Beno Kakolanya asaini mkataba wa miaka miwili Simba sports club

Dripboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
3,178
Reaction score
4,609
Ni Beno Kakolanya. Hakuna ubishi kuwa huyu ni moja ya makipa wenye uwezo mkubwa nchini na tunaamini akishirikiana na wenzake katika kikosi chetu watatuwezesha kuongeza ukubwa wa timu na kutupatia mataji msimu ujao. Tumeshamalizana nae kwa mkataba wa miaka miwili. #NguvuMoja
 
Simba ni mahari fulani pa kuzika vipaji vya wachezaji! Benno asipokuwa makini tutamsahau mapema tu! Wapi Kwasi, Mbonde, Mo Ibrahimu, Salamba, Nduda.....Kila la kheri Benno Maisha popote! Ila msije mkapifana misumari na mwenzako.
Napingana na wewe. Tatizo la hao Wachezaji wamejisahau na hawataki kujituma. Mbona Haruna amerudi vizuri kwenye kiwango chake?!
 
Simba ni mahari fulani pa kuzika vipaji vya wachezaji! Benno asipokuwa makini tutamsahau mapema tu! Wapi Kwasi, Mbonde, Mo Ibrahimu, Salamba, Nduda.....Kila la kheri Benno Maisha popote! Ila msije mkapifana misumari na mwenzako.
wenyewe wanasema Azam ndio inaua vipaji!
 
Simba ni mahari fulani pa kuzika vipaji vya wachezaji! Benno asipokuwa makini tutamsahau mapema tu! Wapi Kwasi, Mbonde, Mo Ibrahimu, Salamba, Nduda.....Kila la kheri Benno Maisha popote! Ila msije mkapifana misumari na mwenzako.
Kweli mkuu simba ndo mahali pa kuzikia vipaji...watu kama samatta na wengineo vipaji vyao vilizikiwa simba 😂 😂 😂
 
Mpaka dirisha la usajili linafungwa kila siku saa saba mchana tunaonyesha mchezaji mmoja aliesajiliwa au kuongeza mkataba.
Bado hatujaenda kwa wachezaji wa kigeni sass...
 
Atasugua bench huyo
Wachezaji wa leo, hawaangalii sana kucheza ama mataji. Kipaumbele chao ni pesa. Hivyo simlaumu sana Beno amefanya uamuzi sahihi kwa wakati sahihi. Lunyamila alicheza haswa leo hii maisha yamempiga.

Ndio maana Oscar katika umri wa miaka 25 alihama zake Chelsea na kwenda zake China kuvuna PESA.
 
Ni Beno Kakolanya. Hakuna ubishi kuwa huyu ni moja ya makipa wenye uwezo mkubwa nchini na tunaamini akishirikiana na wenzake katika kikosi chetu watatuwezesha kuongeza ukubwa wa timu na kutupatia mataji msimu ujao. Tumeshamalizana nae kwa mkataba wa miaka miwili. #NguvuMoja
Tusubiri aanze kugombea namba na Manula. Mwenzake kapewa miaka mitatu.
 
Back
Top Bottom