa athari hizo za UVIKO 19 na Vita ya Ukraine na Urusi, ambapo uchumi wake umeimarika na kupigiwa mfano na Taasisi hizo kubwa za Fedha Duniani, ikiwemo Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
IMG_20221222_152741_797.jpg

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Salum Mkuya, Jijini Washington D.C nchini Marekani wakati wa mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Hivi karibuni
(Picha na WFM)
 
Mkuu ulikuwa bwawa la Nyerere nini? Hii habari ishajadiliwa humu asubuhi na mapema.
 
Leteni hizo hela tunywee bia..watajiju watoto wenu na wajukuu zenu
 
𝙺𝚒𝚕𝚊 𝚠𝚒𝚔𝚒 𝚑𝚊𝚒𝚠𝚎𝚣𝚒 𝚔𝚞𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚙𝚊𝚜𝚒𝚙𝚘 𝚔𝚞𝚜𝚒𝚔𝚒𝚊 𝚖𝚒𝚔𝚘𝚙𝚘.
 
Alivyofariki JPM nlijua nchi itarudi nyuma sana, ila sikua nimejua ni kwa kiasi hiki. Kuna watu ni wabaya sana hapa Tanzania kuliko ibilisi mwenyewe. Lakini sina shaka kua soon tutamalizana na waovu.
 
Kwamba tuseme mkopo ni swala endelevu.... Anyway tuseme hii 1.8 trilln okn+ 91.01 trin, Ile ya nyuma inaweza kufika 100trin son as possible in 2023..,
Tukupe kwa strategic planning na siyo tunakopa kwenda kufanyia shopping ya sikuku za mwisho wa mwaka.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hazipiti wiki mbili hatujasikia Tanzania imekopa.
 
Kukopa ni chache ya maendeleo kwa nchi yenye viongozi wastaarabu, nchi yenye demokrasia na utawala bora. Kwa nchi ambayo rais wamefungwa midomo, hawana uwezo wa kuhoji kwa nini uchumi wa blue ugharimiwe na watanganyika, ni maumivu kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom