johnthebaptist Tego huwa lina sifa zipi?
Maana mwezi uliopita kuna mwili wa binti ulisusiwa na wana ukoo kuuzika wakidai ana Tego, nilitaka kujitosa mimi ili kuuchukua mwili wa marehemu nikatamani nipate japo wana ukoo hata watu au wanne ili tubembe gharama za mazishi, lkn tulipingwa mkwara hatari na wana ukoo, mwisho wa siku nikawa mimi na mama mdogo tu na yeye ni mama wa nyumbani, ikabidi tuache ila niliumia sana mwana ukoo kuzikwa na Serikali kisa ana Tego.
Je Tego ni kitu gani hasa na je ni kitu halisi au ni woga kwa watu wasio na imani katika Mungu wa mbinguni tu?