Benki ya NMB yaja na huduma ya mkopo ya "NMB Salary Advance" kwa wafanyakazi

Kuvuka kwako nje ya Afrika,haiwezi kuwa sababu ya wewe kuwa unajua zaidi.Mazingira yetu hapa ni tofauti sana.
Benki hiyo hiyo,inayotoa mkopo wa milioni 7 na unakatwa jumla ya milioni 12,Hujailalamikia namna hii japo ilianza zamani!Zipo taasisi kama bayport unachukua 1.5M unakatwa jumla 4.5M!..hujawahi kuwalalamikia,Leo unakuja kulia na 6% ya salary advance kweli?Mbona unaonekana kama mchawi una wawangia watumishi wasipewe hiyo?
Mtaani kuna wafanyabiashara wanakopesha kwa riba ya 30% na bado watumishi wanachukua na wakati mwingine wanashindwa kuzilipa na wanalipa ile riba ili aendelee kujikopesha na kulipa riba mbili hadi 3!Ni ajabu sana wewe uliyetoka eti nje ya Afrika unakuja kuzungumzia vitu vya ndotoni visivyotekelezeka na unaamini kuwa ni halisi!!!
 
One months interest free overdraft ndio haitekelezeki? Wewe kaa tu Ugogoni uhangaike kutafuta maji ya kutawaza lemutuz!
 
Nani aliyefanikiwa kuitumia huduma hii wakuu?
 
Huduma nasiki inazingua nimekuta watumishi wanalalamik Kuwa hamna kitu wanajaribu na kujaribu
 
haizingui hata kidogo! Ukishaomba angalia salio usisubiri msg. Nilikua natest nikajikuta napata deni bila kutegemea
 
Kwan unalazimishwa kukopa au ndo shida zetu zinatufanya Tuende
 
Mshahara anaolipwa mtumishi package yake huwa haihusishi kusaidia wazazi,ndugu,michango ya harusi ,zawadi,nyumba ndogo nk.
Tutathmini matumizi yetu ,sina maana kuwa mengi ni ya anasa hapana tunazidiwa sana maana mengi huwa sio ya kwetu kama watumishi,matumizi mengi hutokana na mtu mmoja tu kiwa na ajira ya uhakika katika familia kubwa.Tuondokane na kuwategemea ndugu zetu walioajiriwa ili wasiiichukie serikali yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…