Beno Malisa atenguliwa Ukuu wa Mkoa wa Tabora, Angeline Mabula achukua nafasi yake

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

1. Bi. Angeline Lubala Mabula ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Bi. Mabula anachukua nafasi ya Bw. Beno Morris Malisa, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

2. Bw. Dunford George Mpelumbe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu, ambaye amemaliza muda wake.

3. Bw. Omar Ali Omar ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar. Anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Khamis Hamad, ambaye amemaliza muda wake.

Uapisho wa viongozi wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Screenshot 2026-10-28 173913.png
 
Kuteka, kuua wapinzani na kutengua/kuteua ndiyo kazi anayoiweza tu. Kikwete katuachia msala mzito sana.
 
Ukiwa kada wa CCM utakula nchi mwanzo hadi mwisho utakapokufa. Huyu alikuwa benchi kitambo tu, sasa ameula tena kwa mara nyingine. Wanaccm mwendo ni kula mema ya nchi tu kwa kwenda mbele kana kwamba nchi hii ni ya wana ccm pekee. Teua hata jitu la upinzani likawe RC, DC, RAS, DAS na nyadhifa zingine wananchi wote wale matunda ya nchi yao, si mpaka maridhiano ya siasa za vyama yaje, hata sasa teua tu mtu akatae mwenyewe
 
Hiyo ni Tume ya haki za binadamu gani? Mbona haisikiki hizo haki za binadamu zikikiukwa kama ilivyo kwa THRC ya akina Henga!

BTW: Wabunge wa CCM waliotemwa kura za maoni 2025 jiji la Mwanza wana ngekewa!!

Gambo aache nongwa ale uteuzi!!
 
Back
Top Bottom