Benki ya Dunia yatoa mikopo ya nyumba ya Sh50 bilioni

Benki ya Dunia yatoa mikopo ya nyumba ya Sh50 bilioni

Msukumo mwingine wa kuidhinisha mabilioni hayo,

Taarifa hiyo, inaeleza kwamba benki ya dunia, iliidhinisha fedha hizo, kwa sababu wakazi wengi katika maeneo ya mijini, wanakabiliwa na matatizo ya makazi.

Inaeleza kwamba watu wengi wana matatizo ya makazi kutokana na kasi kubwa ya ongezeko la watu mjini na kusababisha ujenzi wa makazi holela bila kufuata utaratibu kwenye maeneo ambayo hayajapimwa.
kha! kumbe ni mradi wa watu wa mijini?maskini sijui babu na bibi yangu kule kijijini sijui watakumbukwa lini?
 
kha! kumbe ni mradi wa watu wa mijini?maskini sijui babu na bibi yangu kule kijijini sijui watakumbukwa lini?

Kha! yaani unategemea wazee wa kijijini wakumbukwe na hii serikali si kichekesho hicho.Hii serikali iko kwa ajili ya faida ya watu wachache ambao ni viongozi ndani ya Chama Tawala na Serikalini.Bila kufanya mabadiliko ya mfumo uliopo hali hii italiangamiza Taifa.

Kuna msemo usemao mwenye macho haambiwi tazama.Hapa tulipofika kama taifa kuna kila chembe chembe ya machafuko kama hali ya sasa haitabadilika.Je tutakimbilia wapi?
 
Ndio hicho mie nachokiogopa maana watu wakichoka ubinaadamu huondoka na mwanadamu huwa mnyama. Rwanda iliendelea hii hali ghafla bin vu mauaji ya halaiki, senegal pia, sudan pia ubadhirifu wa rasilimu unaofanya na waarabu against wazawa wa eneo hilo. Kiufupi ni kwamba miradi kama iendeleze nchi na sio kuwa inabomboa nchi.
 
52bn ni pesa kidogo sana kwa ajili ya ujenzi wa makaazi mapya, kama zitagawanywa kwa mikoa 25 ya Tanzania, kila mkoa utapata 2.08bn. Kama nyumba moja ya gharama nafuu itagharimu 50mn fedha hizo zitajenga nyumba 42 kwa kila mkoa.

Tatizo la nyumba katika Tanzania ni kubwa kutokana na Serikali kuzidiwa na kazi ya kupima viwanja vipya pamoja na gharama kubwa za ujenzi ambazo zinapanda kila siku.

Serikali ingerudisha Benki ya Nyumba na hizo fedha zingeingizwa kwenye mfumo huo wa kibenki ili kila anayeweza apewe mkopo na kuwekewa riba nafuu. Hivi sasa baadhi ya Taasisi za kiserikali zina mipango ya kuwakopesha fedha waajiriwa kwa ujenzi wa nyumba kitu ambacho wale walio katika ajira za makampuni binafsi hawapati fursa kama hiyo.

Taasisi kama BEnki ya nyumba ingeweza kuwanufaisha waajiriwa wa Serikali na wale wa Binafsi.
 
Back
Top Bottom