Benki ya Dunia yaisifu Tanzania kusimamia Uchumi kwa umahiri

Benki ya Dunia yaisifu Tanzania kusimamia Uchumi kwa umahiri

Truth must told, huu ndio ukweli halisi Tanzania inafanya vizuri sana achilia mbali na washenzi wezi wanaohujumu taifa hili, wezi kila mahali huwa hawakosekani, tuwadhibiti kwa vitendo ili taifa letu liwe mfano bora zaidi.

"Maendeleo ni ya watu na sio vitu!!" Hao world Bank wanaangaliaa ukuaji wa uchumi[ GDP growth rate] na kubainisha kuwa Taifa linafanya vizuri ili hali hawaangalii jinsi ya huo ukuaji unavyowanufaisha wananchi wake[ Distribution of national cake}!!
Maisha ya Watanzania waliowengi ni magumu sana Wakati huu wa mfumuko wa bei na uhaba wa ajira hivyo kuwasifia hawa walioko madarakani ni kuwahadaa wananchi!!
 
Kwahiyo wanajitoa ufaham kwamba hawajasikia aliyo yasema CAG ehh..🤔
Na leo Mb Mpina amesema kwamba kwa hesabu zake karibu trillions 30 zimeibiwa
 
"Maendeleo ni ya watu na sio vitu!!" Hao world Bank wanaangaliaa ukuaji wa uchumi[ GDP growth rate] na kubainisha kuwa Taifa linafanya vizuri ili hali hawaangalii jinsi ya huo ukuaji unavyowanufaisha wananchi wake[ Distribution of national cake}!!
Maisha ya Watanzania waliowengi ni magumu sana Wakati huu wa mfumuko wa bei na uhaba wa ajira hivyo kuwasifia hawa walioko madarakani ni kuwahadaa wananchi!!
Ndio wanaingaalia jinsi tunavyokopa mabilion ya dolla na kuja kuzitawanya huko nchini kwa kujenga vituo vya mafuta , kununua vx na baadae zinarudi tena kwao .
 
Hii Benki ya Dunia hovyo kabisa, kwa Sasa Kuna mfumko wa Bei kwa asilimia 200 na bado Serikali inasifiwa ?
 
Benki ya Dunia imeipongeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayopokea fedha kutoka kwa taasisi hiyo ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.

Lakini imeongeza kuwa Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano kwa usimamizi mahili wa masuala ya uchumi mpana, situ kwa nchi za Afrika Mashariki, bali kwa nchi za Afrika, ambapo kiwango cha ukuaji uchumi cha wastani wa asilimia 5.4 ni cha juu

Hii inathibitisha kuwa Tanzania ni salama na Rais Samia Suluhu Mama endelea kuupiga mwingi katika kukuza uchumi wa nchi na wananchi
 
Wameshajua kuwa serikali imepagawa na mchwa mpya unaovaa tai ?
 
Back
Top Bottom