Mwandishi kawasilisha anachokiamini, lakini binafsi niliyaona makosa ya wacjezaji 2. Beno na Gadiel. Mchaezaji aloyechemka zaidi ni Gadiel maana hakufikiria kabisa anakokwenda anakwenda kuwa nani? Matokeo yake kaacha nyumba yake kaenda kupanga. Beno ni miongoni mwa vipaji halisi vya kitanzania, Lakini ameua kipaji kwa kukosea kuchagua. Najua wazi na nilimsema kocha aliyekuwepo kwamba anakosa sifa moja kubwa ya kuwa "Mlezi", akamkataa mchezaji kwa kosa la kudai haki yake hata kama hakutumia njia sahihi za kistaarabu. Hata hivyo alichokifanya mchezaji ilikuwa kama kuunga juhudi ushabiki wa Simba na Yanga, akakubali kutumika kama chombo cha siasa za mpira. Hakujali yeye atakuwa nani Simba, akakubali kuwa mke wa pili. Tuwapende wachezaji wetu lakini wanapokosea tuwaambie ukweli. Leo De Gea anaweza kwenda Liverpool kuwa msaidizi wa Allison? Hatuoni wenzetu hata nafasi yake uwanjani inaweza kuwa sehemu ya mkataba wake.