Berghahn Journal ya Ujerumani inaandika, viongozi wa Afrika wapigania Uhuru walikuwa na akili sana kuliko kizazi kilichofuatia baada ya uhuru

mockers

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
12,843
Reaction score
35,442
Kutoka kwenye jarida hilo
Wanasema kuwa Afrika kutoendelea ni sababu ya viongozi kutokuwa na uwezo mkubwa wa kiakili ilihali wamelalia rasilimali lukuki.

Jarida linasema wapigania uhuru wengi walikuwa ni watu wenye akili kubwa na maono makubwa na nchi zao kuliko viongozi wa sasa ambao wao wameyarudisha nyuma sana mataifa yao.

Wamezungumzia kutamalaki Kwa rushwa miongoni mwa viongozi na kuwafanya wagawe rasilimali za mataifa yao bila uwiano kwenye mikataba.

Lakini pia wamegusia mikopo isio na tija Kwa mataifa ya afrika ambayo waafrika hulazimika kulipa Kwa muda mrefu sana hivo nchi za Afrika kujikuta wanatumia karne nyingi kulipa madeni ambayo riba zake hua ni za kinyonyaji.

Nimetafakari sana hayo mambo waliyoandika nikaona bado tuna safari ndefu sana.
 
"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa WATU WEUSI katika mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake ni kwa sababu HAWANA AKILI NZURI, endapo kama tungewajumuisha, basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."

Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za Utawala wa ubaguzi wa rangi.

[Emphasis is added]
 
Hilo lipo wazi sana.
 
Hawa wa leo hawana tofauti na Kenge manyoya mnyama anayekula mkia wake mpaka anaanguka na kufa.
 
Kweli tupu, Africa inaongozwa na wajinga haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…