TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Tanzania ndio nchi pekee mwanasiasa hatakiwi kufa, akifa anatafutwa mtu wa kubebeshwa lawama. Hapo bado hujaongeza kwamba wao hawashtakiwi, hata wakipata ajari tunafichwa, hata wakiumwa hatuambiwi, wakiiba hela wanatakiwa wajifikirie.
Nchi ya ajabu hii
 
Kama Taifa tunatakiwa tutoke kwenye siasa hizi za chuki zilizozalishwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Baada ya Uchaguzi ule na John Pombe Magufuli kuingia madarakani, kulitokea uhasama mkubwa sana kati ya watu waliokuwa wanamuunga mkono na wale waliokuwa wanapingana na staili yake ya utawala.

Leo Baada ya kutangazwa kwa Kifo cha Bernard Camilius Membe, unaona kabisa limeibuka kundi la watu humu JF ni kama wanahanikiza furaha yao kwa kifo cha Membe. Watu hao ambao wanajificha nyuma ya kuonesha furaha kwamba Cyprian Musiba hatalipa tena hela alizotakiwa kumlipa Membe, lakini kwa undani unaona kinachowafurahisha zaidi ni kuona mmojawapo wa wapinzani wa Magufuli naye Kafariki.

Wakumbuke kwamba ni wao waliokuwa wanasema wakati wa msiba wa Magufuli kwamba "hakuna atakayeishi milele" na Leo ni ushahidi mwingine kwamba hakuna atakayeishi milele.

Watu wafanye maridhiano dhidi ya nafsi zao!!
Moja moja .Tuanze upya.
 
Nape Nauye, waziri wa habari, tayari amekaangwa na Mungu mbele ya macho yake kutokana na lugha zake chafu alizowahi kuzitoa baada ya kifo cha Rais Magufuli. Kauli ya kwamba Mungu ameamua ugomvi ilionekana wazi alishangilia msiba wa Rais wetu. Leo na yeye Nape ameonyeshwa namna ambavyo Mungu ameamua ugomvi wa Memba na Cyprian.

Bado Zito Kabwe, kwani na yeye ni mmoja wa waliotoa lugha chafu kwa hayati Magufuli kwamba anayempenda akazikwe naye. Zito Kabwe atashuhudia ukuu wa Mungu mbele ya macho yake.

Watanzania ni wale watu wanaosubiria tukio litokee halaf waongezee mashtaka yao as if Mungu wanaishi nae mtaa mmoja, yaani wamejipa jukumu la kumsemea Mungu.
So pathetic, lakini watanzania wote
 
Nape Nauye, waziri wa habari, tayari amekaangwa na Mungu mbele ya macho yake kutokana na lugha zake chafu alizowahi kuzitoa baada ya kifo cha Rais Magufuli. Kauli ya kwamba Mungu ameamua ugomvi ilionekana wazi alishangilia msiba wa Rais wetu. Leo na yeye Nape ameonyeshwa namna ambavyo Mungu ameamua ugomvi wa Memba na Cyprian.

Bado Zito Kabwe, kwani na yeye ni mmoja wa waliotoa lugha chafu kwa hayati Magufuli kwamba anayempenda akazikwe naye. Zito Kabwe atashuhudia ukuu wa Mungu mbele ya macho yake.
Hakuna jiwe halitogeuzwa. Kila mtu atalia kwa lugha yake na maumivu yake ndipo watakapo sema heri wafu wafao ktk Bwana. Waliodhani wamesha mzika sasa wanajizika wakiwa hai hofu imetanda kila kila mahali nawale wanahaha kutoa roho za wenzao ili madudu yao yasijulikane wakae mkao wakula... Nimwendo wa wali maharage...
 
Back
Top Bottom